290. BARAGUMU litalia sana

290

1. Baragumu litalia sana, watu wote watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:

 

2. Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:

 

3. Najua Mchunga wangu mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa.
:/:Nani Mchunga mwema? Yesu, mweza yote. :/:

 

4. Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja.
:/: Nani atahukumu? Yesu, mweza yote. :/:

 

5. Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi.
:/: Nani ni mzabibu? Yesu, mweza yote. :/:

 

6. Unayempenda Baba Mungu, lazima upende ndugu yako; ukiwa hupendi ndugu yako, huwezi kupenda Baba Mungu.
:/:Nani aliyesema? Yesu, mweza yote. :/:

 

7. Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli.
:/: Nani mwenye upendo? Yesu, mweza yote. :/:

 

8. Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu.
:/: Tumshukuru nani? Yesu mweza yote. :/:

THAMBI Aae




291. MIMI mwenye hatiya nilikombolewa

 291

1. Mimi mwenye hatia nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa. Dhambi zangu na zako alizichukua, kwa damu aliniokoa.

Pambio:
Dhambi zimetundikwa msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.

 

2. Yesu mwenye upole na mwenye upendo ananitakasa rohoni. Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, alikufa msalabani.

 

3.Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, kwa kuwa alinifilia. Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda, daima nakushangilia.

Carrie E. Breck, 1855-1934
There was One who was willing to die in my stead, R.S. 737




292. KATIKA damu takatifu

292

1. Katika damu takatifu ya Mwokozi wangu nimesafishwa. Na nguvu ya Mwokozi wangu tu yaweza kunilinda safi.

Pambio:
Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya wokovu na nguvu ya kushinda! Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya wokovu wote!

 

2. Kwa wingi wa neema yake tu nimeokoka, nimeokoka. Wokovu ni kwa ‘jili yako na kwa kila ‘aminiye kweli.

 

3. Kwa nguvu zangu sitashinda na siwezi neno, siwezi neno. Ila Yesu anayenifahamu atanisaidia pote.

 

4. Babangu mwema ananipenda na ananilinda, ananilinda. Sitaogopa giza huku kwa maana yu pamoja nami.

Otto Witt/ C.H. Morris




293. NCHI nzuri ya raha ajabu

 293

1. Nchi nzuri ya raha ajabu, kwa imani twaona si mbali. Baba atungojea sababu ametuandalia mahali.

Pambio:
:/: Tukutane sisi sote huko juu nyumbani mwa Baba!:/:

 

2. Huko juu kwa raha, amani tutaimba na kushangilia, kutolea Mwokozi shukrani kwa sababu alitufilia.

 

3. Baba wetu mpendwa na mwema kwake kuna furaha ya tele. Twamsifu kwa kuwa neema yatutosha kabisa milele.

S.F. Bennet, 1867
There ‘s a land that is fairer than day, R.S. 305; R.H. 788




294. UTUME Roho yako juu yetu

294

1. Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya hapo kale!
:/: Uwashe moto wako ndani yetu, tusiwe watu wa uvuguvugu! :/:

 

2.Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya siku ile.
:/: Mtume Petro alipohubiri katika nyumba yake Kornelio! :/:

 

3.Utume Roho yako juu yetu, utupe nasi Pentekoste yetu!
:/: Maelfu wenye dhambi waokoke, na neno lako lienee pote!:/:

 

4.Utume Roho yako juu yetu! Mikono yako uinyoshe sasa,
:/: ishara za ajabu zifanyike, wagonjwa uwaponye kati yetu! :/:

 

5.Uwaamshe waliosinzia, waliochoka huku safarini!
:/: E’ Bwana utujie kama kale ulivyowabariki watu wako! :/:

K.G. Sjölin, 1906




295. E’FURAHENI watu wake Mungu

295

1. E’, furahini watu wake Mungu! Mwokozi wetu alituokoa. Neema kubwa, pendo la ajabu! Tusifu Mungu sana siku zote!

Pambio:
E’ Mungu ana mamlaka yote, ni ngao na makimbilio yangu; Ni Baba yangu, na anasikia maombi yangu. Asifiwe!

