1. Imba habari njema: Mungu apenda wote! Uihubiri damu ituponyayo roho! Taja karama kubwa: Mwana alitujia, pasha habari hiyo kwa kila mtu!
Pambio: Yesu msalabani alifilia wote, alitupatanisha na Mungu, Baba yetu. Pazia la hekalu likapasuka huko, njia imefunguka kwa wewe, nami!
2.Uwaimbie wenye shida na sikitiko na wapigao vita katika majaribu! Imba katika miji, pasha habari njema: Yesu awatafuta kwa pendo kubwa!
3.Imba katika giza, lisipofika jua, uwaimbie wote, watu wa kila bali! Imba mapema sana, na adhuhuri pia, sifu Mwokozi hata usiku waja!
Elsa Eklund, 1918?
115 PENDO la Mungu ni kubwa
115
1. Pendo la mungu ni kubwa, pasha habari hiyo! pendo la Mungu ni kubwa, mwanzo wa nyimbo zote. malaika waliimba wachunga wakasikia. tunafurahi kujua pendo la mungu ni kubwa.
refrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
2. Pendo la mungu ni kubwa kwako uliye mbali. pendo la Mungu ni kubwa, anakuhurumia. ukiendee kisima kinachotoka golgotha, utaupata uzima katika pendo la mungu.
Refrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la mungu ni kubwa!
3. Pendo la mungu ni kubwa, latufikisha mbingu, pendo la Mungu ni kubwa, tutafurahi sana! huko hakuna jaribu wala ugonjwa na kufa. tumeokoka sababu pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
4. Pendo la mungu ni kubwa, pasha habari hiyo! pendo la Mungu ni kubwa, mwanzo wa nyimbo zote. malaika waliimba wachunga wakasikia. tunafurahi kujua pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
5. Pendo la mungu ni kubwa kwako uliye mbali. pendo la Mungu ni kubwa, anakuhurumia. ukiendee kisima kinachotoka golgotha, utaupata uzima katika pendo la mungu.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
6. Pendo la mungu ni kubwa, latufikisha mbingu, pendo la mungu ni kubwa, tutafurahi sana! huko hakuna jaribu wala ugonjwa na kufa. tumeokoka sababu pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
116 TUIMBIE tumsifu Yesu ju’
116
1. Tuimbie, tumsifu Yesu ju’ya msalaba! Aliteswa na akafa, yote kwa ajili yetu. Akashinda, ‘kafufuka, ni Mwokozi ‘kamilifu.
Pambio: Yesu alitukomboa, na akawa haki yetu. Dhambi aliziondoa, akatupa tumaini: Tutarithi utukufu, nuru, raha na uheri.
2. Yesu alipofufuka akatushindia kufa, akapewa nguvu zote duniani na mbinguni. Sisi sote tumepona kwa kupigwa kwake Yesu.
3. Tushukuru Mungu Baba kwa ajili ya upendo! Tumsifu Yesu Kristo kwa neema yake kubwa! Tumfungulie moyo kwake Roho ‘takatifu!
Venatius Fortanus, env. 600
117 NILIPOFIKA Golgotha
117
1. Nilipofika Golgotha nikaiona huko neema kubwa kama mto, neema ya ajabu.
Pambio: Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne’ma tele na ya milele, ne’ma ya kutosha!
2.Nilipofika moyo wangu ulilemewa sana, sikufaamu bado vema neema yake kubwa.
3.Nilipoona kwamba Yesu alichukua dhambi, neema ikadhihirika, na moyo ukapona.
4. Mbinguni nitakapofika, furaha itakuwa kuimba juu ya neema milele na milele.
E.O. Excell, 1905
118 NI MWOKOZI mzuri ninaye
118
1. Ni Mwokozi mzuri ninaye, alikufa kunikomboa. Alitoa uzima wake kwa ajili ya watu wote.
Pambio: Alikufa msalabani, alikufa msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa msalabani.
2. Aliacha makao juu, akafika ulimwenguni; aliteswa kwa’jili yangu na kunifungulia mbingu.
3.Dhambi zangu ali’chukua, kujitwika hukumu yangu, na alijeruhiwa ili aniponye na ‘nipa raha.
4. Bwana Yesu alifufuka, akarudi mbinguni kwake; na yuaja upesi tena achukue walio wake.
F.A. Graves
119 TUIMBIE msalaba wa Mwokozi
119
1. Tuimbie msalaba wa Mwokozi, damu yake inatusafisha sana! Tunaweza kuwa huru, kwani Yesu alikufa ili ku’ondoa dhambi.
Pambio: Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!
