265. TU wasafiri

265

1. Tu wasafiri, twakaribia nchi ya mbingu kwa Mungu baba. Tusiogope bonde la kufa, Yesu atuongoza kwake!

Pambio:
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote mbinguni!

 

2. Wengi katika wapendwa wetu wamevuka mto wa kufa. Walifuata mwito wa Mungu. Wakahamia nchi nzuri.

 

3. Katika mwendo wa duniani walitazama Mwokozi wao, na waliacha mambo ya huku, walipendeza Bwana Yesu.

 

4. Ndugu wapendwa, tuendelee, hata ikiwa shida njiani! Yesu ni njia, kweli, uzima; tumfuate siku zote! Paul Ongman




266. AYALA naye anayo shauku

 266

1. Ayala naye anayo shauku ya maji ya kisima; na vivyo hivyo ninaona kiu kwa Mungu wa uzima.

Pambio:
Kama ayala aonavyo shauku mito ya maji safi, na vivyo hivyo rohoni mwangu naona kiu kwa Mungu wangu.

 

2. E’ Mungu wangu, Mungu wa fadhili, nakutafuta wewe! Je, nikuone lini kwa ‘kamili, niburudishwe nawe!

 

3. Nazifikiri siku za zamani niliposhangilia. Nijaze tena raha na amani, nakutumainia!

 

4. Na usifadhaike moyo wangu, amini Mungu wako! Fadhili zake hata huko mbingu zatosha sana kwako!

H.E. Lute




267. BABA nakuomba leo na mapema

267

1. Baba, nakuomba leo na mapema: Niongoze pote kwa mapito meme!

Pambio:
Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

2. Nistahimilipo kazi za mchana, unitie nguvu, nakuomba, Bwana!

 

3. Hata jua kuchwa liagapo njia, Baba, nakuomba: Unilinde pia!

 

4. Maadui wengi watuwindawinda, kwa maisha yetu Mungu ni mlinda.

 

5. Katika utoto na ujana tena, ne uzee pia: omba, kesha, shinda!

A. Cummings




268. E’YESU ingia rohoni kabisa

268

1. E’ Yesu, ingia rohoni kabisa, uniweke huru nakunitakasa, nipate kushirikiana na wewe katika mateso na raha daima!

Pambio:
:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:

 

2. Siombi ufalme, siombi heshima, naomba kupewa neema daima, nijue ukweli wa neno la Mungu: Mtoe miili na iwe dhabihu!

 

3. Ingia rohoni, unichungulie, na katika yote unisaidie, nipate kabisa kusudi na nia kujitoa kwako, kukutumikia!

 

4. Hakuna la huku litanizuia nisifananishwe na Yesu Masiya. Nitumainije kufika mbinguni nisiposhiriki Mwokozi mpendwa!

Emil Gustavsson, 1892
O Jesus, min Jesus, 




269. KATIKA bonde na milima

269

1. Katika bonde na milima, kwa mataifa mahali pote, peleka neno la wokovu! Msifu Yesu sana!

Pambio
Msifu Bwana, msifu Bwana! Na tangazeni neno lake, ‘sifuni Yesu daima!

 

2. Mapema na jioni pia hubiri neno la Bwana Yesu! Tangaza njia ya wokovu, msifu Yesu sana!

 

3. Lo! Paradiso malaika wanahimidi Mwokozi wetu. Tuimbe nasi sifa yake, tu’sifu yesu sana!

 

4.Usiyeona kufa bado, uipokee neema leo! Ujisafishe kati’ damu, msifu Yesu Kristo!

H.W. Clark




270. SIMAMA fanya vita pamoja na Mfalme

270

1. Simama, fanya vita pamoja na Mfalme! Bendera tuishike iliyo ya Mwokozi! Mwenyezi huongoza majeshi yake huku. Adui wote pia washindwa mbele yake.

 

2. Sikia baragumu, linatuita sasa! Tuendelee mbele, kusudi ni kushinda! Tusiogope kamwe hatari ya shindano, pigana na adui kwa nguvu yake Mungu!

 

3. Sima, fanya vita kwa jina lake Yesu! Hatuna nguvu sisi, tunamtegemea. Na kwanza tuzivae silaha zake Mungu! Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidii!

 

4. Shindano letu hapa ‘takwisha siku moja; twapiga vita leo, baada pumziko. Na kila mshindaji atapokea taji, na utukufu tele karibu na Mfalme.

Georg Duffield, 1858




271 UWATAFUTE wenzako wapoteao mbali

271

1. Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Yesu mwenyewe apenda kuwaokoa wote.

Pambio
Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Pasha habari ya Yesu na ya wokovu wake!

