39 YESU ameingia katika roho yangu

39

1. Yesu ameingia katika roho yangu, amenifungulia kamba za dhambi zangu. Tena amenijaza Roho Mtakatifu. Ninamsifu sasa kwa wimbo mpya.

Pambio:
Yesu ni yote kwangu, yote na’pata kwake. Ameondoa dhambi, ametakasa mimi. Shangwe rohoni mwangu ni kama maji mengi, namshukuru sana Mwokozi wangu.

2. Siku si ndefu tena, kazi si ngumu sasa, njia yanipendeza, ‘kiwa nyembamba sana. Katika hali zote ninamwimbia Yesu, yeye Mfalme wangu, ninamsifu!

3. Katika mwendo wangu ninazidishwa shangwe, hata wakinicheka, mwovu akijaribu. Hima Mwokozi wangu atanyakua mimi toka machoni pao. Haleluya!

Ivar Lindestad




40 AMENIWEKA huru kweli

40

1. Ameniwaka huru kweli, naimba sasa: Haleluya! Kwa msalaba nimepata kutoka katika utumwa.

Pambio:
Nimeokoka, nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka. Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.

 

2. Zamani nilifungwa sana kwa minyororo ya shetani, nikamwendea Bwana Yesu, akaniweka huru kweli.

 

3. Neema kubwa nilipata kuacha njia ya mauti, na nguvu ya wokovu huo yanichukua siku zote.

 

4. Na siku moja nitafika mbinguni kwake Mungu wangu. Milele nitamhimidi na kumwimbia kwa shukrani.

 

 




41 SIKU nyingi nilifanya dhambi

41

1. Siku nyingi nilifanya dhambi, sikujua Neno la Mwokozi, sikujua maumivu yake kwa ‘jili yangu.

Pambio:
Bwana Yesu alinirehemu, dhambi zangu alizichukua. Namsifu Yesu kwa ajili ya msalaba.

2. Niliposikia Neno lake, moyo wangu ukalia sana. Nikaona maumivu yake kwa ‘jili yangu.

3. Bwana Yesu ni Mwokozi wangu, jua na Mfalme na uzima. Ninamhibidi kwa ajili ya msalaba.

William R. Newell, 1868-1956
Years I spent, R.S. 773




42 BWANA Yesu amevunja minyororo ya maovu

42

1. Siku nyingi nilifanya dhambi, sikujua Neno la Mwokozi, sikujua maumivu yake kwa ‘jili yangu.

Pambio:
Bwana Yesu alinirehemu, dhambi zangu alizichukua. Namsifu Yesu kwa ajili ya msalaba.

 

2. Niliposikia Neno lake, moyo wangu ukalia sana. Nikaona maumivu yake kwa ‘jili yangu.

 

3. Bwana Yesu ni Mwokozi wangu, jua na Mfalme na uzima. Ninamhibidi kwa ajili ya msalaba. William R. Newell, 1868-1956




43 JUU ya mwamba umejenga kanisa lako duniani

43

1. Juu ya mwamba umejenga kanisa lako duniani, umeliweka huru kweli katika damu yako, Yesu.

Pambio:
Juu ya mwamba, juu ya mwamba huru na safi umelijenga. Juu ya mwamba, juu ya mwamba, huru na safi tusimame!

 

2. Neema kubwa! Nimepata sehemu yangu kanisani. Vita ya roho imekwisha, umenijaza utulivu.

 

3. Kati’ hekalu lake Mungu nimefanyika jiwe hai. Ninashiriki mwili wake kama kiungo chake Kristo.

 

4. Ju’ ya msingi huo safi liwe kanisa lako zima! Vyote vikiondoka huku, litasimama, litashinda.

Charles P. Jones, Otto Witt, 1922




44 Tu watu huru

44

1. Tu watu huru, huru kweli katika Yesu Kristo. Tunahubiri neno lake kwa moto ‘takatifu. Tuendelee, mbele, mbele, tukashinde majaribu! Twapiga vita ya imani, tuvumilie yote!

 

2. Tu jeshi kubwa la askari, tu safi kati’ damu. Mfalme wetu, Yesu Kristo, ni kiongozi wetu. Kwa nguvu yake kubwa mno tutadumu hata kufa.Tuendelee, mbele, mbele, tumshukuru Mungu.

