14 MWOKOZI wangu ulikwenda juu kukaa kuumeni kwake Baba

1. MWOKOZI wangu ulikwenda juu kuumeni kwake Baba;

Utakusanya sisi sote huko, Mbinguni kwako utatufikisha.

:/: Makao mema wa’tulinda, Unatungoja kwake Mungu Baba. :/:

 

2. Mwokozi wetu wewe, Yesu Kristo, kwa’ajili yetu mbele yake Baba.

Wachungu sana sisi, kundi lako, Na watusaidia ‘jaribuni.

:/: Na sikuzote unatuombea, watushindia vita kaili huku. :/:

 

3. Mikono yako uliwanyoshea walio wako, siku uli’kwenda;

Na hivyo siku utakaporudi utabariki wakuaminio.

:/: Ulivyokwenda, utakavyorudi; Niombe, nikakeshe kwa imani!:/:




15 MUNGU moto wako uniutumie

1. MUNGU, moto wako uniutumie, Ninangoja nguvu yako! Nipe na uzima na upendo wako, Unijaze, E’Mwokozi wangu!.

 

2. Teketeza usiyopenda, Nisafishe kati’ damu! Na karibu yangu uivunje tena, unionyeshe, Yesu, niwe safi.

 

3. Unilinde, Yesu sikuasi tena unifunge kwa pendo! Mimi ni dhaifu, unitunze kwako ‘uniongoze kwa mkono wako.

 

4. Huko juu kwako tutaona raha, na huzuni itakwisha. Nyimbo za shukrani zitajaza mbingu; utukuzwe, Yesu, Mkombozi

 




16 YO YOTE uonayo huku katika mwendo wako

16

1. YO yote uonayo huku katika mwendo wako, Yafaa kumwambiya Yesu atakusaidia.

Refrain:
:/: Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi ne’ma yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu. :/:

2. Ukichukiwa na wenzake na ukijaribiwa, Mwokozi yu karibu sana, Maombi asikia.

3. Ukiwa mwana mpotevu, na mbali na Babako, Amani una’kosa sasa, Urudi kwake Yesu!

4. Ukiwa na makosa mengi, Na roho yako ngumu, Neema yake yakutosha, utubu dhambi zako

5. Ikiwa nguvu mara nyingi kuomba kwa bidii, uombe Baba, kama mwana, akusikia kweli!

Carl Lundgren





17 UKAE nami giza inafika!

17

1. UKAE name, giza imefika! Usiniache, Mungu, nakuomba! Unayejuwa udhaifu wangu’ Nategemea wewe, ‘kae nami

 

2. Maisha yangu ni mafupi sana, Uzuri wa dunia utakwisha. Kuna machozi, kufa huku chini, wewe Mwokozi wangu, ‘kae name!

 

4. Nakuhitaji wewe siku zote, Unayeweza sana kunilinda. Wewe shujaa wa kushinda wote, katika hali zote ‘kae.

 

5. Unionyeshe msalaba wako, Nione nuru yako kati’ giza! Na nikiishi au nitakufa, wewe, Mwokozi wangu, ‘kae name!




18 MUNGU wetu yu karibu kututia nguvu yake

18

1. MUNGU wetu Yu karibu kututia nguvu yake. Mbingu in maghubari, Tuletee mvua saa!

Refrain:
Tusikie, Mungu wetu, Tubariki saa hii! Tunangoja, tunangoja, tunyeshee nguvu yako!

 

2. Mungu wetu Yu karibu, hapa ni Patakatifu, Sisi sote tunangoja kujaliwa naye Mungu.

 

3. Mungu wetu Yu karibu, Kwa imani tunaomba: Tuwashie moto safi ndani ya mioyo yetu.

 

4. Mungu ufungue mbingu, Twalia nguvu zako! Tubariki saa hii kwa rehema zako kuu!




19 MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘Takatifu

19

1. MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘takatifu, Tunaomba kwa imani “Umtume hapa kwetu!

 Refrain : Mungu wetu, Mungu wetu, Umimine Roho yako, mioyoni mwetu, Bwana utimize kazi yako!

