214 NAMTAFUTA mwana wangu

214

1. Namtafuta mwana wangu, mtoto yu wapi leo? Alienifurahisha mbele, ningali ninampenda.

Pambio:
Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, mwanangu, mpendwa wangu!

 

2. Uliyekuwa safi sana katika utoto wako, uliichafua roho yako kwa dhambi na njia mbaya.

 

3. Ninatamani kukuona katika usafi tena, na kukusikia ukiomba na kumshukuru Yesu.

4. Nitafutie mpotevu kwa pendo na tumaini! Unisalimie mwana wangu, ya kwamba ninamngoja!

Robert Lowry, 1877
Oh, where is my wandering boy to-night.




215 MWENYEZI Mungu anafanya ishara kubwa Duniani

215

1. Mwenyezi Mungu anafanya ishara kubwa duniani, anaondoa minyororo inayofunga watu huku. Avunja nyavu za shetani, na wakosaji waokoka.

 

2. Maneno yake yana nguvu kushinda yote ya zamani. Na watu wanapiga mbio kuomba ne’ma ya Mwokozi. Wakiyapata masamaha, waimba wote: “Sifu Mungu!”

 

3. Tazama, ndugu wengi sana wanafuata Yesu leo; katika kila nchi sasa maelfu wanapenda Mungu. Wengine wanavutwa naye Mwenyezi Mungu, Baba yetu.

 

4.Inua macho, mvunaji, mavuno yanaiva sana! Uende kutafuta watu, uwapeleke kwake Yesu! E’ ndugu wote, amkeni, ‘kawaokowe wenye dhambi!

 

5. Wengine wanapoingia ufalme wako, Yesu Kristo, nisibakie huku chini, neema hiyo nakuomba! Nakaa mikononi mwako, unifikishe huko kwako!

 

6.Najua siku ni karibu Mwokozi atakaporudi, awachukue watu wake mpaka nchi ya amani. E’ siku ya uheri bora, nakutamani. Uje mbio.

Nils Frykman, 1877




216 NAFASI ingaliko arusini

216

1. Nafasi ingaliko arusini ita’yokuwa kwake Mungu Baba. Njoo kwake, nafasi ingaliko!

 

2.Njiani mwako jua linakuchwa, jioni inakaribia sasa. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

3. Karamu ya arusi ni tayari, na Bwana anakualika wewe. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

4. Wanaingia watu wengi huko, ufanye hima, uingie nawe! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

5. Tazama, lango limefunguliwa, neema gani: Utakaribikshwa! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

6.Ufike mbio, utaona heri, Yesu atoa wingi wa neema! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

7.Je, utaona shangwe ya mbinguni? Bwana arusi akungoja sana. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

8.Uliyesitasita unaitwa, ujiazimu kuja kwake Mungu! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

9.Ukichelewa, lango litafungwa, na utalisikia neno hili: “Ondokeni! Sikuwajua ninyi!”

H. Bonar




217 BWANA Yesu atakuja kutoka mbinguni

217

1. Bwana Yesu atakuja kotoka mbinguni, atawachukua wote wanaomwamini.

Pambio:
Kama nyota za mbinguni watu wake watang’aa katika taji yake, kuwa sifa ya Yesu.

 

2. Atawakusanya wote waliompenda, watakuwa tunu yake milele mbinguni.

 

3. Na watoto watakuwa pamoja na Yesu, watang’aa kama lulu nyumbani mwa Baba.

G.F. Root




218 MTOTO mimi ni maskini

218

1. Mtoto mimi ni maskini, lakini nafurahi kwa kuwa Baba yangu mwema ananitunza vema.

 

2. Babangu anipenda sana, anionyesha njia. Upendo wake unapita uzuri wa dunia.

 

3. Katika shida na huzuni naimba kwa furaha: “Nina makimbilio yangu kwa Mungu Baba yangu”.




219 HATUMUJUI rafiki mwema

 219

1. Hatumjui rafiki mwema, ila Yesu, ila Yesu; yeye mwenyewe atufahamu, yeye Bwana peke yake.

Pambio:
Yesu anatujua, pia Yesu anatuonya njia. Yesu rafiki kupita wote, wote, wote pia wa dunia.