 

3. Kwa Yesu tuna uhodari na mamlaka kubwa, maana tunayaamini maneno yake yote. Kisima wazi, cha ajabu, kinatoka msalaba, tuliyakunywa maji yake, ni maji ya uzima.

 

4. Mbinguni nchi ya asili [raha], ya haki na amani, tuta’pofika huko juu tutamwimbia Yesu. Na kila chozi litafutwa na mkono wa Mwokozi. Kwa shangwe kubwa tutarithi ufalme wa ahadi.

Werner Skibsted




45 WAIZRAELI walika’ Babeli utumwani

45

1. Waisraeli walika’ Babeli utumwani, wakawa na huzuni tu kwa ‘jili ya sayuni.

Pambio
Hapo amri ilifika waliweza kuondoka, shangwe gani mioyoni mwao! Walitwaa vinubi vyao, wakaenda wanaimba hadi, hata kurithi nchi yao.

 

2. Vinubi havikubigwa wakati wa utumwa, na walikaa kimya tu mahali pa ugeni.

 

3. Walipotoka Babeli, ikawa kama ndoto; furaha nyingi rohoni, faraja na uheri.

 

4. Mataifa walisema: «Mungu umefanyaje? Watumwa wameondoka, wamewekwa huru»!

 

5. Katika ulimwengu hu’ ni wengi wafungwao. Uhuru ni kwa Yesu tu kwa kila a’miniye.

Pambio:
Ndiye ameleta amri: Tunaweza kuokoka, shangwe ku’kwa kila ‘aminiye! Njoo sasa, twa’ kinubi, tufuate kwa kuimba hata kuirithi nchi yetu!

Werner Skibstedt




46 HAIFAI kuyasumbukia mambo yatakayokua kesho

46

1. Haifai kuyasumbukia mambo yatakayokuwa kesho. Baba yangu anajua yote, ni vizuri nikumbuke hivyo. Yeye mwenye moyo wa upendo ananipa yafaayo kweli, kama sikitiko au shangwe, na amani yake kila siku.

 

2. Siku zote yu karibu nami, na neema anapima sawa. Achukuwa masumbuko yote, yeye aitwaye Mungu Baba. Kunitunza hivyo kila siku, mambo hayo ame’tadariki. Kama siku, kadhalika nguvu! Ni ahadi niliyoipewa.

 

3. Mungu, unisaidie tena ‘kaa kimya kwako siku zote! Niamini sana neno lalo, ‘sipoteze bure nguvu yako! Nakatika mambo yote huku nipokee kwa mikono yako nguvu na neema yakutosha, hata nitakapofika kwako!

Lina Sandell-Berg, 1865




47 NIKIONA udhaifu na imani haba

47

1. Nikiona udhaifu na imani haba, nikijaribiwa sana, Yesu anilinda.

Pambio:
Anilinda vema, anilinda vema, kwani Yesu anipenda, anilinda vema.

 

2. Peke yangu sitaweza kuambata yeye, pendo langu ni dhaifu; Yesu anilinda.

 

3. Mimi mali yake sasa, alinikomboa, alitoa damu yake; Yesu anilinda.

 

4.Haniachi kupotea, anilinda sana. Kila ‘mwaminiye kweli, Yesu amlinda 

R. Habershon




48 SIWEZI mimi kufahamu sana neema yake Mungu kwangu

 48

1. Siwezi mimi kufaamu sana neema yake Mungu kwangu, zamani nilikuwa mkosaji, lakini alinisamehe.

Pambio:
Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.

2. Siwezi mimi kufaamu sana upendo wake ‘kubwa mno; nimeamini neno lake kubwa kweli, na ninaona raha tele.

3. Siwezi kufaamu kazi kubwa ya Roho yake ndani yetu, anayeweza kufundisha mtu kutegemea Yesu.

4. Sijui mimi siku zangu tena za kutembea duniani. Na labda nitaona shida huku, taabu na huzuni nyingi.

5. Sijui mimi kama siku moja nitakuona kufa huku, au kwa hima nitabadilika, ajapo Bwana na mawingu.

James Mc Granaham
I know not why, R.S. 617




49 NJIA yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi

 49

1. Njia yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi, ninapo wema wake, sina shaka, hofu tena. Nina raha ya mbinguni, ninakaa kwa salama. :/: Na katika mambo yote ananitendea mema. :/: [br]

