64 KIMYA E’moyo wangu

64

1. Kimya, e’moyo wangu, mbele za Bwana Yesu! Unahitaji sana ‘kaa daima kwake. Njia salama ipi ulimwenguni huku bila kumfuata Yesu na neno lake?

Pambio:
Uniongoze, Bwana, katika njia yako! Hata ikiwa shida nitawasili kwako.

 

2. Kimya, e’moyo wangu, omba kwa tumaini! Nuru itatokea ukiamini Mungu, na umwambie Yesu shaka uliyo nayo, atakuosha sana, atakuonya njia.

 

3. Kimya, e’moyo wangu, msikilize Mungu! akuletea nguvu, tena hekima kweli. Na ukiendelea katika neno lake, Mungu atakujaza nguvu na uthabiti.

J. Mountain, 1922




65 HUKO ju’ ya nyota zote kuna chi yenye mema

65

1. Huko ju’ ya nyota zote kuna nchi yenye mema, Mji wake ni Yerusalemu; Dhambi haitakuwamo, wala kufa na huzuni, Kwake yesu nitapata kao.

Pambio:
Sikitiko na machozi hayatakuwako huko, Wala giza au vita ya dunia. Huko hatutayaona mambo ya kutuumiza. U Yerusalemu ‘takatifu!

 

2.Nifikapo mji huo nitaona Yesu kwanza, aliyechukua dhambi zangu. Nitaona uso wake, nitamshukuru yeye aliyeniweka huru kweli.

 

3.Huko nitaona tena jeshi la walioshinda kwa imani huku duniani, na pamoja nao wote nita’sifu Mungu sana juu ya neema yake kubwa.




66 WAKRISTO wa nchi zote watakusanyika huko kwa Yesu

66

1. Wakristo wa nchi zote watakusanyika huko mbinguni kwa Yesu, mezani pake, kati’ ufalme wake; kuona uzuri wake, kujazwa neema yake. Wataimba huko ju’ milele na milele.

Pambio:
Watoka bahari zote, watoka katika shida, watoka milima, watoka mabonde kufika kwa Mungu Baba, kuvikwa mavazi safi, kuona Mwokozi wao, yeye ali’wafilia ju’ ya msalaba.

 

2. Watakusanyika wengi walikotoka huku. Mateso na kufa, shida na giza hawata’ona kamwe. Ya kale hayatakuwa, lo! yote ni mapya huko! Itakuwa raha tu pamoja na faraja.

 

3. Tazama mlango huko uliokufunguliwa, na kuna mahali Yesu aita: « Njoo nyumbani kwangu wenzetu waliofika wanatungojea huko, malaika wanaimba kukukaribisha. Amanda Sandbergh




67 TUNAKARIBIA kao la mbinguni

67

1. Tunakaribia kao la mbinguni, hata jua likifichwa na mawingu. Tufuate Bwana Yesu siku zote, ni furaha yetu kumwandama yeye!

Pambio:
Tunakaribia mbingu kati’ yote, haleluya! ‘sifuni Mungu! Jipe moyo safarini kwani Yesu yu pamoja nasi hata mwisho!

 

2. Tunakaribia kao la mbinguni, hata tukiona pepo na dhoruba. Bwana yu karibu, na uwezo wake ni makimbilio yetu hatarini.

 

3.Njia yetu inapita kati’ jangwa, na miguu inauma mara nyingi, walakini tunakwenda tukiimba na kusifu Yesu, Mwokozi wetu.

 

4. Mwendo wetu utaisha siku moja, tutapata kustarehe huko juu. Tukiona shaka, shida hapa chini, tutapata utulivu kwake Yesu.

Pambio:
Tunakaribia mbingu kati’ yote, haleluya! ‘sifuni Mungu! Tunataka kufuata hata mwisho. E’ rafiki, utuandamie!

Nathan Cronsie, 1914




68 MBINGUNI kwa Mwokozi wangu mwema nitaamka asubuyi moja

68

1. Mbinguni kwa Mwkozi wangu mwema nitaamka asubuhi moja, Nitayaona majeraha yake, sauti yake nitaisikia.

 

2. Makao ya milele ni tayari, ali’waandalia watu wake. Tutamsifu Yesu sana huko, aliyetuokoa na hatari.

 

3.Na nyimbo za wokovu zinaimbwa mbinguni mbele ya Mwokozi wetu; tungesikia huku nusu ndogo, vitani tungepata ushujaa.

