189 UNIHUBIRI habari njema

189

1.Unihubiri habari njema, neno la ukombozi, hata ikiwa siufahamu wingi wa wema! Nilipokuwa katika giza, ndipo Mwokozi alinijia, na akanipa wokovu, raha na tumaini.

Pambio:
Mimi kipofu, naona sasa, anasikia maombi yangu, naye hatanisahau, kwani ananipenda.

 

2. Amefungua mkono wake, kuna wokovu humo; ukilemewa moyoni mwako, uje kwake Yesu! Uliyechoka kwa dhambi zako, umtazame Mwokozi wako, na utapata wokovu, njoo, anakupenda.




190 KISIMA cha lehi kingali

190

1. Kisima cha Lehi kingali kwa kila aliye na kiu. Kinatoa maji mazima yaliyo ya kuburudisha.

Pambio:
Kisima chema cha maji safi hakikauki hata milele. Ni heri yangu, napumzika, na roho yangu inatulia.

 

2.Ulie na kiu rohoni, ukinyong’onyea njiani, tazama kisima jangwani kilicho na afya, uzima!

 

3. Mtungi ukiwa mtupu, ukipungukiwa imani, ufike kisima cha maji yabubujikayo daima!

 

4.Na penye kisima cha lehi upange na kupumzika! Uketi kivulini mwake, na moyo utaburudishwa!

Ida Björkman M et T




191 YAPIGWA hodi kwangu

191

1. Yapigwa hodi kwangu, mgeni a’fika, akiniomba: “Nifungulie! Umande umeshuka kichwani usiku, na nywele zangu zimelowa maji”.

 

2. A! Huyu si mgeni, ni Yesu Mwokozi, sauti yake nzuri na’jua. Ninamfungulia, naona ni Yesu; na siku hiyo sitaisahau.

 

3. Anong’oneza sasa rohoni: “U wangu”, karibu naye ninatulia. Ananitia nguvu, baraka ya mbingu; daima nitakaa kwake Yesu.

 

4. Ni kweli, mimi ni wa Mwokozi milele, amenitaja: “Ndugu, mpenzi”. Ananikarimia hazina za mbingu, ninaingoja siku ya arusi.

Fr. Schibboleth. arr L.P




192 SAUTI moja iliniuliza

192

1. Sauti moja iliniuliza: ” Wajua nilikufanyia nini? :/: Kwa’jili yako niliteswa sana; ufike kwangu, kwani nakupenda! ” :/:

 

2. ” Nilipokuwa huku duniani wakanitia taji ya miiba, :/: Na sikupambwa fedha na dhahabu, lakini majeraha na uchungu.” :/:

 

3. ” Golgotha nilifika siku moja, na nilikufa ju’ ya msalaba. :/: Tazama, katika mikono yangu nimekuchora, e’ mtoto wangu.”:/:

 

4.Heleluya, rohoni ninaimba! Nimejiweka mikononi mwake. :/: Na Yesu ananiongoza sasa, nifike nchi nzuri huko juu. :/:

K.E. Svedlung




193 NINENO zuri la ‘aminiwa

193

1. Ni neno zuri la ‘aminiwa, listahililo kukubaliwa, ya kwamba Yesu alitujia awaokoe wenye makosa.

 

2. Wa kwanza mimi wa wenye dhambi, lakini ninafurahi sasa sababu Yesu, Mwokozi wangu, aliniosha kwa damu yake.

 

3. Mwokozi wetu yu nasi hapa, atenda kazi kwa nia yake; awasha moto rohoni mwetu, uwezo gani utampinga?

 

4. Viziwi wanasikia sasa, viwete wanatembea sawa, wenye ukoma watakasika, Injili yake yahubiriwa.

 

5. E’ Bwana Yesu, tupulizie, tujaze Roho Mtakatifu! Uwaamshe waliokufa katika dhambi, uwaangaze!

 

6. Fungua mbingu unyeshe mvua panapo kiu na jangwa tupu! Uligeuze, likachanue na kufurahi kwa shangwe kuu!

 

7. Na mataifa wakusujudu mahali pako patakatifu! Amina. Wako ni utukufu na sifa zote! Haleluya!

Joel Blomkvist, 1876




194 USIKIE Bwana Yesu anakuita leo

194

1. Usikie Bwana Yesu anayekuita leo! Aliteswa, alikufa kwa ajili yako wewe.

Pambio:
Usikie Bwana Yesu! Anabisha mlangoni. Umfungulie moyo, umkaribishe sasa!