2. Njia yote naongozwa, namtegemea Yesu. Anilinda jaribuni, anitia nguvu pia. Nikiona kiu hapa, nikichoka safarini,:/: Mwamba uliopoasuka unabubujika maji. :/: [br]

3. Njia yote naongozwa kwa mkono wake bora, atanituliza tena kwa babake huko juu. Miguuni pake Yesu ninataka kusujudu,:/: Nakusifu yeye, kwani aliniongoza huku. :/: [br]

Fanny Crosby, R. Lowry, 1875
All the way my Saviour leads me, R.S. 445




50 SITASUMBUKA kwa kuwa Mungu ananitunza daima √√

50

Sitasumbuka kwa kuwa mungu ananitunza daima, anachukua mizigo yangu nyakati zote za mwendo.

Refrain:
Sijaiona nyingine siku jana imetoweka na leo mungu anazijua hitaji zote ninazo.

 

Sitasumbuka kwa kuwa mungu ni baba yangu kabisa, hawezi kunisahau mimi ingawa akijificha.

Refrain:
Sijaiona nyingine siku jana imetoweka na leo mungu anazijua hitaji zote ninazo

 

Sitasumbuka kwa kuwa mungu anishibisha neema, anipa yote yanifaayo kwa roho yangu na mwili.

Refrain:
Sijaiona nyingine siku jana imetoweka na leo mungu anazijua hitaji zote ninazo

 

Maua yote anayavika na ndege wote wa anga wanapokea chakula chao pasipo shamba na ghala.

Refrain:
Sijaiona nyingine siku jana imetoweka na leo mungu anazijua hitaji zote ninazo

 

Ninafurahi katika bwana, na kama ndege naimba. Najua kwamba nyakati zote babangu ananitunza,

Refrain:
Sijaiona nyingine siku jana imetoweka na leo mungu anazijua hitaji zote ninazo. 

________________________________________________________________________

 




51 NAONA amani Golghota alipo jitoa Mwokozi

51

1. Naona amani Golgotha alipojitoa Mwokozi,
:/:Na huko nina kimbilio kwa Yesu aliyejitoa.:/:

 

2. Sitaki ‘tamani fahari na dhambi katika dunia,
:/: Sababu wokovu ninao katika ‘jeraha ya Yesu. :/:

 

3. Aliziondoa kabisa mizigo na kamba ya dhambi.
:/: Na niliokoka halisi kwa neno la Mungu wa ‘hai. :/:

 

4. Maneno ya Mungu ni kwetu chakula na dawa ya roho,
:/: na nguvu ya kusaidia mkristo katika safari. :/:

 

5. Mimi sasa hekalu la Roho, anayemiliki moyoni;
:/: na Yesu ataniongoza kwa njia ya ahadi zake. :/:

 

6.Uliye dhambini ufike kwa Yesu Mwokozi wa wote!
:/: Anakunyoshea mikono ya pendo kukusaidia. :/:




52 KWASALAMA baba awalinda watu wake

52

1. Kwa salama Baba Mungu awalinda watu wake, hata nyota za mbinguni si salama kama wao.

 

2. Mungu awalinda hivyo katika upendo wake. Wanakumbatiwa naye, wanarehemiwa sana.

 

3.Hawavutwi toka kwake kwa furaha wala shida. Yeye ni rafiki ‘kubwa wa walio watu wake.

 

4. Wanalishwa, wanavikwa, wanafarijiwa naye. Hata nywele za kichwani zimehesabiwa zote.

 

5. Enyi kundi lake dogo, Mungu atawahifadhi! Na adui watashindwa kwa uwezo wake ‘kubwa.

 

6. Akitoa, akiwapa, baba yetu hageuki. Na mapenzi yake ndiyo: Wana wapatishwe wema.

 

Lina Sandell-Berg, 1856


 




53 KATI’ mikono yake Yesu ananilinda katika pendo

 53

1. Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika pendo kubwa ninapumzika sana. Sasa sauti nzuri itokeayo juu inanikumbukia mbingu na raha yake.