 

2. Washa moto wako tena, ndani ya mioyo yetu, Hata vyote vya majani vitateketea sana!

 

3. Utakase roho zetu, Na kiburi uivunje! Wewe U mfalme wetu, utawale watu wako!

 

4. Utujaze siku zote Pendo lako kubwa, Mungu! Sisi tuwe nyumba yake, Roho yako takatifu!

 

5. Na karama zake Roho utuzigawie Bwana! Na wangonjwa uwaponye, Wote wakuone Mungu!

 

 




20 BWANA Yesu uniongoze baharini huku chini

20

1. BWANA Yesu, uniongoze Baharini huku chini, Juu ya mawimbi mengi, Katika dhoruba kali! Bwana Yesu, uniongoze, Nakutegemea wewe.

2. Bwana Yesu, uniongoze, Utulize moyo wangu! Neno moja kwako, Marashwari baharini. Bwana Yesu uniongoze, Nipe utulivu wako!

3. Bwana Yesu uniongoze, Niyashinde majaribu! Mengi ya kunidanganya, Mengi ya kufunga macho! Bwana Yesu uniongoze, Niwe mshinadji kweli.

4. Bwana Yesu uniongoze, Siku nita’vuka ng’ambo! Nikiona woga , giza, Nipe nuru na amani! Bwana Yesu, uniongoze, Uwe nami hata mwisho!

 




21 JUU ya mbingu zote

21

1. JUU ya mbingu zote, Nyota na jua pia, Hapo yafika kweli Maombi ya mwene dua. Roho ya mwana-damu yamfikia Mungu, Huko yabisha lango na kumtafuta Baba.

2. Roho haitaona raha amani huku; Kuna bandari njema Mbinguni kwa Mungu Baba. Moyo utatulia, Nuru itatokea Tukifuata njia ya sala na maabudu.

3. Hata mototo ‘dogo mwenye kuomba Mungu, Hana la kuogopa; Kuomba kwa faa sana. Tusisahau tena, pote twendapo huku kwamba maombi yetu yafika kwa Baba.

 

Augusta Lönnborg, 1895

 




22 YESU KRISTO bwana wangu

22

1. YESU Kristo Bwana wangu, Una amri na uwezo za kuziondoa dhambi, Na ‘takasa roho yangu.

Refrain:
Nitolee masamaha, ‘niokoe na jaribu, unilinde hata mwisho, Unitwae kwako juu!

2. Mbele nilikuwa mwovu, nilikukataa, Yesu, Kwa hakika sikujuwa wewe na upendo wako!

3. Bwana Yesu, usamehe dhambi nilizozifanya! ‘siitike majaribu, nguvu yako inilinde!

4. Tangu sasa Wewe, Yesu, U Mwokozi na Rafiki, Nimetengwa na Shetani, Niwe wako siki zote!

 




23 NIKITAZAMA kwa imani Mwokozi wangu

23

1. NIKITAZAMA kwa imani, Mwokozi wangu, Yesu, Nawaka kwa upendo wake, Na ninavutwa kwake; Naona majeraha yake, Mikono na ubavu wake, Na humo najificha sana, Moyoni mwa upendo

 

2. Imanuel upendwaye, Nilinde sikuzote, Mpaka nihamie kwako Mbinguni mwa uheri! Milele na milele huko hapana la kunizuia Nimsifu Bwana Yesu kwa damu na ‘jereha.




24 E’MUNGU mwenye kweli

1. E’Mungu mwenye kweli, nakuamini sana, maneno yako yote, milele yata dumu ‘’niite kati’ shida nitakusaidia nategemea Bwana, ahadi yako hiyo.

 

2. Na katika uchungu ni heri kuamini kuamini, naweka roho yangu kulindwa nawe, baba, uliye nifundisha kuita jina lako; naona tumaini na tegemeo kwako!

 

3. Ninavyoomba kweli, najuwa wasikia. Yalioyo mema kwangu, najuwa wayafanya. Katuka shida kali waweza kunilinda; wanichukuwa mimi na masumbuko yangu.