 

2.Uwatafute wenzako kwa neno la upendo! Mungu atalibariki na kulithibitisha.

 

3.Uwatafute wenzako kwa’jili ya Mwokozi! Aliwakomboa wote, ni mali yake kweli.

 

4.Uwatafute wenzako kabla ajapo Yesu! Wasipotee kabisa, uwaokoe mbio!

Fred P. Morris




272. NANI ni wa Yesu

271

1. Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Atafute watu na kuwahubiri! Nani anataka kujitoa leo, kufuata Yesu katika mateso?

Pambio
Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Nani atakaye na amwitikie! Mimi ni wa Yesu, nimtumikie, nitafute watu, kwake warudie!

 

2. Kwa upendo wake tunalazimishwa kutafuta wenye dhambi na makosa. Tunaendelea kuwavuta kwake, hata wanaomba: Mungu tuokoe!

 

3. Yesu alitununua sisi sote ju’ ya msalaba na kwa damu yake. Kwake tumepata raha na uhuru; tunataka sasa kuwa waaminifu!

 

4. Hata vita ikiongezeka huku tunayo bendera ya kushinda kwetu. Siku ya hatima inakaribia, itaibadili vita iwe shangwe.

Frances R. Hauergal




273. NI uheri kumwamini Mungu

273

1. Ni uheri kumwamini Mungu kama Ibrahimu wa zamani. Hakutiwa shaka kwa uchungu, ila alitii kwa imani. Ni uheri kuendea sawa katika mapito ya sheria. Ukijaribiwa na kukawa, mwisho Mungu atakujalia.

 

2. Mashujaa wote wa Biblia hawakufurahia anasa. Wakafunzwa kutumainia Mungu na uweza wake hasa. Tena wakaenda kwa imani ya kutetemesha ulimwengu, wakashinda giza na shetani. Sifa na heshima zina Mungu!

 

3. Yesu atakaye kuzwa naye kwanza adhiliwe kuwa vumbi; Mwana wake mwema na ambaye baba humpenda, humrudi. Hivyo Mungu awakamilisha watu wake kwa mateso huku, na zaidi kuwafahamisha kulijua pendo lake kuu.

 

4.Na ikiwa raha ya dunia yatoweka katika jaribu, mwaminifu atafurahia Mungu wake, kwani yu karibu. Na mavuno ya taabu yake yakichomwa na kuharibika, atategemea Bwana wake na kwa hiyo hata nung’unika.

 

5.Jipe moyo, enyi kundi dogo, na msiogope hatarini! Shika neno la Mwenyezi Mungu, litawaongoza safarini! Haleluya, kwani majaribu yahimiza msafiri mwendo, hata ataona kwa karibu mji wa amani na upendo!

Emil Gustavsson, 1889




274. NINAFURAHIYA kisima daima

274

1. Ninafurahia kisima daima, kisima cha damu ya Yesu. Katika upendo nalindwa salama, nasifu Mwokozi mpendwa.

Pambio
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.

 

2. Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi kwa maji ya ‘hai. Yananilietea kupita kipimo uzima na shangwe rohoni.

 

3. Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi katika uheri. Ufike upesi ulie na kiu, kisima kinabubujika!

 

4. Nakaa karibu ya kisima hiki, naona furaha na raha. Nakando ya maji nafasi kwa wote, waweza kupona kabisa.

Emil Gustavsson, 1892




275 E’MUNGU mwenye haki

275

1. E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku katika mambo yote yanayokupendeza! Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka yananitia tetemeko mpaka kufa.

 

2. Ni heri siku zote kutegemea Yesu na kuenenda sawa katika nyayo zake, kwa kuwa yeye ni Mchunga anayeniongoza vema, nipate kuingia katika raha yake.

 

3. Safari yangu sasa yaelekea mbingu, Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha kuona yeye aliyeninunua kwake.

 

4. Ulimwenguni humu, matata na kuchoka. Nikihitaji kitu nafadhahika bure, lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi, natumaini sitakosa dhawabu yangu!

 

5. Mbinguni sitaona adui zangu tena. Hayatakuwa mambo yakupokonya pale. Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya! Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu!


Video imeimbiwa na METHUSELA Bushambale na DAVID IMANI

THAMBI




276. MATENDO ya Mungu yapita fahamu

276

1.  Matendo ya Mungu yapita ‘fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.

 

2.Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?

 

3. E’ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama mbinguni!

 

4.Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ‘takwisha, milele nitashangilia.

 

5. Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye neema katika shauri na tendo.

 

6.Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao mbinguni.