 

2. Hatumjui rafiki mwema kama Yesu, Bwana Yesu. Na pendo lake ni la ajabu, linadumu siku zote.

 

3. Je, ataweza kutusahau? Hataweza ku’sahau. Twafarijiwa kwa pendo lake kila siku, kila siku.

 

4. Nani ashika agano lake? Bwana Yesu peke yake. Alikataa kusaidia? Hataweza kukataa.

 

5. Nani rafiki mpendwa wangu? Bwana Yesu peke yake. Anastahili kupata sifa huku chini na mbinguni.

Johnson-Oatman
There’s not a friend, RH. 110




220 YESU wewe U mchunga wetu

220

1. Yesu, wewe u mchunga wangu, twakuomba: Utulinde! Utulishe sisi kundi lako, tukashibe neno lako!

Yesu mwema, Yesu mwema, tushibishe kwa neema! Yesu mwema, Yesu mwema, tushibishe kwa neema!

 

2. Tuongoze kwa mapito yako hata maji matulivu! Tuhuishe roho zetu huko tukajazwe uhodari!

Yesu mwema, Yesu mwema, ututie nguvu yako! Yesu mwema, Yesu mwema, ututie nguvu yako!

 

3. Yesu, uwe nasi hata mwisho, tutakapokata roho! Tupeleke katika makao uliyotuandalia!

Yesu mwema, Yesu mwema, tufikishe hata kwako! Yesu mwema, Yesu mwema, tufikishe hata kwako!

W.R. Bradbury




221 E’MTOTO yainue macho yako mbinguni

221

1. E’mtoto, yainue macho yako mbinguni! Bwana Yesu huko juu, kwa upendo akuone.

 

2.Ukiomba asikia, akulinda mashakani; na anakuandalia kao zuri huko kwake.

 

3. Penda Yesu, mfuate, tii neno lake pia! Tena malaika wake watakuchukua kwake.




223 NI UHERI bora kumwamini

 223

1. Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu, kabla hatujazionja dhambi na mashaka zinazoharibu roho zetu.

Pambio:
Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu, na kumfuata kila siku. Na ujana wetu ukitukimbia tena, shangwe ya wokovu itabaki.

 

2.Ni uheri bora kumtii Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Hivyo tutakuwa na dhamiri safi, njema kwa maisha yetu yote pia.

 

3.Ni uheri bora kumtumikia Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Bwana Yesu akumbuka kila tendo dogo, atalipa kwa neema yake.

 

4.Ni uheri bora kumngoja Bwana Yesu kwa wakati wa ujana wetu. Atatuchukua kwake kwa furaha kubwa, tutakuwa naye siku zote.




224 YESU mwenye pendo kubwa

224

1. Yesu, mwenye pendo kubwa, usinipitie! Katika maombi yangu unibarikie!

Pambio:
Yesu, Yesu, unisikilie! Ukiwabariki wote, usinipitie!

 

2.Ninakiendea sasa kiti cha neema; kutoamini kwangu u’ondoe vema!

 

3.Nakutegemea, Bwana, njia unionye! Roho yangu imevunjwa, Yesu, uniponye!

 

4. Wewe, Yesu, ni kisima cha furaha yetu. Nani ni mchunga mwema, ila Bwana wetu! Frances J Crosby;

Van Alstyne, 1868




225 LO! bendera mbele yako

225

1. Lo! Bendera mbele yako, usihofu sasa! Usimame kwa imara kama Danieli!

Pambio:
Uwe mhodari kama Danieli! Weka makusudi mema bila kuogopa!