25 MVUA yambingu unyeshe

25

1. Mvua ya mbingu unyeshe, kama ulivyo ahidi! Juu ya dunia yote inye kutubarikia!

Pambio
Mvua ya mbingu, mvua ya mbingu utume! Utunyeshee neema, tunakuomba, e’ Mungu!

2. Mvua ya mbingu unyeshe, ituamshe na sisi! Ju’ya vilima na bonde mvua ya mbingu ifike!

3. Mvua ya mbingu unyeshe katika dunia yote! Watu wa Mungu wapone, mbegu za roho ziote!

4. Mvua ya mbingu unyeshe, tunapokuelekea! Utujalie baraka tunakuomba, e’ Mungu!




26 NAKUHITAJI Yesu

26

1. Nakuhitaji, Yesu, Mwokozi wangu mwema, sauti yako nzuri iniletee raha!

Pambio:
Nakuhitaji, Yesu, usiku na mchana! Katika sala yangu unibariki sasa!

 

2. Nakuhitaji, Yesu, unionyeshe njia! Na unitimizie ahadi za neema!

 

3. Nakuhitaji, Yesu, uwe karibu nami, nipate kulishinda jaribu la shetani!

 

4. Nakuhitaji, Yesu, katika mambo yote, kwa kuwa bila wewe maisha hayafai.

 

5. Nakuhitaji, Yesu, njiani huku chini, nipate kuwa kwako milele na milele!

 

Annie S. Hawks, 1835-1918
I nee Thee every hour, R.H. 568




27 UNA uhodari leo wakumufwata Yesu hata ukichekwa sana

27

1. Una uhodari leo wa kumfuata Yesu, hata ukichekwa sana na kuteswa duniani?

 

2. Una uhodari leo kuwa mtu wake Mungu? Ukiona haya sana, kisha utaona nini?

 

3. Mji unaonekana ukijengwa mlimani, hivyo na imani yetu inadhihirika sana.

 

4.Ukipenda Yesu na kuliko vitu vyote, unataka kumkiri, mbele ya wenzako huku.

 

5. Chuki au ‘pendeleo kwako kitu bure tena, watafuta siku zote sifa zake yesu Kristo.

 

6.Ujihoji nafsi yako ukitaka kuokoka! Uliekataa Mungu, tubu dhambi zako leo!

 

7. Umsihi masamaha, akuokoe ‘kati damu! Omba uhodari tena wa kumfuata Yesu!

 

8. Uchague Yesu leo, uwe mfuasi wake! Ukitwaa msalaba utaipokea taji!

 

Lina Sandell-Berg, 1859




28 NINATAKA kufuata wewe

 28

1. Ninataka kufuata wewe, Yesu, siku zote, ‘kiwa katika furaha au shida na udhia. Unaponitangulia ninakuja nyuma mbio. Ninajua ni karibu Kuwasili huko kwako.

 

2. Haifai niulize: Bwana, unakwenda wapi? Au kwa kusitasita kuishika njia yako. Kweli hapa kazi moja: Kufuata wewe mbio, kwenda njia ile moja wewe unionyeshayo.

 

3. Walakini kama kitu kinataka kunifunga, au kuwa mgogoro katita safari yangu, ‘kate kamba mara moja ifungayo roho yangu! Ninataka kuwa huru kukutumikia vema

 

4. Bwana Yesu, unilinde, uhifadhi nia yangu! Nikichoka kwa safari, nong’oneza kwa upendo: «Mwana, u mtoto wangu, uniandamie punde, utapumzika sana tena kwangu huko juu».

 

Lina Sandell-Berg, 1896
o Jesus, Sgt. 605 (231)




29 UNIVUTE Yesu

29
1. Univute, Yesu, nifuate nyayo zako, ‘kiwa kwa rafiki au katika wageni, na mahali pa furaha au sikitiko; sina budi kumkaribia Yesu.

Pambio:
Nimfuate, nimkaribie, siku zote na popote nimwandame Yesu! Nimfuate, nimkaribie, Yesu mbele, nami nyuma, hata mwisho!