 

Emil Gustavsson, 1886




277. NITAOGOPA nini gizani duniani

277

1. Nitaogopa nini gizani duniani? Sikuachiwa peke’ mbali ya tumaini! Mwokozi yu karibu, asiyebadilika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Pambio:
Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.

 

2. “E’ usifadhaike moyoni mwako, mwana”, anong’oneza Yesu, “Nitegemee sana!” Na hapo woga wangu waruka kwa hakika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

 

3.Na nikijaribiwa na jua lifichwapo, hata sioni raha, wala faraja hapo, nakimbilia Yesu, na yote yapinduka.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Mrs. C.D. Martin




278. NINAINUA macho yangu ka Mungu

278

1. Ninainua macho yangu kwa Mungu aketiye juu, aliye msaada wangu, njiani pangu nuru kuu. Aliyefanya yote, maombi huyasikia. Katika njia zangu zote atanilinda pote pia.

 

2. Bwanangu asiache tena mguu wangu usogezwe, kwa kuwa ni mlinzi mwema, naye hatasinzia kamwe. Alinda roho yangu nisije nikapotea. Hitaji za maisha yangu baraka yake ya’enea.

 

3. Aniokoa na uovu, na roho yangu imepona. Kwa yeye nguvu na wokovu, nilizionja naku’ona. Ananilinda pote: kutoka na kuingia; anijaliza mema yote hata nakutumainia.

J. Arrhenius, 1694




279. UPENDO wake Mungu unatuunganisha

279

1. Upendo wake Mungu unatuunganisha. ‘Shirika wa watakatifu – uheri wa mbinguni.

 

2. Katika sala zetu twakaribia Baba kwa tumaini, ujasiri na kwa imani moja.

 

3.Upendo wa kikristo ha’vunji urafiki. Twalia naye kwa uchungu, furaha twa’shiriki.

 

4. Tunaachana huku kwa sikitiko sana. Kwa shangwe tena kwake Mungu twaweza kuonana.

Fohn Faweet
Blessed be the tie that binds, R.S. 946; R.H. 713




280. JINA lake Yesu linadumu

280

1. Jina lake Yesu Kristo linadumu siku zote; jina hili la milele haliwezi kunyauka; linafaa watu wote, na wazee na vijana; linaweza kuongoza kila mtu kwake Mungu.

Pambio:
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.

 

2. Jina hili linavuma pande zote za dunia, na kwa wote linaleta tumaini na faraja. Jina hili laondoa uadui na ubaya, hata milki ya Mwokozi itaanza kutawala.

 

3. Na katika giza huku jina hili linang’aa, laonyesha msafiri njia wazi ya uzima. Jua likitiwa giza, jina hili linadumu; na milele lisifiwe hapa na mbinguni juu.




281. YOTE ninayo niliyapokea kwa wema wake

 281

1. Yote ninayo niliyapokea kwa wema wake unaonea. Namsifu Yesu, namtegemea, aliniokoa kwa neema.

Pambio:
Niliyekuwa nimetoroka, kwa pendo lake nimeokoka. Yesu yu mwema na mwenye rehema, nimeokolewa kwa neema!

 

2. Nilitembea zamani dhambini katika njia ya kufa, lakini Yesu alinitafuta porini, akaniokoa kwa neema.

 

3. Natakasiwa na Yesu Mwokozi, si kwa majuto na si kwa machozi, bali kwa damu, ninao ‘kombozi; nimeokolewa kwa neema.

 

4. Raha ya mbingu imeniingia, kwa shangwe kubwa ninafurahia Yesu, kwa kuwa anirehemia; nimeokolewa kwa neema.

J.M. Gray, 1905 Otto Witt, 1922
Naught have I gotten, RS. 605




282 UKIONA kiu sana ujalivu

 282

1. Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi, roho yake safi pia, liamini neno la babako na atakujazi, nawe utashangilia.

Pambio:
Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: “Njoo bila ‘sitasita!” Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

 

2. Vichukue vyombo vyako, uvioshe safi sana kisimani pa Golgotha! Afadhali kujitoa lote kwa Mungu Bwana, na imani itaota.

 

3.Na mafuta ya neema hayakomi. Asifiwe! Tunakuwa na shukrani! Anataka kumimina Roho ya ahadi yake. Mpokee kwa imani!

Leila Morris, 1922
Are you looking for the fulness, R.H. 214




283. NIMEYASIKIA mengi aliyoyafanya Yesu

283
1. Nimeyasikia mengi aliyoyafanya Yesu katika maisha yake huku chini: Pote alitenda mema, alisaidia wote. Kwa furaha ninaimba: “Yesu yeye yule leo!”

Pambio
Yesu Kristo yeye yule jana, leo, siku zote. Hutafuta wapotevu, huokoa na waovu. Mwokozi wetu yeye yule!