 

4. Lakini Yesu yupo nasi leo, usiku kama moto mbele yetu. Na neno lake, ni upanga wetu, ahadi ni safina ju’ ya maji.

 

5. Tungoje Yesu siku chache tena! Twakaribia mwisho wa safari. Tungoje asubuhi huko juu! Atatukaribisha Bwana Yesu!

Charlotte af Thibell




69 JE, Tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani

69

1. Je, tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani, na pamoja na wakristo ‘ona raha ya milele?

Pambio:
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!

 

2. Je, tutaonana tena, ba’da ya dhoruba zote huko katika bandari ya salama na amani?

 

3. Je, tutaonana tena kati’ mji wa dhahabu, Penye mto wa uzima nayo miti ya matunda?

 

4. Je, tutaonana tena na kusifu Mungu wetu miongoni mwa wakristo waimbao huko juu?

 

5. Tutaona na wapenzi waliotuacha huku? Je, tutawaona wote katika makao meme

 

6. Tutaona Bwana Yesu katika kutano huko, tutakaribishwa naye katika karamu kuu.

Th. Hastings




70 KUNA mji uko juu

70

1. Kuna mji huko juu, umejengwa naye Mungu, humo kuna mto ‘moja wenye maji mazima kabisa.

Pambio:
Tutakusanyika huko kwa raha penye mto mwema sana, tutakusanyika na wakristo penye mto wa maji mazima.

 

2.Huko pwani nchi nzuri, bila dhambi na huzuni, tutaimba nyimbo mpya, nyimbo njema ‘kusifu Mwokozi.

 

3. Kama twamwamini Yesu, kama hatufichi dhambi, kama moyo ni mweupe, tutafika mtoni pa mbingu.

 

4. Tu karibu ya kufika na kuona mto ule, Mungu atatupa raha na kutustarehesha daima.

R. Lowry
Shall we gather at the river, R.S. 664 




71 NIMEKWISHA kuingia nchi nzuri ya ahadi

71

1.Nimekwisha kuingia nchi nzuri ya ahadi, nchi njema ya wokovu wake Mungu. Huko ni vijito vingi vya baraka na furaha, huko shida haifiki.

Pambio:
Nimekwisha kuingia nchi nzuri ya ahadi. Moyo wangu hufurahi, ninaishi kwa neema.

 

2.Nimefika kanaani, hapo ni urithi wangu, na sitaki kuondoka tena kamwe. Sasa nira ni laini na mzigo si mzito, Yesu ni furaha yangu.

 

3.Nimekwisha kuingia nchi ya amani kuu, hata mwili wangu unatiwa nguvu. Nchi hiyo ni ya raha na faraja imo pia, hapo tunaka’ salama.

 

4.Nime’ngia nchi hiyo, ndiye Bwana Yesu Kristo, ninakaa tatika urithi wangu. Kwa imani ninakunywa maji hai ya kisima, huku ni furaha kubwa.

 

5.Nitafika hata mbingu, nchi ya hazina yangu, dhambi na mateso hazitakuwako, wala giza ya usiku, wala sikitiko chungu, wala shida, wala kufa. Werner Skibsted




72 MIMI mgeni katika dunia

72

1. Mimi ngeni katika dunia, ninasafiri kufika mbinguni. Hata ikiwa hatari njiani, nitaishinda pamoja na Mungu. Kama Ibrahimu majaribuni nita’vyoshinda kwa nguvu ya Mungu. Nitavumilia nifike mbinguni, ndilo kusudi la moyo.

 

2.Nikitembea gizani kabisa mimi mnyonge pamoja na Yesu, na nikipita motoni, majini, nakusudia kufika mbinguni. Mungu ajua mapito jangwani, naye Mwenyezi atanifikisha. Nitavumilia nifike mbinguni, ndilo kusudi la moyo.

