321 Mwokozi mzuri ni Yesu Kristo, ninamshukuru sana

1. Mwokozi mzuri ni Yesu Kristo, ninamshukuru sana. Alinitafuta kwa njia mbaya, ni mali ya Yesu Mwana.

Pambio:
Kwa damu nafunguliwa, kwa damu nafunguliwa. Alitoa yote kwa mimi na wote, kwa damu nafunguliwa.

 

2. Alibeba dhambi msalabani, alitukomboa sote. Barua za deni na mashitaki, alizipasua zote.

 

3. Ni heri kujua makimbilio, wakati wamajaribu. Nashinda kwa nguvu ya damu yake, asanti Mtakatifu.

 

4. Aliteswa sana kwa Getsemane, uchungu aliunywesha. Lakini kwa mwisho msalabani, alisema imekwisha.

Missionnary

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

HTML Snippets Powered By : XYZScripts.com