 

2. Na kipofu yule, jina lake ndilo Bartimayo, aliposikia Yesu yu karibu, kwa imani akaomba, akapona kwa neema. Nafurahi kwa kuimba: “Yesu yeye yule leo!”

 

3. Watu wote wenye dhambi na wagonjwa na maskini wanaitwa kwake Yesu kwa rehema. Uiguse nguo yake, sawa mwanamke yule, utapewa nguvu yake, kwani Yesu yeye yule!

 

4. Nimeyasikia tena jinsi alivyoombea maadui wake ju’ ya msalaba. Aliteswa kwa miiba, aliona maumivu. Ninaimba kwa furaha: “Yesu yeye yule leo!”

S.C. Kaufman, 1895
Have you ever heard the story, R.H. 442




284. USIMTAFUTE Yesu kati’wafu kaburini

284

1. Usimtafute Yesu kati’ wafu kaburini! Yu mzima, tumsifu, hakushindwa na kuzimu!
:/: Yesu hai, Yesu hai, mshindaji wa mauti! :/:

 

2. Maadui walifunga Bwana Yesu kaburini, Mungu alimfufua Mwana wake. Furahini!
:/: Yesu hai, Yesu hai, imba hivyo duniani! :/:

 

3. Yesu hai, ni habari ya kupasha pande zote. Yu Mwokozi wetu kweli, alitufilia sote.
:/: Yesu hai, Yesu hai, Mkombozi asifiwe!:/:

P.P. Bliss




285. NENO la Mungu ndani ya Biblia

285

1. Neno la Mungu ndani ya Biblia limetolewa na Mwenyezi Mungu. Biblia yetu inatuambia: Njoo kwa Yesu, Mkombozi wetu!

Pambio:
Neno la Mungu tulilolipewa, njia ya mbingu limetuonyesha; nuru gizani ya kutuongoza katika mwendo wetu kwenda mbinguni.

 

2. Siku za giza zinakaribia, kama walivyosema manabii. Biblia yetu itatuangaza na kutuonya njia hata mwisho.

 

3. Katika neno la Biblia yetu tunaupata utajiri wote. Mbingu na nchi zitaangamia, neno la Mungu litashinda yote.

Thoro Harris, 1874-1955




286. YESU ulikaribishwa arusini

286

1. Yesu, ulikaribishwa arusini huko Kana; hapo ikadhihirishwa nguvu yako kwa ishara.

 

2. Leo tunakuhitaji, wabariki ndugu hawa: Bwana na bibi-arusi! Ndoa yao iwe sawa!

 

3. Katika taabu, raha, wafungane kwa upendo! Watumike kwa furaha, w’andamane kati’ mwendo!

 

4. Yesu, U mlinzi wao, uwalinde na mabaya! Uhifadhi nyumba yao! Tunaomba mema haya!

C.G. Lundin




287. TUNAMTIA mikononi mwako

287

1. Tunamtia mikononi mwako mtoto huyu, umtunze sana, na kila siku kwa neema yako umbariki, Bwana Yesu Kristo!

 

2. Ulimwengu kuna majaribu mahali pote, shida na mitego. Lakini uwe mchungaji wake, na umwongoze, E’ rafiki mwema!

 

3. Mwokozi kwa upendo ‘mchukue, asije akashindwa safarini! Na umlinde kwa rehema yako, apate kuwa wako siku zote!

 

4. Utume nuru ya neema kwake na maji ya uzima toka kwako e Bwana Yesu. Twakuomba leo ulinde mwana wetu kwa salama.

T.B. Barrat




288. MUNGU wetu

288

1. Mungu wetu, utulinde na utubariki sote! Bwana, uturehemie, tutolee nuru pote! Utuangazie uso, tupe na amani yako! Mungu Baba, Roho, Mwana, tunakushukuru sana!

J. Svedberg, 1694




289. NINATAMANI kwenda mbingu

289

1. Ninatamani kwenda mbingu nchi yangu niliyopewa na Mungu kwa imani. Ni shangwe bora kuona mji ule; kwa kwenda kule sitaogopa kitu.

Pambio:
E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ‘takatifu!

 

2. E’ Mungu, tumepata Mwana Yesu Kristo, kipawa kweli kinachoshinda yote. Anahubiri amani kwao wote walio huku karibu, nao mbali.

 

3. Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si wapitaji na tena si wageni, tunatumika kwa roho ya upendo.

 

4. Amani kwetu na matumaini tele, salamu toka kwa Mungu wa milele ni posho ya watumishi wa upendo; tunaurithi uzima wa milele.

THAMBI Aae