 

2. Siku zote ulicheza, kupendeza mwili wako; ulimsahau Yesu, naye alikufilia.

 

3.Unasema: “Nitakuja kusikia neno lake”. E’ rafiki, ukumbuke, unaweza kufa leo!

 

4. Yesu akuita leo kwa neema na upendo. Leo siku ya wokovu, umfungulie moyo!

 

5. Tunampa Bwana Yesu moyo na wakati wetu. Yeye ni Mfalme wetu wa milele na milele.

 

C.C. William/ D.W. Whittle, 1878
Have you any room for Jesus, R.S. 122; R.H. 362




195 TUNASIKIA leo habari

195

1. Tunasikia leo habari, inawaita watu wafike; watu wa hapa, watu wa mbali, wote wapate sasa wokovu!

 

2. Mtu wa dhambi uje upesi, Yesu angoja kukuokoa! Tena kwa nini unachelewa? Leo ni siku ya kuokoka.

 

3.Ulikimbia Yesu Mwokozi aliyekukomboa kwa damu. Usikimbie mbali zaidi, ila urudi, uje upesi!

 

4. Katika dhambi hutaiona raha halisi, hata kidogo. Yesu mwenyewe atakujaza raha ya kweli ndani ya roho.

 

5. Mtu wa heri katika shida, katika mambo yote ya huku, ni hali ya mkristo wa kweli, mtu wa heri hata milele.

T. Joseph Grytzell, 1891




196 USIEIFANYA bidii kabisa

196

1. Usiyefanya bidii kabisa, hutaingia mbinguni. Uikinge roho kwa neno la Mungu, usipotee milele! Njia ni nyembamba na mlango ‘dogo, ujitahidishe kuingia humo! Ukubali leo wokovu wa Mungu ili ufike mbinguni!

 

2. Vizuio vingi katika safari, mwovu anakujaribu. Uvishinde vyote vinavyozuia, vyote katika dunia! Usimfuate kila aitaye, ungeweza kupoteza roho yako! Bwana Yesu anakupenda daima; ujitahidi kabisa!

 

3. Pasipo imani huwezi kufika hata bandari salama wala kuingia katika uzima; hilo ni neno la Mungu. Kwa imani tupu utaokolewa, usikie sasa neno la wokovu! Tubu dhambi zako, amini Mwokozi; hiyo ni njia, hakika.

 

4. Mungu anaita, wo wote wafike, waupokee uzima! Atakupa nawe hazina ya mbingu, ukitafuta kwa kweli. Mungu Baba anapenda roho yako, Yesu anataka kuokoa wewe, Roho ‘takatifu anakuamsha.

 

Ukiitika u heri! T. Lars Linderot, 1798




197 HAPO nilipokua dhambini

197

1. Hapo nilipokuwa dhambini, niliumwa kwatika roho. Sasa ninafurahi kwa shangwe kwani Yesu ameniponya.

Pambio:
Ndiyo kazi kubwa ya ajabu: Mwokozi aliniokoa! Naye anapenda watu wote, atakuokoa wewe.

 

2. Dhambi zote nilizozitenda zimefutwa na Bwana Yesu. Sikitiko kwa ‘jili ya dhambi zilikoma nilipotubu.

 

3. Sasa mimi sitaki kurudi, nachukia kabisa dhambi. Nimeonja furaha ya Mungu na amani na raha yake.

T. Allan Törnberg




198 E’MTU mwenye kiu

198

1. E’ mtu mwenye kiu, ufike kwake Yesu, :/: upate maji ya uzima, hutaona kiu kamwe!

Pambio:
:/: Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!