 

2. Wenye hofu hawawezi kuingia mbingu. Tweka tu bendera yetu, endelea mbele!

 

3. Mashujaa wa shetani wangeshindwa sana wakikuta jeshi la askari wa imani.

 

4. Endelea kwa kushinda, Yesu ni Mfalme! Taji ya uzima utapata huko juu.




226 MACHO yangu ya kumtazama

226

1. Macho yangu kumtazama, masikio yakumsikia, na miguu yakumfuata Yesu, rafiki yangu!

 

2. Roho yangu inapenda Yesu, na ulimi unamshukuru, kwa mikono namtumikia Yesu, rafiki yangu!




227 MUNGU aliye mbinguni alitupa kiongozi

227

1. Mungu aliye mbinguni alitupa kiongozi, naye ni rafiki wa watoto wote. Ukijua jina lake, ulitaje sasa hivi! Anapenda wote, hata wewe, nami.

Pambio:
Mbingu na ufalme wake wa wototo wote sasa! Mbio tuishike njia iendayo kwake Yesu ili tuione raha ya mbinguni!

 

2. Yesu mwenye pendo kubwa awakumbatia wote, anawabariki kwa huruma yake. Hatuoni huku chini mtu mwema kama yeye, hasahau mtu, hata mnyang’angyi.

 

3. Yesu ni Mchunga mwema, anawakusanya sasa mkononi mwake wana wa kondoo. Kifuani mwake tena anawachukua wote hata kwa ufalme wake huko juu.




228 WAKATI wa utoto wako

228

1. Wakati wa utoto wako, hujapoona shida bado, sauti ilikuambia: “Unipe sasa moyo wako!”

Pambio:
Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: ” Njoo kwangu!”

 

2. Na katika ujana wako wausikia mwito wake, na jinsi utakavyoshinda shetani akikujaribu.

 

3. Wakati wa uzee wako dhambini ukiendelea hata kukaribia kufa, Mwokozi akuita tena.




229 MWOKOZI Mfalme, ulisulubiwa

229

1. Mwokozu Mfalme, ulisulibiwa, e’pasaka wetu, ulidhihakiwa. Ukatoka damu, ‘kaona uchungu ulipotimiza mapenzi ya Mungu. Huku Gethsemane ulihuzunika, kwa neno la mbingu ukafarijika. Katika kuomba ukatiwa nguvu, na mwisho ukafa tupate wokovu.

 

2. Kwa ‘jili ya mimi ulijeruhiwa, ukaonja kufa, nipate uzima. Ulijisahau, ukanikumbuka, uliwaombea waliokutesa. Na ulijitoa dhabihu ya kweli, na kuusikia uchungu mkali. Kwa pendo kamili ulikusudia kuonja mauti kwa ‘jili ya wote.

3. Je, kupatanishwa na Mungu ni nini? Ni kwamba laana la dhambi lakoma. Kufika karibu na Mungu ni nini? Ni kuwa rafiki wa Mungu wa mbingu. Na sasa ufike kutoka dhambini, utie hatia na dhambi nuruni! Mwokozi mpendwa akuhurumia, atakufungua na ‘kusaidia.

Fr. E. Falk




230 GOLGOTHA Mwokozi alitundikwa mtini

230

1. Golgotha Mwokozi alitundikwa mtini kwa’jili ya wote. Na damu akaitoa Mwokozi ili kutangua dhambi.

Penye msalaba nilikombolewa kwa damu ya Yesu iliyotolewa. Mwamuzi mwenyewe alinikomboa, akanilipia deni.

 

2. Golgotha nami nimesulibiwa pamoja na Yesu Mwokozi; na njia kwa Mungu Baba ni wazi, pazia limepasuka.

Nimesulibiwa pamoja na Kristo, na mtu wa kale alikufa hapo. Na mambo ya kale yamekwisha’pita, lo! yote ni mapya sasa!

 

3. Niliunganishwa naye Mwokozi, na sasa ni hai kwa Mungu. Kuishi ni Kristo, siri ajabu, na kufa faida kwangu!

Kwa damu ya Yesu nimetakasika, hatia na dhambi zimeondolewa. Shetani hawezi kunidhuru tena, nimewekwa huru kweli.