Pambio:
Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika pendo kubwa ninapumzika sana.

 

2. Kati’ mikono yake nitakaa daima, sitatetema tena, yeye ni uwezo wangu. Shaka sinayo sasa, wala sioni woga, hata ikiwa shida, Yesu anifariji.

 

3. Yesu Mwokozi wangu alikombo mimi, Ufa wa mwamba ule, nitapumzika humo. Katika saa ngumu ya majaribu tele ninasaburi’ona jua la asubuhi.

Safe in the arms of Jesus, R.S. 663




54 USIOGOPE mateso yako

54

1. Usiogope mateso yako, Mungu anakulinda, bali tazama mapenzi yake,

Pambio:
Mungu anakulinda Mungu anakulinda siku kwa siku njiani mwake. Anakulinda salama. Mungu anakulinda.

 

2.Ukichukuwa mizigo ‘zito, Mungu anakulinda, kati’ hatari za njia yako Mungu anakulinda.

 

3. Anakumbuka hitaji zako, Mungu anakulinda. Utashiriki ujazi wake, Mungu anakulinda.

 

4. Katika njia ya migogoro, Mungu anakulinda. Mfunulie fadhaa zako, Mungu anakulinda.

Cevilla D. Martin, 1904
Be not dismayed, R.H. 458




55 TUPATE kwa nani faraja ya roho




56 YESU ninakutolea vyote

 56

1. Yesu, ninakutolea vyote ninakuwa navyo, nikupende, nifuate wewe siku zote hapa!

Pambio:
Ninakupa vyote, ninakupa vyote, Bwana Yesu upendwaye, ninakupa vyote.

 

2. Miguuni pako, Yesu, ninakusujudu sasa. Ninakutolea vyote: roho, moyo na maungo.

 

3.Najitoa kwako, Yesu, nafsi yote iwe yako! Bwana Yesu, nakusihi: Niwashie moto wako!

 

4. Yesu, ninakupa vyote, unijaze Roho yako! Nisikie moto wako ukiwaka ndani yangu!

 

5. Vyote ninakupa, Bwana, viwe mali yako kweli! Na fahari ya dunia naiona ni ya bure.

J.W. van de Venter, 1896
All to Jesus I surrender,, R.S. 581




57 YESU uliye kufa kwa ajili yangu

 57

1. Yesu, uliyekufa kwa ajili yangu, ninajitoa kwako, niwe mali yako! Bwana, nivute kwako, nifaamishe pendo, niwe dhabihu hai katika shukrani!

 

2. Yesu, nafika kwako, kao la rehema; Bwana, nitie nguvu kwa neema yako! Niuchukue tena kwa radhi msalaba, ni’tumikie wewe, Mkombozi wangu!

 

3. Bwana, uniumbie moyo haki, safi, kwako niishi tena hata kufa kwangu! Niwatafute wenye dhambi na udhaifu, niwapeleke kwako, Bwana wa upendo!

 

4. Vyote ninavyo huku nimepewa nawe, ukivitaka, Bwana, uvitwae vyote! Nina urithi wangu kwako mbinguni juu, nitakuona huko kwa furaha kuu!

S.D. Phelps, 1862
Evgt. 81More love to Thee,, o, Christ, R.S. 959




58 UNIPE raha tele kama mto

58

1. Unipe raha tele kama mto, nipite jangwa huku kwa furaha; unipe imani tena, Yesu, ningoje siku yako kwa bidii!

 

2. Kwa siku chache ninaona shida, dhoruba zinanisumbua huku. Napanda mbegu zangu nikilia, lakini nitavuna kwa furaha.

 

3. Kwa siku chache ninaburudishwa mtoni penye njia yangu huku, lakini siku kubwa itafika, nita’inywea chemchemi yake.

 

4. Kwa siku chache naitunza taa, nadumu kwa kuomba na kungoja. Na siku za uchungu ziishapo, nitamkuta Yesu huko juu.

Jane Crewdson




59 YESU ninakutolea moyo na maisha yangu

59

1. Yesu, ninakutolea, moyo na maisha yangu, niwe mfuasi wako, Safi na mtakatifu.

Pambio:
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:

 

2. E’ Mwokozi, nitakase, unijaze pendo lako. Na maisha yangu yote yawe yako, Bwana wangu!

 

3.Ninataka kuheshimu wewe, Mkobozi mwema; nifanane nawe, yesu, kati’ watu wa dunia!