 

3. Tusisumbuke katika safari, tuwatazame wali’tangulia! Yesu Mwokozi alitukomboa, msalabani alitufilia! Naye atatufikisha mbinguni; hivi tuimbe kwa mda kitambo: tutavumilia tufike mbinguni, ndilo kusudi la moyo!




73 NAJUA njia moja ya ku’fikia mbingu

73

1.Najua njia moja yakufika mbinguni, ingawa ikipita katika majaribu, lakini iendako mjini huko juu, :/: Na njia hiyo Yesu. :/:

 

2.Najua na amani iliyo ya milele, huwezi kuipewa kwa fedha na dhahabu; ni tunu ya rehema iliyotoka Baba. :/: Amani hiyo Yesu. :/:

 

3.Najua nguvu moja yakuniponya roho, initiayo raha, amani na faraja, inanilinda vema na nguo yangu safi, :/: Na nguvu hiyo Yesu:/:

 

4.Najua na kifiko mbinguni huko juu, na siku ni karibu kita’poonekana. Yafa’kukaza mwendo, kupiga mbio sana! :/: Kifiko ni mbinguni. :/:

Hildur Elmers, 1894




74 MGENI mimi hapa mahali pa ugeni

74

1. Mgeni mimi mahali pa ugeni, na kwenda mbali mno katika nchi nzuri. Na ni mjumbe huku kutoka Mungu wetu, nina habari ya Mfalme.

Pambio:
Habari yake nzuri sana, furaha yao malaika: «Mpatanishwe sasa na Mungu Baba yetu»! Habari yake ndio hiyo.

 

2. Salamu ya Mwokozi kwa kila mtu hapa: Urudi kwake Mungu, utoke utumwani! Ufike kwake Yesu, tubia dhambi zako! Habari hiyo ya Mfalme!

 

3. Mbinguni nchi nzuri, yapita vitu vyote, furaha huko tele na raha ya milele. Ukiamini Yesu uta’pokea huko. Habari hiyo ya Mfalme!

E.T. Cassel
I am a stronger here, R.S. 75




75 NILIE msafiri

75

1.Niliye msafiri, mgeni duniani; sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni. Ninatamani nami kukaa siku zote pamoja naye Baba katika utukufu.

Pambio:
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri wa binguni wapita yote huku.

 

2. Mwokozi yuko huko, rafiki yangu mwema, aliyenikomboa na ku’chukua dhambi. Na hata nikiona furaha siku zote ningali natamani makao ya mbinguni.

 

3.Na nikipewa huku vipawa vya thamani, na wakiimba nyimbo za kunifurahisha, rafiki wangu wote wakipendeza mimi, ningali natamani makao ya mbinguni.

 

4.Upesi nitaona kifiko cha mbinguni, Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha; Na huko nitaona nilivyotumaini, kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.

Lina Sandell-Berg, 1868
Home, home, sweet home





76 MGENI mimi

76

1. Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini. Msinipinge, niwafuate watakatifu walioshinda! Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini.

 

2. Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu. Na kwa mkono natwaa gongo, nazo silaha nimejivika. Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu.

 

3. Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya. Machozi, kufa, maombolezo sitayaona mbinguni tena. Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya.

 

4. Mchunga mwema, ninakuomba, ‘tangulie, niongoze njia yote, kwa kuwa giza na dhambi tena zaniwekea mitego mingi! Mchunga mwema, ninakuomba, ‘tangulie, niongoze njia yote!




77 NAIFUATA njia ya ku’fikia mbingu

77

1. Naifuata njia ya kufikia mbingu na mji mwema ule alio’jenga Mungu. Ninasafiri sasa kutoka duniani nifikie nchi hiyo ya raha na uzima.

Pambio:
Naifuata njia ya ku’fikia mbingu na mji mwema ule alio’jenga Mungu.

 

2. Sijauona bado uzuri wake bora wa mji wa mbinguni, usio na machozi; lakini siku moja, kwa shangwe ya milele nitamsifu Yesu katika mji ule.

 

3. Nifikapo mjini, mlango wake wazi, na hapo malaika watanikaribisha; shindano la dunia halitakuwa huko, na nitaona raha milele na milele.