Henrik Schlager, 1870-1934




231 MWOKOZI alitoa damu kwa’ jili ya waovu

231

1. Mwokozi alitoa damu kwa’jili ya waovu, msalabani alikufa kuniokoa mimi.

Pambio
E’ Yesu, niokoe sana, nifunze kuamini! Na unilinde tena, Bwana, nisipotee kamwe!

 

2. Alijitwika dhambi zetu, huzuni na maradhi; neema kubwa, wema wingi, upendo wa ajabu!

 

3. Na hapo jua likafichwa, ikawa giza kuu; muumba alitufilia kutulipia deni.

 

4. Magoti yangu nayapiga msalabani pake, na kwa machozi natazama mateso yake huko.

 

5. Nitakurudishia nini, Mwokozi wangu mwema? E’ Bwana, nikutumikie maisha yangu yote!

Isaac Watts
O Lord, remember me




232 NILIPOFIKA kwa bwana Yesu

 232

1. Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikapaaza sauti yangu: “Yesu Mwokozi, unirehemu!” Akaniokoa.

:/: Yesu asifiwe! :/: Alisikia kilio changu, Yesu asifiwe!

 

2. Nilipofika kwa Bwana Yesu, nikamsihi Mwokozi wangu: “Unitakase, nifanye safi!” Akanisikia.

:/: Yesu asifiwe.:/: Alisikia maombi yangu, Yesu asifiwe!

 

3. Ona kisima cha msalaba, leo kingali chabubujika kuniokoa na kusafisha! Yesu asifiwe!

:/: Yesu asifiwe:/: Aniokoa, anisafisha, Yesu asifiwe!

 

4. Njoo kwa Yesu, kisima hicho, unywe, uoshwe katika maji! Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe.

:/: Yesu asifiwe! :/: Kiu yapoa, na watakaswa, Yesu asifiwe!

E.A. Hoffman, 1877
Down at the Cross, R.S. 192




233 TAZAMA Mwokozi aliekufilia

233

1. Tazama Mwokozi aliyekufilia ili wewe upate uzima! Tazama, kwa pendo atakusaidia, usidumu dhambini daima!

Pambio:
Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

 

2. Mwokozi alisulibiwa ju’ ya mti ili sisi tupate wokovu. Alitukomboa kwa damu yake safi, kwate yeye twapata wongofu.

 

3. Hakuna majuto yaweza’ kutuponya, ila damu ya Yesu Masiya. Ufike kwa Yesu apate kukuonya jinsi yaondokavyo hatia!

 

4. Rafiki, waitwa na Mungu kwa wokovu, anataka ufike upesi. Kwa nini kukawa, ufike bila hofu, uondoke katika hatari!

 

5. Ufike, pokea uzima wa milele, Bwana Yesu ali’tuletea! Karama ya mbingu ni tumaini letu, ipokee na hutapotea!

Amelia M. Hull, 1860




234 UTUKUFU wa mbinguni niwa heri na amani

234

1. Utukufu wa mbinguni ni wa heri na amani, dhambi hazitakuwamo. Vitu vyote vilivyomo ni vya tunu na thamani, dhambi hazitakuwamo.

Pambio
Dhambi hazitaingia mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia mbinguni.

 

2. Kama unatumaini kufikia nchi ile na kuona Bwana Yesu, utafute utakaso na kupata moyo safi! Dhambi hazitakuwamo.

 

3. Unaweza ‘tenda dhambi na kukana Bwana Yesu, walakini ukumbuke: Dhambi zako zitafunga lango la mbinguni, kwani dhambi hazitakuwamo.

 

4. Na ukiwa mkaidi hata sa’ ya kufa kwako, utaitwa hukumuni, na utaambiwa huko: “Ondokeni siwajui!” Dhambi hazitakuwamo.

Pambio:
Ukitaka kufikako mbingu ya utakatifu, tubu sasa, hacha dhambi, utafute moyo safi, na utaingia mbingu!