 

4.Nikikaa kimya kwako kama yule Mariamu, nifundishwe nawe, Bwana, sitahangaika tena.

 

5. Tawi lake mzabibu, ulitunze na ‘safisha, ili kwa uwezo wako litaza’ matunda mengi!

 

Verner Skibstedt, 1930
Lord, I hear of show’rs, R.S. 277




60 NIHERI kuona ndugu njiani pa kwenda mbinguni

60

1. Ni heri kuonga ndugu njiani pa kwenda mbingu. Tukinyong’onyea sana kwa kuwa tu peke yetu, kushirikiana kwa ndugu kunaturudisha moyo, na Mungu atupa nguvu tukiyainua macho.

 

2. Twafungamana rohoni, tulio wa nyumba yake, huoni ulimwenguni kushirikiana kwetu. Na tuna Mwokokozi mmoja, imani ni moja pia, watoto wa baba ‘moja twashika sheria yake.

 

3. Furaha ya ulimwengu haitatuvuta tena, Twaona kung’aa kwake ni bure na bila kisa. Lakini tukikusanyika kwa jina la Mungu Baba, atuandalia kweli karamu ilio bora.

 

4. Tukivumilia hata ukomo wa mashindano, mbinguni tutawaona wakristo wapenzi wote. Hatutatawanyika huko, tu wote umoja kweli, milele tuta’pokaa nyumbani kwa Baba yetu.

Kirsten D. Hansen Aagaard, 1870




61 ENYI wetu wa Sayuni

61

1. Enyi watu wa Sayuni, kundi dogo la Mwokozi, Yesu aliwanunua kuwa mali yake Mungu. Sasa mnapita njia ya miiba na hatari kati’ nchi ya ugeni; bali mbingu mtafika.

 

2. Kumwamini, kumpenda Yesu ni uheri wetu; amri zote zinashikwa kwa upendo na amani. Kwa imani twaokoka, pendo ni uzima wetu. Yesu utusaidie, utujaze pendo lako!

 

3.Juu ya msingi huo, Yesu, unijenge mimi, na zaidi niungane nawe na kanisa lako! Sisi tu matawi yako, tushirikiane sana, na katika kundi nzima iwe nia moja kweli!

A.C. Rutström




62 MUNGU nivute kwako

62

1. Mungu, nivute kwako, karibu kwako, hata ikiwa shida ikinisukuma! Katika yote hapa ‘takuwa wimbo wangu: Mungu, nivute kwako, karibu kwako.

 

2. ‘Kiwa katika mwendo jua likichwa, giza yanizunguuka, peke yangu mimi, kwako, e’ Baba yangu, nafika, nakuomba: Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

 

3. Unionyeshe njia yakwenda juu, nijue kupokea yote toka kwako! Unifariji sana, niimbe tena hivi: Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

 

4. Katika mambo yote nikushukuru, majaribu’ pote nikumbuke wewe! Unifundishe hivi: Omba katika yote! Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

5.Nikimaliza mwendo wa msafiri, Mungu utaniita kwako huko juu. Na nitaimba tena kati’ watakatifu: Umenivuta, Mungu, karibu kwako!

Sarah Flower Adams, 1841
Near, my God, to Thee, R.S. 569




63 YESU nivute karibu nawe

63

1. Yesu, nivute karibu nawe, ‘kiwa kwa shida, ikiwa kwa raha! Uliyekufa msalabani, :/: ‘nifaamishe upendo na ne’ma! :/:

 

2. Yesu, nivute, mimi maskini, sina vipaji vya kukutolea, moyo ninao wenye udhaifu, :/: Uupokee, ‘uoshe kwa damu! :/:

 

3. Yesu, nivute, nikutolee yote ninayo, e’ Bwana mpendwa, ninakuomba: Uyaondoe :/: yote yanayo nitenga na Mungu! :/:

 

4. Yesu, nivute karibu nawe hata ukomo wa vita na shida! Tena mbinguni nitakuwapo :/: karibu nawe, e’ Yesu Mwokozi! :/:

Leila Morris, 1862-1929