 

2.Na tazama, ndugu wengi wamekwisha kunywa! :/: Ni heri kubwa, maji hayo hayatakauka kamwe! :/:

 

3.Na wewe unywe pia, upate nguvu sana! :/: Tumia katika shindano upanga wa neno lake! :/:

 

4.Na mwendo wa imani uta’poumaliza, :/: utayakunywa maji bora m kwa Mungu mbinguni juu. :/:

 

T.B. Barrat




199 NJONI wote muteswao

 199

1. Njoni wote mteswao! Wote wenye sikitiko kwa ajili ya makosa, mje sasa kwa Mwokozi! Kwake mtaona raha, utulivu na amani. Matulizo mioyoni mtapata kwake Yesu.

 

2.Hataacha sikitiko kulemea moyo wako; Yesu ni mchunga mwema, akuficha mazizini. Pendo lake lina nguvu, huchukua masumbuko, hufariji roho yako, hukutwaa kwake Mungu.

 

3. Yesu kama nyota nzuri ing’aayo asubuhi, mtu amfuataye ataona njia wazi. hata nyota za mbinguni zikiteketea zote, nyota hiyo ya milele haitazimika kamwe.

 

Tune: Who can cheer the heart like Jesus, R.H. 518; MA. 490




200 NJONI wote

200

1. Njoni wote, mle, mnywe, Yesu anasema hivyo. “Nimetoa mwili wangu kwa ajili yenu ninyi.” Kila mtu mwenye njaa aje na apate kula! Na aliye na makosa atasamehewa yote.

 

2.Ninakuja kwako, Yesu, unithibitishe moyo! Uliona umaskini, niwe mwenye uta-jiri. Nishibishe mema yako na karama takatifu! Unijaze Roho yako kama ulivyoahidi!

 

3. Yesu, ninakuja kwako niungane nawe, Bwana! Mimi mwenye udhaifu, nakutegemea wewe. Na kwa damu yako, Yesu, ninatakasika sasa. Nashiriki mwili wako katika agano jipya.

Tune: Who can cheer the heart like jesus, R.H. 518; MA. 490




201 NJO mwenye huzuni nyingi

201

  1. Njoo, mwenye huzuni nyingi! Yesu anakungoja. Uje, atoe mzigo wako, ata’okoa wewe!

Pambio
Njoo, uliye na huzuni! Njoo kwa Mungu wa neema! Roho wa Mungu anakuita, Yesu anakungoja.

 

2. Njoo, mwenye makosa mengi! Yesu anakungoja. Kwake neema na upendo tele! Ata’okoa wewe.

 

3. Njoo, leo uache dhambi! Yesu anakungoja. Ukilemewa moyoni mwako, uje kwa Yesu mbio!

 

4. Njoo, sasa, E’mwenye dhambi! Yesu anakungoja. Na ukitaka kumfuata, ata’okoa wewe.

Georg Fr. Root




202 NJOO kwa Yesu Mwokozi

202

1. Njoo kwa Yesu Mwokozi, unayeteswa rohoni! Damu iliyomwagika itakuosha kabisa.

Pambio:
Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.

 

2. Mbona kukawa dhambini bila uzima wa Mungu? Uje upesi kwa Yesu ili upate amani!

 

3. Saa zapita upesi, hazitarudi kabisa. Bado kidogo na tena utapelekwa kuzimu.

 

4. Yesu atamchukua bibi-arusi mbinguni, na tutaimba milele sifa za Mwana-kondoo.

Pambio
Huko karibu na Yesu, mbali ya mambo ya nchi, huru na heri rohoni nitafurahi milele!

T.B. Barrat




203 HATUA moja kati ya wewe na Mwokozi

203

1.Hatua moja kati ya wewe na Mwokozi. Wakawilia nini? Ufike kwake leo!

Pambio:
Hatua moja, hatua moja, njoo akungoja! Njoo kutubu dhambi, atasamehe zote! Usikatae tena wokovu wake Mungu!

 

2.Hatua moja mbele, anakungoja sasa. Amini neno lake, na utapata raha!