2. Twafurahi kwa neema yake kubwa, alikuja ili tuwe na uzima. Kama njia ni nyembamba duniani, Yesu atatupa nguvu na ‘hodari.
3. Tuuimbe moto ule ‘takatifu uli’tupwa na Mwokozi duniani! Tuvipige vita vilivyo vizuri, nasi tutapewa taji ya uzima!
120 MSALABANI nilimuona Yesu
120
1. Msalabani nilimwona Yesu, Mwokozi wangu aliyeniponya; rohoni mwangu giza ikatoka, ninafuata Yesu sasa.
Pambio: Nimeokoka kutoka dhambi, na siku zote ninaimba kwa furaha. Ni vita kali kushinda yote, lakini Yesu yu karibu.
2. Mwokozi wangu ananipa nguvu, nikiuona udhaifu huku. Na vita yote itakapokwisha, nitaipata raha kwake.
3. Mwokozi wangu, ninakufuata, furaha yako inanituliza. Na siku moja utakuja tena kunichukua huko kwako.
121 YESU nifuraha yangu
121
1. Yesu ni furaha yangu, amejaa pendo kweli. Anaweza kusimika kila mwenye udhaifu. Ananipa ujasiri, nguvu, raha na faraja. Hata nikionja kufa, Yesu ni mchunga wangu.
2. Nimefungwa na Mwokozi kwa kifungu cha upendo, hata kufa hakuwezi kunitenga naye Yesu. Mimi wake siku zote, ninataka kumtii. Kwa neema nimepona, nisitumikie dhambi.
3. Kwa mikono ya upendo ninakumbatiwa naye, sitaweza kutafsiri pendo lake kubwa kwangu. Napokea nguvu yake, yanijaza moyo wangu. Yesu ananiongoza katika safari yangu.
Torvald Löwe
122 MWOKOZI kamili ni Yesu pekee
122
1. Mwokozi kamili ni Yesu pekee, Mwokozi mzuri halisi. Katika wokovu wa Mungu mkuu ninalindwa naye kabisa.
Pambio Katika wokovu nalindwa salama, naishi kwa maji ya ‘hai. Upendo wa Mungu unanizunguuka :/: na kanihifadhi daima. :/:
2. Baraka ya mbingu inanijaliza kwa Roho ya utakatifu. Nasifu Mwokozi katika furaha, wokovu umenifikia.
3. Mwokozi mzuri ni Yesu pekee, aniondoaye mizigo. Njiani ananiongoza vizuri, anipa na nguvu ya mwendo.
4. Nitakapomwona Mwokozi mbinguni baada ya shida za huku, Nitamhimidi na kumshukuru Bwana ninayempenda.
Fanny J. Crosby, 1903
123 MWOKOZI mzuri ninaye
123
1. Mwokozi mzuri ninaye, zamani sikumfahamu, na sasa ninamhubiri, wengine wapate kuona.
Pambio: Wote watamwona, wote watamwona Mwokozi mzuri ninaye; Lo! Wote watamwona.
3. Apita wo wote kwa wema, mfano ‘tukufu wa Baba, lakini anitaja ndugu, niliye maskini kabisa.
4.Natoa maisha na pendo kwa Yesu aliyenipenda. Katika ishara za Mungu upendo wapita yo yote.
Carrie E. Breek, 1902 I have such a wonderful Saviour, R.H. 640
124 NAONA pendo kubwa mno
124
1. Naona pendo kubwa mno, latoka kwa Mwokozi wangu, ni tele kama maji mengi yatembeayo baharini. Lanitolea tumaini yakwamba nitatiwa nguvu; na niwe mhodari tena kwa pendo kubwa la Mwokozi!
Pambio: Haleluya! Ni pendo kubwa linalotoka moyo wako! E’ Mungu wangu nakuomba: Nijaze pendo lako tele!
2. Na pendo hilo kubwa mno huyaondoa majivuno, na kunifunza haki kweli, uongo wote niuvue! Hunituliza moyo wangu, huruma nayo hunitia. Na sote tuwe na umoja katika pendo la Mwokozi.
3. Nijazwe pendo hilo kubwa, linibidishe siku zote! Rononi niwe na juhudi nitumikie Bwana Yesu! …
Hazina yako ‘nipeleke kwa watu waliopotea, wafahamishwe pendo kubwa ulilo nalo, Mungu wangu!
A. Playle, 1899
125 HALELUYA! nafurahi
125
1. Haleluya! Nafurahi, ninaimba kila siku sifa zake Mungu wangu, aliyeniweka huru. Haleluya! Bwana Yesu aliniokoa kweli! Haleluya! Mimi wake, yeye ni Mwokozi wangu!
