6 TWA’SIFU Mungu kwa ajili ya damu takatifu
1. Twa’sifu Mungu kwa ajili ya damu takatifu,
Inayotosha kuonda makosa yetu yote. [br]
2.Wakristo wanakusanyika karibu ya kisima,
hawapunguki kitu kanwe, wakaa kwa Mwokozi. [br]
3. Tuimbe duniani pote juu ya pendo kubwa,
kwa kuwa tumefunguliwa kisima cha Golgotha ! [br]
4. Kisima hicho : Yesu kristo : na maji damu yake.
Wasumbuka Wastarehe, Waburudishwe hapa! [br]
5. Na wanye dhambi wanaitwa kwa wingi wa rehema,
Na wakosaji na maskini wasaidiwa sana. [br]
6. Tumeipata tunu kubwa, Neema kwa neema.
Apokeaye fungu lake, Ni mtu wa uheri. [br]
7. Heleluya! Tuna’himidi Mwenyezi na Mwanawe
Na Roho takatifu pia. Haleluya! Amina.