78 NINAUZIMA wa milele

78

1. Nina uzima wa milele, na tumaini ni imara, mbinguni nitaona Yesu, Mwokozi wangu kwa furaha.

 

2.Nina urithi bora huko unaolindwa hata mwisho. Na kila siku ya jaribu natiwa nguvu naye Baba.

 

3.Namshukuru Mungu wangu! Ananitunza siku zote katika shida na taabu, kwa hiyo sisumbuki tena.

 

4. Rohoni mwangu ni amani, naimba kwa furaha kubwa. Nikiongozwa naye Yesu naendelea kwa salama.

 

5. E’ Bwana Yesu, unifunze ku’tumikia wewe vema wakati ubakio tena wa mwendo wangu dunianai!

Nils Frykman, 1883




79 MAISHA mafupi yahuku dunia

79

1. Maisha ya mtu [mafupi] ya hapa dunia yanaifanana safari chomboni. Twapita bahari katika hatari, lakini Mwokozi anatuongoza.

Pambio:
Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.

 

2. Twapita katika baridi na pepo, maneno ya Mungu ni nuri gizani. Hatari na hofu na chombo kibaya hatuta’kumbuka karibu na Yesu.

 

3.Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu, tunakaribia bandari upesi. Na humo hakuna dhoruba na pepo; safari tutaimaliza salama.

 

4. Tutakapofika bandari ya mbingu tutamshukuru Mwokozi mkuu. Hatutaziona hatari na hofu karibu na Yesu mwenyewe mbinguni.




80 ZITAKAPOTIMIA siku zahuduma yangu nitaona asubuhi ya uzima

80

1. Zitakapotimia siku za huduma yangu, nitaona asubuhi ya uzima. Huko juu mbinguni nitamwona Bwana Yesu, Na karibu yake nitaisikia.

Pambio:
Nitamtambua yeye, na karibu ya Yesu nitakaa. Nitamtambua yeye kwa alama za majeraha yake.

 

2.Itakuwa furaha kuona uso wake, na uzuri utokao macho yake. Moyo utafurika na uheri na furaha, ju’ ya kao aliloniandalia.

 

3.Na walio mbinguni wananingojea kwao, nakumbuka siku tulipoachana. Wataimba kabisa kunikaribisha huko, walakini nitamwona Yesu kwanza.

Fanny J. Crosby
When my life-work is ended, R.S. 364




81 ALIPOKUFA Yesu ju’ ya musalaba

81

1. Alipokufa Yesu ju’ ya msalaba wake akaishinda dhambi na uwezo wa shetani. Aliniweka huru, niwe mbali na hatia; na tena atanichukua kwake.

Pambio:
Mbinguni niendako haitakuwa dhambi, ni nchi nzuri ya salama mno. Na Bwana, Mungu wetu, atatuangazia; tukusanyane sisi sote humo!

 

2.Ninafuata njia ya Mwokozi wangu sasa, aniongoza vema, anafuta kila chozi. Ananilinda katika hatari za njiani, karibu naye vita yatulia.

 

3. Mbinguni nchi yangu, na bendera ni upendo, na Roho arabuni ya urithi wangu huko; na neno lake ni chakula changu safarini; neema inanipeleka kwake.

Carl Widmark, 1912




82 NINAJUA chi nzuri

82

1. Ninajua nchi nzuri, huko Mungu alifanya nyumba na makao kwetu; natamani kufikako.

Pambio:
Mbinguni, kao la malaika! Mbinguni, vyote vinamulika! Mbinguni Mungu atualika tukusanyane mbinguni kwake!

 

2. Katika safari yangu ninajiuliza sana kama nami nitafika penye Mungu ndie jua.

 

3. Kwa neema yake kubwa nitakaa kwake Mungu, Bwana Yesu atanipa taji nzuri ya uzima.

 

4. Sasa ninapiga mbio, nifikie nchi hiyo ya uzima na furaha, nchi ya tamani yangu!

Eric Bergqvist, 1903




83 NINAJUA nchi uko juu

83

1. Ninajua nchi huko juu, hapo Mungu alijenga mji, na aita ‘moma moja kwake, waliomaliza mwendo huku.

Pambio:
Shida, kufa na huzuni hazitakuwapo huko. Yesu atafuta kila chozi, tutaona shangwe, nayo tele.