2. Heri! Nilieokoka kwa neema yake kubwa ninataka kumsifu Mungu na wokovu wake. Wakinung’unika wote, sitawafuata wao; nitasifu Mungu wangu siku zote na milele.
3. Kama ndege waimbavyo asubuhi bustanini, Na sauti ya mawingu ivumavyo baharini, hivyo nitamshukuru Bwana wangu kwa furaha. Roho yangu itaimba: Haleluya! Sifu Mungu!
4. Haleluya! Furahini mbele yake Mungu wetu! Na watakatifu wote, mwimbieni jina lake! Malaika wote pia, ……msifuni Bwana Mungu! Mbingu zote zitajibu: Haleluya, Haleluya!
Einar Karlsson, 1917
126 E’MTAKATIFU Mungu wamajeshi
126
1. E’ Mtakatifu, Mungu wa majeshi, leo asubuhi tunaimba mbele yako! E’ Mtakatifu, Mungu wa rehema, Bwana Mwenyezi, tunakuabudu!
2. E’ Mtakatifu, huko ju’ mbinguni, lo! Wazee huzitupa taji mbele zako. Jeshi la mbinguni wanakusujudu uliye hai sasa na milele.
3. E’ Mtakatifu! Mtu mwenye dhambi hataweza kuuona utukufu wako. Wewe tu ni mwema, tunakuheshimu, E’ mwenye nguvu, pendo na uwezo.
4. E’ Mtakatifu, jina lako kubwa lisifiwe hapa chini, juu ya po pote! Mungu wa neema, nguvu na uwezo, mwenye baraka, tunakushukuru!
Dr. J.B. Dykes Holy, holy, holy, R.S. 25
127 NIMEUONA mto safi
127
1. Nimeuona mto safi, kisima cha ajabu, ni damu yake Yesu Kristo, inayonitakasa.
Pambio: Nimeuona mto safi uniosha moyo wangu. Namshukuru Mungu wangu, aliniweka huru kweli!
2. Kwa nia na dhamiri safi naendelea mbele, ninasafiri kwenda mbingu kuona raha yake.
3.Neema kubwa, nimeonja uheri mbinguni, maana damu yake Yesu imeniponya moyo!
Mrs. Pheber Palmer The cleansing bood, Sgt. 18. MA.
128 NINA rafiki mwema
128
1. Nina rafiki mwema, naye alinifilia; alinivuta kwake na amenifanya mpya. Ni mali yake Yesu tu, ninaongozwa naye, alikomboa mimi kwa agano la upendo.
2.Nina rafiki mwema, na aliondoa dhambi, aliniweka huru na kunipa Roho yake. Na vitu vyote ninavyo ninavitoa kwake, maisha yangu ni yake, yaimba sifa zake.
3.Nina rafiki mwema na anayeweza yote, pamoja naye Yesu tu nashinda majaribu, atanitwaa kwake ju’ mbinguni kwa furaha; Nitastarehe katika makao ya milele.
J.G. Small I have a friend,
129 NINATAKA kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote
1. Ninataka kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote. Twende sote sasa tumsifu Yeye, na pendo kubwa la Mwokozi! Haleluya! Yu Mfalme ‘kuu!
Pambio: Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!
2.Na baraka yake anaimimina, kama mvua inyeshavyo juu yangu. Nastarehe mikononi mwake Yesu, rehema yake inatosha.
3. Siku moja nitamwona Yesu Kristo kati’ nchi nzuri sana ya furaha, macho yangu yatamtazama yeye, kuona sura ya Mfalme.
Albert Simpson Rietz
130 NINATAKA kumsifu Yesu
130
1. Ninataka kumsifu Yesu, Bwana wangu mwema. Aliteswa hata kufa, ili niwe huru kweli.
Pambio: Mwimbieni Bwana Yesu kwa upendo wake ‘kubwa! Alilipa deni langu, nimewekwa huru kweli.
2. Ninataka ‘shuhudia pendo kubwa la Mwokozi, jinsi alivyoniponya nilipopotea mbali.
3. Ninasifu Mwokozi kwa uwezo wake bora; naye anitia nguvu nimshinde yule mwovu.
4. Ninataka kumwimbia Yesu Kristo, Bwana wangu. Aliniokoa kweli, niwe heri siku zote.
Philip P. Bliss, 1838-1876
131 MIMI mukristu
131
1. Mimi mkristo nita’vyokuwa katika yote mpaka kufa. Mimi mkristo, ‘navyoshuhudu, dunia yote ikinicheka. Mimi mkristo kwa moyo wote sababu ninampenda Kristo, aliyekufa kwa ‘jili yangu. Anastahili kupendwa nami.