 

3.Hatua moja mbele, uzima uta’ona. Siku si nyingi huku, ‘jitoe kwake Mungu!

 

4.Hatua moja mbele, kwa nini kukawia? Omba: E’ Bwana Yesu, unipokee sasa!

Fanny J. Crosby




204 PENDO la Mwokozi kubwa mno

204

1. Hatua moja kati ya wewe na Mwokozi. Wakawilia nini? Ufike kwake leo!

Pambio:
Hatua moja, hatua moja, njoo akungoja! Njoo kutubu dhambi, atasamehe zote! Usikatae tena wokovu wake Mungu!

 

2. Hatua moja mbele, anakungoja sasa. Amini neno lake, na utapata raha!

 

3. Hatua moja mbele, uzima uta’ona. Siku si nyingi huku, ‘jitoe kwake Mungu!

 

4. Hatua moja mbele, kwa nini kukawia? Omba: E’ Bwana Yesu, unipokee sasa!

Fanny J. Crosby




205 YESU Mwokozi aita kwapendo mimi na wewe na wote

205

1. Pendo la Mwokozi kubwa mno! Yesu akuita, ufike kwake sasa!

Pambio:
:/: Anangoja, anabisha, ufungue!:/:

 

2. Amengoja wewe siku nyingi, analia sana juu ya dhambi zako.

 

3. Kwa huruma nyingi akuita. ‘Geukie Mungu, anakungoja sasa!

 

4. Yesu atakupa raha kubwa na uzima tele ulio wa milele.

Armée du Salut.




206 RAFIKI yangu tazama

206

1. Rafiki yangu, tazama, wapita njia ya wapi? Milele, je? utakaa wapi ukikataa Mungu?

Pambio:
Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari
kwa sababu utamuona!

 

2.Dunia haina raha, amani wala salama. Fahari yake ikikuloga, utapotea njia.

 

3. Lo! Yesu anakuita! Kwa nini unachelewa? Ushike njia ufike kwake! Ataja jina lako.

 

4.Uache haya na hofu, Mwokozi anakupenda! Kwa damu alikomboa wewe, anakutaka sasa.

 

5.Ikiwa unachelewa kupatanishwa na Mungu, utamkuta Mwokozi kama mwamuzi mwenye haki.

Oscar Hallof, 1921




207 UMGEUKIE Mwokozi

207

1.Umgeukie Mwokozi, jitenge na ovu na dhambi! Babako angoja ufike; usiangamie milele!

 

2. Kijana, unafurahia maisha na mambo ya nchi. Baada ya muda kitambo utahukumiwa na Mungu.

 

3. Kwa nini kujiangamiza katika tamaa za huku? Usijipoteze dhambini! Dunia isikuharibu!

 

4.Umkimbilie Mwokozi, atakupokea kwa pendo, na utaokoka hakika kwa nguvu ya damu ya Yesu!

 

5. Walio mbinguni waimba, wanayo mavazi meupe; hutaki sehemu pamoja na wao nyumbani mwa Baba?

 

6. Je, mwisho utaona wapi mahali pa kujisitiri? Dunia itakapochomwa utakosa makimbilio.

 

7. Ujipatanishe na Mungu, na usichelewe, rafiki! Ukimkataa Mwokozi, utatupwa nje gizani.

 

8. Chagua pasipo kukawa! Mwokozi atakupokea. Angoja ufike kutubu; atakutakasa kwa damu.




208 PIGA makengele ya furaha leo kwa sababu mutu ametubu

208

1. Piga makengele ya furaha leo kwa sababu mtu ametubu! Mwana mpotevu amerudi sasa, baba amemsamehe yote.

 

2.Nyimbo za furaha ya mbinguni, Nyimbo za furaha ya wakristo! Tuna’sifu Mungu kwa sababu sasa mtu huyu amwamini Yesu.