 

2. Huko hawataingia kamwe wenye dhambi, wala cha kinyonge, E’ rafiki, ujihoji leo kama wewe utaona mbingu!

 

3. Utazame, mto ungaliko uwezao kusafisha sana! Ujioshe kati’ damu safi ya Mwokozi wetu Yesu Kristo!

 

4. Nafurahi kwani ninajua kao langu liko huko juu, natamani sana kufikako. Njoo, Yesu, unitwae mbio.

Mathilde Wiel-Öjerholm




84 NINAKUMBUKA sayuni

84

1. Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri mbinguni, bahari kama kioo na’furahia rohoni. Nyuma kimeta cha nuru Naona mji wa mbingu, nyimbo za nyumba ya Baba nasikiliza daima.

Pambio:
Mapambazuko mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.

 

2. Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu, naye aliwakomboa wote; wafalme, watumwa. Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida; mbavuni mwake nafasi kama bandari salama.

 

3. Kuna ‘jaribu njiani, mengi yakunizuia, na mara nyingi miiba, inaumiza miguu. Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa, mbingu ninaitazama na ku’himiza safari.

Th. B. Barrat, 1904




85 TWAPASHA habari ya mbinguni

85

1. Twapasha habari ya mbingu, mahali pa watu wa heri, na tunatamani ku’ona ufuko wa nchi ya mbingu.

Pambio:
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.

 

2. Twapasha habari ya mbingu na mji mzuri ajabu, na jeshi la watakatifu waliomaliza safari.

 

3. Twapasha habari ya pendo, amani na nguo nyeupe. na raha baada ya vita, makao karibu na Mungu.

 

4. Twapasha habari ya Yesu, alituokoa na dhambi. Ingawa ni shida njiani atatufikisha mbinguni.

Elisabeth Mills, 1829




86 TUTAONA furaha mbinguni

86

1. Tutaona furaha mbinguni, ni makao ya watu wa heri. Tutakuwa pamoja na Mungu na kusifu Mwokozi wetu.

Pambio:
Tutafurahi na tutaabudu huko juu kwake Mungu. Tutafurahi na tutaabudu siku tutakapofika.

 

2. Mara nyingi furaha ya hapa yapinduka machozi machongu, walakini hazitakuwapo sikitiko na shida huko.

 

3. Kama shida na shaka zafika kuzuia safari ya hapa, tutazame daima mbinguni, huko juu ni raha yetu!

Robert Harkness




87 MWSHO wanjia ya Mungu ni mbingu

87

1. Mwisho wa njia ya mkristo ni mbinguni; Yesu ananiongoza salama. Kama shetani akinijaribu nakitazamia kifiko.

Pambio:
Kwetu mbinguni hatutatawanyika, dhambi na mateso hayatakuwapo, Na hatutaona machozi na shida, ila furaha milele.

 

2. Tutawaona walioishinda dhambi, shetani na mambo mabaya, na tutaona Mwokozi mpenzi; tutafananishwa na yeye.

 

3.Nani ataka kufika mbinguni? Yesu ni njia, uzima na kweli. Njoo kwa Yesu! Akuandalia kao la milele mbinguni.

 

4. :/: Malaika wanangoja:/: malaika wanangoja huko mbinguni! :/: Malaika wanangoja:/: kutusalimu: «karibu».




88 MPONYI apitaye wote amefika hapa

88

1. Mponyi apitaye wote amefika hapa. Awaponyesha watu moyo. Yesu wa upendo.

Pambio:
Jina linalopita yote juu na chini pote pia, jina kubwa, jina jema: Yesu wa upendo.

 

2. Awasamehe watu dhambi wakizitubia, awapokea kwa neema, waipate afya.

 

3. Tukiwa na masikitiko, Yesu afariji. Akitubarikia sana, woga waondoka.

 

4. Watoto walipenda sana jina lake Yesu, liwalindalo na mabaya, wakijaribiwa.

 

5. Shetani aogopa sana jina lake Yesu. Katika vita ju’ ya dhambi latutia nguvu.

 

6. Mbinguni tena kwa furaha tutamwona Yesu. Tutasahau shida zote, tutamshukuru.