 

2. E’, furahini watu wake Mungu! Tuimbe nyimbo za furaha nyingi! Tusiogope ila tumwamini na twende mbele kwa uweza wake!

 

3. E’, furahini watu wake Mungu! Tukimahangilia (sic) Mungu wetu, jirani zetu wasioamini watatamani kumjua Yesu.

 

4. E’, furahini watu wake Mungu! Mfalme wetu yu pamoja nasi. Kitambo bado- na tutahamia mbinguni kwake Mkombozi wetu.




296. Dhambi hatia zimeondolewa

296

1. Dhambi, hatia zimeondolewa, yote ya kale yamepita sasa. Damu ya Yesu imenisafisha; ninamfurahia Mkombozi wangu.

Pambio
Mavazi safi na kao nzuri ninayo huko ju’ mbinguni. Thawabu nita’pewa huko ni taji ya uzima. Na Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa, alilipa deni langu. Pendo lake kubwa nina’sifu siku zote, ninamfurahia Mkombozi.

 

2. Siku za manung’uniko zimekwisha, nimeokoka katika utumwa. Sasa naona raha na furaha sababu Bwana Yesu alinikomboa.

 

3. Shaka na hofu zimeondolewa, na siogopi kufa kwangu tena. Katika Yesu ninatumaini. Na ninalindwa vema naye siku zote.

 

4. Roho wa Mungu amenijaliza, anifariji katika mwenendo. Yesu Mwokozi yu karibu nami, aliye ngao yangu na makimbilio.




297. NIPE saa moja nawe Yesu

297

1. Nipe saa moja nawe Yesu nikichoka huku duniani! Hata nikiona vita kali, wanistarehesha siku zote.

Pambio:
Nipe saa moja nawe Yesu, kwani giza iko duniani! Natamani kukukaribia, kusikia neno lako zuri.

 

2. Nipe saa moja nawe Yesu katika jaribu na taabu! U makimbilio yangu mema katika hatari na ghasia.

 

3. Nipe saa moja nawe Yesu uliechukua dhambi zangu. Ninataka kueleza yote, kwani unanifaamu sana.

……………………………………………………………

Video ya sauti

 




298. NINAO wimbo wakunifurahiya

298

1. Ninao wimbo wakunifurahisha wa Mwokozi, wa Mwokozi. Namshukuru kwa roho yote pia, Mwokozi mzuri ninaye!

Pambio:
Mwokozi – wimbo wangu, Mwokozi, Mwokozi! Mahali pote na siku zote nitamsifu Yesu kati’ yote. Mwokozi ni wimbo wangu wa huku na Mbinguni.

 

2. Na jina moja ni lenye pendo tele: Yesu, Yesu, ndilo jina! Anipa yote niliyokosa mbele, Mwokozi mzuri ninaye.




299 JE, umelisikia jina zuri

299

1. Je, umelisikia jina zuri, Jina la Mwokozi wetu? Linaimbiwa duniani pote na katika watu wote.

Pambio:
Yesu, jina hilo linapita majina yote kwa uzuri! Ni lenye nguvu ya kutuokoa na hatia na makosa.

 

2. Linafariji moyo wa huzuni, latutia raha kuu. Katika shida na hatari huku jina hili latulinda.

 

3. Katika giza huku jina hili linang’aa kama nyota, lanipa utulivu na ‘hodari siku zote hata kufa.

 

4. Majina yote yasahauliwa, ila jina lake Yesu milele litang’aa huko juu. Yesu, jina nzuri mno!

Allan Törnberg, 1935




300. MUNGU abariki nyote

300

1. Mungu awabarikie nyote na awe pamoja nanyi! Awalinde kwa amani! Mungu n’awe nanyi siku zote!

Pambio:
Mungu n’awe nanyi daima hata mwisho wenu wa safari! Mungu n’awe nanyi daima hata tuonane huko juu!

 

2. Mungu wetu awalinde pote na kuwahifadhi vema kwa mikono ya rehema! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

3. Mungu awaangazie nuru, na awashibishe sana kwa fadhili zake Bwana! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

4. Mungu awainulie uso! Na wakati wa kuhama mpelekwe kwa salama! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

5. Mungu awabarikie nyote, awalinde m-we huru, awaangazie nuru! Awainulie uso wake!

J.E. Rankin / Daniel Hallberg
God be with you till we meet again, R.S. 942; R.H. 722