 

3. Piga makengele, ni furaha nyingi; mkosaji amefunguliwa! Yesu alivunja minyororo yake, alimpa roho ya kimwana.

 

4. Piga makengele! Hiyo ni habari yakupasha mbali na karibu. Mtu amepata kuwa mtu mpya, dhambi zake zimeondolewa!

W.O. Crushing




209 UWATAFUTE wanao potea

209

1. Uwatafute wanaopotea, na kwa upendo watoe dhambi! Lia pamoja na wenye huzuni, uwapeleke kwa Yesu Mwokozi! Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.

 

2. Anatafuta waliokimbia, anawangoja warudi upesi. Uwafundishe kwa pendo na kweli ju’ ya neema na haki ya Yesu!

 

3.Ndani ya roho na katika siri labda waona shauku ya Mungu. Uwaongoze kwa Yesu Mwokozi, wafahamishe upendo wa Mungu!

 

4.Uwatafute wanaopotea! Mungu atoa upendo na nguvu. Uwapeleke kwa Yesu mpozi, Mwenye huruma na afya kwa wote!

Fanny Crosby, 1869
Rescue the perishing, R.S. 345; R.H. 561 




210 IMBA injili ya Yesu kwa moyo na roho kabisa

210

1. Imba injili ya Yesu kwa moyo na roho kabisa! Lango la neema yake ni wazi kwa watu wote.

Pambio:
Imba, imba injili, na watu wasikilize! Imba injili ya Yesu, maneno ya pendo lake!

 

2. Imba injili ya Yesu! Yaleta uhuru kwa wote. Imba habari ya damu inayotakasa moyo!

 

3. Imba injili ya Yesu, kwa wimbo utawafundisha! Imba habari ya Yesu! Aweza kuwaokoa.

 

4. Imba injili ya Yesu, na raha na matumaini! Imba habari ya haki, wapate kujua Mungu!

 

5. Imba injili ya Yesu, hubiri amani kwa wote! Na tumsifu Mwokozi afanyaye yote vema!

Philip Philips, 1877




211 NJOO kwa Yesu

 211

1. Njoo kwa Yesu, usishangae! Akuonyeshe njia ya mbingu. Msikilize, anakusihi: Mtu wa dhambi, njoo!

Pambio:
Heri, heri, tutakusanyika kwake Mungu kwa furaha kuu! Shida na shaka hazitakuwa kwetu mbinguni juu.

 

2. Yesu aita, wote wafike, atatuliza wenye huzuni, kuwatolea pendo na raha. Usikiaye, njoo!

 

3. Sasa wakati wakuokoka, uje upesi, umkubali! Mwenye amsikitiko na dhambi, njoo kwa Yesu sasa!

G.F. Root, 1870
Come to the Saviour, R.S. 123; R.H. 308




212 SAUTI ya Yesu niliisikia

212

1. Sauti ya Yesu niliisikia, kwa pendo aliniambia: “Ufike, nataka kukusaidia, nangoja, nangoja, ufike!”

Pambio:
Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee wokofu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!

 

2. Ukiwa na hofu kufika kwa Yesu, uliye na dhambi rohoni, kumbuka ya kuwa huruma ni tele; ufike kwa Yesu, angoja!

 

3.Ukiwa maskini, dhaifu kabisa, Mwokozi anakufahamu. Anakuambia: ” Pokea neema, uache mzigo wa dhambi!”

 

4. Na kama nilivyo ninamfikia Mwokozi aliyenipenda. Ninaupokea wokovu na raha; kwa shangwe ninamshukuru!




213 KAMA unataka kuwa mtu wake Yesu

213
1. Kama unataka kuwa mtu wake Yesu, kama unataka kufuata yeye, kama unataka yeye akusaidie: Mpe Yesu moyo wako!

Pambio:
Ataondoa dhambi zako zote, na utaipokea nguvu yake! Ukiokoka utaona kwamba ni vizuri kufuata Yesu kweli.

 

2. Kama unataka kuwa mtu mwenye heri, ufungue moyo, Yesu aingie! Kama unataka utulivu na faraja, mpe Yesu moyo wako!

 

3. Kama unataka kumtumikia Yesu na kuifuata njia yake hapa, kama unataka kuingia huko mbingu: Mpe Yesu moyo wako!

C.S. Nusbaum
Would you live for Jesus. R.S. 574