2. Juu ya milima nitasikiliza Yesu, hata mabondeni nitaandamana naye. Jua, giza, afya, ‘gonjwa, utulivu, vita, kati’ hayo yote Yesu yu karibu.

3. Nikiteka maji, au nikilima shamba, nikika’ nyumbani au ‘kiwa safarini, hata huko soko neno moja ni halisi: Sina budi kumkaribia Yesu

Down in the valley, R.H. 245




30 TARUMBETA lake Kristo linalia pande zote

30

1. Tarumbeta lake Kristo linalia pande zote, na wakristo wote wanajipanga vita ju’ ya mahodari wa shetani. Kweli tutashinda, kwani Yesu yupo mbele.

Pambio:
Twende, Yesu a’tuita, twende na wakristo wote! Twende, na tusiogope, Yesu yupo mbele yetu!

 

2. Neno la akida wetu lipo: «Mniaminie»! Naye anatangulia, tunakuja wote mbio. Kwa silaha zake Mungu kila mtu atashinda, kwani Yesu yupo mbele.

 

3.Na tukiwa mbali ya akida wetu tutashindwa, tutafungwa na adui na pengine kupotea. Walakini kule mbele watu wote watashinda, kwani Yesu yupo mbele.

 

4. Tarumbeta litalia tena, vita itakwisha, na askari watapata raha na matunzo. Watapumzika na milele watashangilia, kwani Yesu yupo mbele




31 KATIKA safari yetu kwenda huko juu tusilale usingizi

31

1. Katika safari yetu kwenda huko juu tusilale usingizi, tuwe na bidii!

Pambio:
Kaza mwendo tusifungwe, twende mbio tu! Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme ‘kuu!

 

2. Bwana Yesu anatupa maji ya uzima, maji hai ya milele ya kuburudisha.

 

3. Njia na miiba mingi inatuzuia, hofu na hatari nyingi zina fadhaisha.

 

4. Mungu wetu atungoja huko kwake juu, Yesu ni Mwokozi wetu, tufuate Yeye!

P.P. Bliss




32 HAPO nilikua chini katika dhambi nyingi

32

1. Hapo nilikuwa chini Katika dhambi nyingi, roho yangu iliona kufa na giza tele. Mungu alikisikia kilio changu huko, naye akanipandisha, kuniponya.

Pambio:
:/: Nimeokoka, nimeokoka! Yesu Mwokozi wangu aliniokoa:/:

2. Sasa Yesu amekuwa makimbilio yangu, na upendo wake ‘kubwa uko moyoni mwangu. Ne’ma yake kubwa sana inajaliza roho, niwe mwaminifu kwake siku zote!

3. Ewe, mwenye sikitiko, kuna matumaini: Yesu anakufahamu, atakusaidia. Atakupandisha toka tope la kuteleza, upokee ne’ma yake kwa wokovu!

James Rowe, 1912




33 HURU kama ndege bustanini

33

1. Huru kama ndege bustanini, sasa nafurahi kwa sababu Yesu ni rafiki yangu ‘kubwa; nina amani siku zote.


2. Aliniokoa na mashaka, alinipa tunu ya rehema. Mimi ni mtoto wa babangu, na nuru inang’aa sana.


3. Ninataka ku’shukuru Bwana, alitupa dhambi zangu mbali, na sitaziona tena kamwe, hazitanitawala tena.


4. Jua likifichwa kwa mawingu, kiti cha rehema ni karibu, hayo ndipo shida ziishapo, na roho yangu yatulia.


5. Radhi kama mwana kwa babake, kwa salama kama bandarini, Ninapumzika kwa Mwokozi, mbali na shida na huzuni.


6. Yesu yu karibu siku zote, achukua mimi na mzigo. Napokea kwa mkono wake neema na mateso pia.


7. Nilimpa Yesu moyo wangu, ninapenda kumtumikia; neno lake linapendwa nami, na nira yake ni laini.


8.Nafurahi sana kanisani kati ya watoto wa babangu, Roho ya neema ni karibu, kunanifurahisha sana.