C.W. Naylor




235 TUMEKOMBOZWA katika nchi

1. Tumekombozwa katika nchi, usikilize vema, rafiki!
:/: Tumeokoka tufike juu, taji kutiwa, furaha kuu! :/:

 

2. Tumekombozwa katika watu, hata tuchekwe kitambo huku.
:/: Twavumilia katika shida, twatazamia ‘heri wa mbingu. :/:

 

3. Tumekombozwa, tuwe wa huru, tukichokozwa haitudhuru.
:/:Tutaondoka, ‘hamia mbingu, tutasimama mbele ya Mungu.:/:

 

4. Tumekombozwa, furaha kuu, twaandaliwa karamu kuu!
:/: Salamu hiyo uitangaze, wafike mbio na waokoke! :/:

 

5. E’ mama, baba, mbona kungoja? Ndugu na dada, fika pamoja!
:/: Mwenye kukawa hataingia, leo waitwa na Yesu pia. :/: R.

Edhelgerg




236 DHAIFU mwenye dhambi

236

1. Dhaifu, mwenye dhambi, nilipotea njia, lakini Bwana Yesu alinihurumia. Nategemea yeye, najua pendo lake, ajaza roho yangu, ninavyo vyote mwake.

Pamio:
Ajaza roho yangu, apita vitu vyote. Amani na upendo ni zangu siku zote. Ajaza roho yangu, neema kubwa kwangu! Namhimidi Yesu: Yu yote ndani yangu.

 

2. Sitaki dhambi tena, haiku’faidia; rafiki yangu, Yesu, ananisaidia. Alitangua dhambi kwa msalaba wake, kwa yeye ukombozi, na vyote vimo mwake.

 

3. Napenda kufuata daima nyayo zake, nibadilishwe sana, nifananishwe naye! Na tena siku moja atanikaribisha nyumbani mwake Baba, na atanijaliza!

Otto Witt




237 MWOKOZI wangu ni mwamba bora

237

1. Mwokozi wangu ni mwamba bora, ahadi kama milima; zaniletea amani tele, na mibaraka daima. Katika mwamba ni raha kuu, baraka tele kutoka juu. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

2. Makimbilio ni mwamba huo katika teso lo lote; Nisikimbie adui ‘kuu, nishinde katika vyote! Dunia yote ikitingika, ahadi zake hazipunguki. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

3. Nakaa mbali ya udhalimu, hatia, dhambi, hukumu. Na kwa imani nikisimama, adui atakimbia. Nayo mawazo ya giza tupu hayatapata nafasi huko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

4. Nafurahia baraka zote za ulimwengu wa roho. Karama hizo nalizipewa katika kufa kwa Yesu. Hakuna woga na shaka huko, hayatakuwa manung’uniko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

Otto Witt




238 NIFANANISHWE nawe mwokozi

238

1. Nifananishwe nawe Mwokozi, ni haja yangu iliyo kuu. Ninakuomba, na kwa machozi, nikufuate, Bwana wa juu!

Pambio:
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye upendo, safi halisi! Unitakase, unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!

 

2. Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye rehema, pendo ajabu! Niwapeleke kwa Mkombozi walioshindwa na majaribu!

 

3. Nifananishwe nawe Bwanangu, Mtakatifu, mwenye saburi! Niwe mnyofu kazini mwangu, mtu thabiti bila jeuri!

 

4. Nifananishwe nawe Mwokozi! Nimiminie pendo moyoni! Nibadilishe, e’ Mkombozi, niwe tayari kwenda mbinguni!

Thomas O. Chisholm, 1866-1960
O , to be like thee, blessed Redeemer, R.H. 412




239 NENO mbaya lisitoke kamwe kwa ulimi wako

239

1. Neno baya lisitoke kamwe kwa ulimi wako! Pendo likuchunge pote, hata na maneno yako!

Pambio:
Amri ya Yesu ni “Mpendane”! Kama watoto wema tumtii! Amri ya Yesu ni “Mpendane”! Kama watoto tumtii!

 

2. Pendo ni la mbingu, safi, urafiki ‘takatifu. Tusiyaharibu tena kwa maneno yetu ‘gumu!

 

3. Neno moja la hasira au tendo la uovu, kwa upesi linavunja fungu la upendo safi.

T. Truvé