2. Mimi mkristo, neema kubwa! Niliokoka kutoka dhambi. Mimi mkristo, hata ikiwa katika shida na mapigano. Mimi mkristo, na ni askari, nafanya vita kushinda dhambi. Akida wangu ni Bwana Yesu, pamoja naye ‘tashinda yote.
3. Mimi mkristo, na ni mgeni, nimeifunga safari yangu; na sitamani yaliyo huku, ninatafuta yaliyo juu. Mimi mkristo na nchi yangu ni huku juu katika mbingu, hamna njaa na shida humo. Wakristo wote washiba mno
4. Mimi mkristo! Ni neno zuri la kufariji moyoni mwangu linanitwaa ju’ ya huzuni, nipumzike kwa Mungu wangu; Mkristo katika kila hali, na nikiitwa na kufa tena, kwa raha kubwa nitakubali kuchukuliwa mbinguni juu.
Joseph Grytzell, 1892
132 YESU mwokozi unanipenda
1. Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako ni kubwa kabisa. Ulinivuta karibu nawa, Mimi ni wako daima dawamu.
2. Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako lapita akili. Linanifunza kuzifahamu raha, upole na utu adili.
3. Yesu Mwokozi, unanipenda, mimi maskini, dhaifu, mnyonge. Nimetakaswa kwa damu yako; ninakuomba, ‘nijaze upendo!
4. Yesu Mwokozi, unanipenda, umenitilia wimbo kinywani wa kukusifu hata milele, nitakuona halisi mbinguni.
133 UFURAHI moyo wangu
1. Ufurahi, moyo wangu, heri nyingi umepata! :/: Sikitiko limekwisha, Yesu ni wangu nami wake. :/:
2. Ameponya roho yangu, yeye ni mponyaji mwema; :/: Na kwa Roho ‘takatifu anabatiza watu wake. :/:
3.Jina langu ni mbinguni, Yesu ameliandika. :/: Mimi mali ya Mwokozi hata milele na milele.:/:
4.Na moyoni mwangu sasa ninaimba: Mungu, Baba! :/:Ni furaha kubwa sana, nina rafiki kila saa. :/:
5.Nimeondolewa dhambi, nisitende ovu tena! :/: Kwani Yesu aokoa kila wakati na dakita. :/:
6.Nyimbo za kusifu Mungu zinajaa mbingu zote. :/: Moyo wangu unajibu: Amina. Mungu asifiwe» :/:
Emil Gustavsson, 1887
134 WETU wa Mungu
1. Watu wa Mungu, mshangilieni kabisa, na mwimbieni Mfalme wa mbingu na nchi! Mungu yu nasi kwa pendo kubwa, kamili ili tupate wokovu.
2. Ona ajabu! Mwokozi aliyejidhili! Pendo kamili na neema nyingi ya Mungu: Alizaliwa, akawa mwana Adamu, atukomboe na dhambi!
3. Sisi wakristo tumwimbie tena pamoja Yesu Mwokozi aliye dhabihu ya kweli! Na atukuzwe hapa na huko mbinguni, kwani alitufilia!
4. Yesu Mfalme, kwa pendo uliniokoa, nikufuate, nikutumikie daima! Huko mbinguni nitakusifu milele katika watakatifu.
2.Sina nguvu, ni dhaifu bila Yesu Mwokozi, ila kwa nguvu zake nasimama imara.
3.Moyo wangu, ufurahi, mimi mtu wa Yesu! Nampenda daima na kumtumikia.
4.Pendo kubwa la Mwokozi lanijaza rohoni. Nina raha kamili, moyo unastarehe.
5.Sifu Mungu, Baba yetu, Yesu Kristo Mwokozi, Roho Mtakatifu! Haleluya, Amina!
138 SASA tayari kwetu siku yakuokoka
1. Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka, Yesu alitimiza yote msalabani. Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao, wapate kustarehe, wapone nafsi zao.
Pambio: Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.
2. Wewe kwa damu yako ulikomboa sisi, na jua la neema linatuangazia. Tumefahamu sasa pendo la Mungu wetu. Damu imetuunga kati’ agano jipya.
3. Njoo upesi nawe uliyesitasita! Mungu atakujaza neema yake kubwa, raha rohoni mwako inayokutuliza, matumaini, nguvu, pendo lililo bora.
H. Schlager, 1925 Speak to my soul, Lord Jesus, R.S. 567