9. Mimi ni mdogo duniani, tena msafiri na mgeni. Kwetu ni mbinguni huko juu; babangu ananiongoza.


10. Saa za mashaka zitakwisha, kuja kwake Yesu ni karibu. Nitaona raha kubwa sana katika nyumba ya babangu.

Nils Frykman




34 KWA pendo lake kubwa alitafuta mimi

34

1. Kwa pendo lake kubwa alitafuta mimi, na alinichukua begani mazizini na nyimbo zao malaika zikajaza mbingu pia.

Pambio:
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.

2. Mchunga mwema Yesu aliniponya roho, na akaniambia: «Mtoto upendwaye». Sauti yake ya upendo ikaufariji moyo.
3. Ninakumbuka jinsi alivyotoka damu, na taji ya miiba, mateso ya mauti. Na penye msalaba wake ninashukuru Bwana Yesu.
4. Namfuata yeye katika nuru yake, waridi za ahadi zapamba njia yangu. Milele nitaendelea kusifu Yesu kwa furaha
5. Na saa zinapita, nangoja asubuhi utakaponiita, niende kwako juu. Nitasimama kwa amani mbinguni mbele yako, Yesu.

W. Sencer Walton




35 NIMEFIKA kwake Yesu

35

1. Nimefika kwake Yesu, Na rohoni mwangu sasa, jua lake la neema linang’aa kila siku.

Pambio:
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.

2. Pepo za neema yake zinavuma ndani yangu, na mawimbi ya wokovu yananijaliza sasa.

3. Sasa Bwana Yesu Kristo amefanya kao kwangu. Nimepewa mfariji, Roho ya ahadi yake.

4. «Siku roho afikapo mtajua kwa hakika kwamba ninakaa kwenu», hivyo Yesu alisema.

5. Kweli, amefika kwetu, sasa yumo ndani yetu. Ujitoe kwake Mungu, aioshe roho yako!

6. Yesu atakapokuja katita utakatifu, nitafananishwa naye, nitamshukuru sana.

Pambio:
Zitakuwa nyimbo nyingi tuta’poingia mbingu, na milele tutaimba na kusifu Mungu wetu.


Werner Skibsted




36 YESU ameniokowa

36

1. Yesu ameniokoa, amenipa utulivu. Kwake ninaona raha, ninataka kumsifu.

Pambio:
Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.

2. Kwa furaha ninaimba wimbo mpya wa wokovu. Nisichoke kamwe hapa kumwimbia Mkombozi.

3.Ni habari za neema zakupasha pande zote. Mhubiri, enda mbio kufikia nchi zote!

4. Yesu, siku nita’kufa na maisha ni tayari, ‘nichukue kwako juu penye raha ya milele!

S.L. Oberholzer, 1885

 




37 BWANA Yesu aliniokoa kweli

37

1. Bwana Yesu aliniokoa kweli, ninataka kufuata yeye sasa. Kila siku nimtumikie vema, yeye anipaye roho kwa neema!

Pambio:
Nafuata njia nzuri ya Mfalme Yesu Kristo, Na katika njia hiyo Mwendo ni pamoja naye.

 

2. Sitaifuata njia mbaya tena, nimewekwa huru kweli naye Yesu. Kumtumikia ni furaha yangu, ananishibisha kwa fadhili zake.

 

3. Huko mbele ninaona mji mwema, nimeacha njia ndefu nyuma yangu. Nuru ya Babangu yaniangazia, nitembee kwa salama siku zote.

 

Henri Dixon Loes




38 NILIKWENDA mbali sana

38

1. Nilikwenda mbali sana, ‘kufuata njia mbaya, nikamsahau Yesu anayenipenda sana.

Pambio:
Nina raha na furaha, Yesu alinitafuta, akaniokoa kweli, mimi wake siku zote.

 

2. Na sikufikiri siku nitakapodhihirishwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na kuhukumiwa naye.

 

3. Dhambi zilinichokesha, nikageukia Mungu, akasema neno nzuri la amani na furaha.


Original Version:

Modified Version: