139 NINAFURAHA kubwa

1. Nina furaha kubwa, napumzika sana, kwa kuwa nimefika kwa Mungu, Baba yangu. Ameniweka huru na mbali na utumwa, na sasa nakaa salama.

 

2. Zamani nilidhani kuacha dhambi zote, lakini sikuweza kushinda peke yangu. Ninamwamini sasa Mwokozi wangu, Yesu, na yeye ananishindia.

 

3. Mwokozi wangu, Yesu, aliyenifilia, aliokoa mimi, angali anipenda; nahesabiwa haki katika damu yake, inayosafisha kabisa.

 

4. Na nikijaribiwa na mwili wangu tena, ninakumbuka Yesu, apita vitu vyote. Neema yake kubwa kuliko dhambi zangu. Ninamshukuru Mwokozi.

 

5. Na sasa Bwana Yesu akaa ndani yangu, neema yake kubwa yanizunguuka mimi. Sitasumbuka tena, nimejiweka kwake, na Mungu anilinda vema

 

6. Shetani akitaka kufanya vita sasa, sitaogopa yeye na mamlaka yake. Maneno yake Mungu, ni yenye nguvu sana kwa wote wanaoamini.

 

7. Ninaenenda sasa kwa jina lake Yesu, salama nitafika nyumbani mwa Babangu. Lakini safarini naimba siku zote, nikimshukuru Mwokozi.

Nils Frykman, 1881




140 UKICHUKULIWA na mashaka yako

1. Ukichukuliwa na mashaka yako na kuona hufu kwamba utakwama, uhesabu mibaraka yake Mungu, na utashangaa kwa rehema yake.

Pambio:
Uhesabu mibaraka yote Mungu aliyoyakubariki! Ukumbuke mambo yote pia, na utashangaa kwa rehema yake!

 

2. Na ukiudhiwa na huzuni nyingi, ukiona msalaba ni mzito, uhesabu mibaraka kuchwa pia, na kwa moyo wote utasifu Mungu.

 

3. Wengi watamani mali ya dunia; utajiri wako ni Mwenyezi Mungu. Uhesabu mibaraka na kumbuka: Mali haiwezi kufungua mbingu.

 

4. Na katika mambo yote huku chini ukumbuke pendo kubwa la Mwokozi! Na ujumlishe mibaraka yote, tena mwisho atakuchukua kwake!

Johnson Oatman Jr
When upon life’s billows, R.S. 5





141 MWOKOZI wetu anatupa furaha duniani

 

1. Mwokozi wetu anatupa furaha duniani, atuongoza kwa neema na anatushibisha. 

Tazama, yupo pamoja nasi, neema haitaisha kamwe !
Haleluya, haleluya, haleluya amina!

 

2. Ni vema kumupenda mungu aliyetukomboa, vizuri kuwa mtu wake, sitapotea kwamwe.
Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka.
Haleluya, haleluya, haleluya amina

 

3. Ikiwa giza mara nyingi, na jua likifishwa, na tukijaribiwa huku, twajua ni kwa muda.
Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena.
Haleluya, haleluya, haleluya, amina

 

4. Na tusisumbukie tena chakula wala nyumba, maana vyote twavipata kwa ne’ma yake mungu!
Njiani yote atuongoza, aichukuwa mizigo yetu.
Haleluya, haleluya, haleluya, amina

 

5. Ikiwa vema huku chini kutegemea yesu, furaha gani huko juu kuona uso wake!
Tutaiona furaha tele, nutukufu hautaisha
Haleluya, haleluya, haleluya, amina!

______________________________________________________________________

 




142 KWANAMNA nyingi nilitafuta kupata raha moyoni mwangu

1. Kwa namna nyingi nilitafuta kupata raha moyoni mwangu. Unyonge wangu haukukoma ila kwa Bwana Yesu.

 

2. Na moyo wenye hatia nyingi nilimwendea Mwokozi wangu, na alinipa wokovu wake na nguvu ya kushinda.

 

3. Kwa pendo kubwa Mwokozi wangu aliuweka uzima wake, si kitu mimi ulimwenguni, nina wokovu kwake.

 

4. Ijapo ninachukiwa huku ni mteule wa Bwana Yesu, napenda sasa kumfuata, nifike kwake Mungu!

 




143 HERI alisi

1. Heri halisi, Yesu ni wangu! Yeye mchunga, mimi ni wake. Heri yakini, yote ni heri, roho na moyo zimeokoka.

Pambio:
Yesu ni wimbo na raha yangu, nitamsifu hata milele! Na nitamwona huko mbinguni. Yesu ni wangu na mimi wake.

 

2.Nilijitoa kwa Bwana Yesu, na nilipewa wokovu wake. Huko mbinguni kuna furaha juu ya mtu aliyetubu.

 

3. Sasa naweza kusifu Yesu, na roho yangu inafurahi. Mimi si kitu mbele ya Mungu, bali ni heri. Namshukuru!

 

4.Nimebatizwa katika Roho, shangwe ya mbingu imo rohoni. Moto moyoni, pia kinywani, nashuhudia pendo la Mungu.

 

Fanny J. Crosby – Van Alstyne, 1873
Blessed assurance, R.S. 417




144 SAWA na kisima safi

1.Sawa na kisima safi, chenye maji mengi, mema, ni upendo wa Mwokozi ukaao ndani yake.

Pambio:
Yesu amelifungua lango zuri la mbinguni ili niingie humo kwa neema yake kuu.

2. Kama ndege awindavyo mara nyingi niliumwa, Moyo wangu ulilia, Yesu hakunifukuza.

3.Ni ajabu kubwa kweli, alinisamehe yote! Juu ya rehema yake ninaimba kwa furaha.

4.Asubuhi ya uzima nitafika mlangoni; kwa ajili ya upendo nitapata kuingia.

Fredrick Bloom, 1917




145 MUNGU wangu mkuu

1. Mungu wangu mkuu, wanijaza mwenyewe, na uzima u katika wewe. Nina raha moyoni na amani halisi, ninaishi katika upendo.

 

2. Sasa ninakusifu wewe, Yesu Mwokozi, unakaa rohoni daima. Kila ‘nachohitaji wanijaza kwa pendo. Wewe yote, na mimi si kitu.

 

3. Jina lako ni pendo, kulijua hakika kunafanya safari nyepesi. Mimi mtu dhaifu, ila kwako ni nguvu; niongoze katika safari!

 

4. Mbele ya uso wako giza yote yatoka; nuru inaangaza moyoni. Yamepita ya kale, sasa yote ni mapya. Ni maisha ya heri ajabu!

 

Joseph Gulseth, 1901




146 KARIBU nawengu nilipotea njia

1. Karibu na wenzangu nilipotea njia, rohoni mwangu njaa, na sikuona raha, lakini sasa Yesu ni Mchungaji wangu, naandamana naye siku zote.

 

2. Katika shamba lake nimefuata Yesu, ninapajua anapolisha kundi lake. Na penye maji hai napunzika sana, naona raha hapo siku zote.

 

3. Lakini mchungaji apita vitu vyote, uzima aliweka kwa ‘jili ya kondoo. Nikumbukapo Yesu, sioni tena kitu cha kupendeza ila yeye, Bwana.

 

4. Naimba kwa furaha rohoni mwangu hivi: « Upendo wako, Yesu, ninausifu sana!» Na jina lake Yesu ni kama manukato; ananilinda vema siku zote.

Lewi Pethrus




147 MWENYEZI Mungu wazamani

1. Mwenyezi Mungu wa zamani zote ni kimbilio la vizazi vyote. Katika vita anawashindia na ku’okoa watu wake wote.

Pambio
Mfalme ‘kubwa ndiye Mungu, vitani anatushindia. Kwa shangwe kubwa tumsifu na tumwimbie Mungu wetu!

 

2. Mwenyezi Mungu wa zamani zote aliokoa watu utumwani, kwa njia kavu katika bahari wakafikishwa ng’ambo kwa salama.

 

3. Mwenyezi Mungu wa zamani zote Karmeli alishinda yule Ba’li, akasikia ombi la Eliya, ‘katuma moto juu ya sadaka.

 

4. Mwenyezi Mungu wa zamani zote akawa naye Daudi vitani; aki’tupia jiwe Goliati, shujaa alikufa mara moja

 

5. Mwenyezi Mungu wa zamani zote, uovu wote utashindwa naye. Atamseta yule mdanganyi, shetani, chini ya miguu yake.

 

6. Mwenyezi Mungu wa zamani zote atuongoza kwa mikono yake; anatulinda hatarini huku, mbinguni tutafika kwa salama.




148 NGUVU ile ilishuka juu’ya wanafunzi

1. Nguvu ile ilishuka ju’ ya wanafunzi wote mjini mwa Yerusalem’ siku ya Pentekoste, lo! Nguvu hiyo ya Mwokozi ni sawa leo; shukuru Mungu!

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:

 

2.Yesu aliwapa ahadi: «Mtapokea nguvu». Na Roho akashuka na wakamsifu Mungu. Walio wenye udhaifu, wakahubiri kwa uthabiti.

 

3. Roho yule aingiapo anatutia nguvu, tupate kwa imani ku’ kushinda yule mwovu. Kwa moyo wenye moto safi tuite watu kwa Mkombozi!

 

4.Uingie sasa rohoni, uwashe moto wako, tupate kusimama kwa usafi siku zote! Ufike sasa kama mbele wakati huo wa Pentecoste!

Leila Morris, 1862-1929
The power that fell at Pentecost, R.H. 219




149 UZIMA ninao moyoni daima

1. Uzima ninao moyoni daima, uzima ni Yesu Mwokozi, aliyeingia rohoni hakika, akanitilia ‘hodari.

Pambio:
Nashiba rohoni kwa raha ya Mungu, na moto wa mbingu ulimo. Napata kukaa nuruni kabisa, na nuru ni Yesu Mwokozi.

2. Baraka zilizo katika wokovu nilizozipata kwa bure, nilipoungama makosa na dhambi kwa Yesu Mwokozi wa wote.

3. Mwokozi aliniondoa porini, natunzwa shambani mwa Mungu. Na sasa kwa mvua na jua la mbingu ninamzalia matunda.

4. Naona maisha ni yenye maana: Ni ku’tumikia Mwokozi. Kuishi ni Kristo na kufa faida kwa kila mkristo wa kweli.


Video ya sauti




150 NATAKA kupokea baraka yake Mungu

1. Nataka kupokea baraka yake Mungu, nataka kubatizwa kwa Roho ‘takatifu. Ju’ ya ahadi yake napumzika sana, aliahidi mimi kupata Roho yake.

Pambio:
Sawa na bahari, sawa na bahari ni neema yake anileteayo. Anayenijaliza, anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu. Asifiwe sana!

 

2. Kanisa lake Mungu linaipata mvua, vijito vya baraka vinamiminwa sasa. Furaha ya uzima ni kubwa kati yetu. Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!

 

3. Mawimbi ya wokovu yanatujia sasa. E’ Mungu, tunaomba: Ujaze sisi sote! Watakatifu wako watakasike sana! Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!

 

4. Mawimbi ya wokovu yaliyofika kwetu, E’ Mungu, uyatume ulimwenguni mwote, maelfu kati watu wapate kuokoka, waimbe haleluya, wamshukuru Yesu!

H.J. Zelley, 1900
Like a mghty sea




151 MWOKOZI moto safi

151

1. Mwokozi, moto safi, tunataka moto wako juu yetu! Twaomba kwako leo, Mungu: Washa moto ndani yetu, washa moto! Tazama sisi hapa leo, na tupe Roho yako, Mungu! Tupate Pentekoste yetu! Tunangoja moto wako juu yetu!

 

2. E’Mungu wetu usikie, tunaomba moto wako juu yetu! Twadumu katika kuomba: Washa moto ndani yetu, washa moto! Tunahitaji nguvu yako ili tutakasike sana na kuyashinda majaribu. Tunangoja moto wako juu yetu.

 

3. Mioyo iliyo baridi inataka moto wako juu yao. Hitaji zote tutajazwa, tukipata moto wako ndani yetu. Siwezi mimi peke yangu kushinda mambo ya shetani, lakini ninaomba, Mungu: Washa moto ndani yangu, washa moto!

 

4.Naomba moto juu yangu ili nihudumu huku kwa upendo; nauhitaji moto wako, niwe na bidii nyingi na ‘hodari. Ju’ ya madh’bahu takatifu nakuwekea moyo wangu, Mungu, washa moto, washa moto, washa moto!

W. Booth, 1894
Thou Christ, of burning, cleansing flame, R.H. 25




152 YESU alipolala kati’ kaburi

152

1. Yesu alipolala kati’ kaburi, giza ilifunika Yesu Mwokozi.

Pambio:
Alifufuka hakika, akavunja nguvu ya mauti, mshindaji ju’ ya mamlaka yote; ni Mflme wa milele na milele, Alikuwa amekufa, na tazama amefufuka!

 

2. Walinzi wa kaburi walikimbia, muhuri na vifungo vilivunjika.

 

3. Mauti na pingo hazikuweza kumshika Yesu Mwokozi.




153 YESU CHRISTO alifufuka

153

1. Yesu Kristo alifufuka, akatoka kaburini. Furahini na msifuni, kwani alishinda kufa!

Pambio:
Habari njema: Alifufuka katika wafu! Yesu yu hai, naye atakuja tena.

 

2. Nguvu za mauti na dhambi Yesu Kristo alishinda; nasi sote tutashinda kwa nguvu yake ya ajabu.

 

3. Kundi dogo, msiogope, Bwana Yesu ni uzima! Aliziondoa dhambi na anawafariji moyo.

 

4. E’ wakristo, shangilieni, Yesu aliyefufuka yu karibu, atakuja na atatufufua sote!

Eric Bergqvist, 1904




154 E’RAFIKI shaka zako zipeleke kwake Yesu

154

1. E’rafiki, shaka zako zipeleke kwake yesu!
Aliyemwamini yey hataona haya kamwe.

Refrain:
Naamini, naamini, ninakuamini, yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako

2. Dhambi zote ziungame na kwa damu utakaswe,
akuvike haki yake! Atakufikisha kwake.

Refrain:
Naamini, naamini, ninakuamini, yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako

3. Masumbuko yako yote uyaweke mbele yake!
Ukipita uvulini, bwana yesu yupo nawe.

Refrain:
Naamini, naamini, ninakuamini, yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako

4. Na furaha yako pia ijulike kwake yesu,
yeye bwana ju’ ya yote akubarikie yote!

Refrain:
Naamini, naamini, ninakuamini, yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako

5. Ujitoe kwake yesu: roho, mwili na akili vyote vya
maisha yako anataka ku’takasa.

Refrain:
Naamini, naamini, ninakuamini, yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako




155 KATIKA matumaini kwa Mungu wangu nakaa katika raha na utulivu

155

1. Katika matumaini kwa Mungu wangu nakaa katika raha na utulivu. Na yeye ni mwamba wangu, imara sana; katika dhoruba zote ananilinda.

 

2. Mwenyezi ni ngome yangu, sitatetema; siwezi kuhofu tena huzuni, shida. Ikiwa ni vita kali, sitaogopa; ni msaidizi wangu karibu nami.

 

3. Mahali pa kustarehe kwa Yesu Kristo; napata amani, raha, furaha kubwa. Faraja katika shida, gizani nuru, na katika pepo nyingi bandari nzuri.

Jonas Petersen
Allenast i hopp till Gud, Evgt. 1; M.A. 225




156 WALIAMINIO neno lake Mungu watapata nguvu kuwa washindaji

156

1. Waliaminio neno lake Mungu watapata nguvu kuwa washindaji, kwani Bwana Yesu alituahidi atathibitisha neno kwa ishara.

Pambio:
Shinda, shinda, nguvu ya kushinda! Shinda, shinda, shinda kila saa! Mungu atatupa nguvu ya kushinda, Tumtii Yesu nasi tutashinda!

 

2. Kati’ vita kali tuwe na ‘hodari, Mungu ndie nguvu yetu ya ajabu! Tu’amini neno: Na ishara kubwa ziatafuatana na waaminio.

 

3.Nguvu ya kupiga vita ya imani, nguvu ya kupinga hila za shetani! Yesu amesema: Na ishara kubwa zitafuatana na waaminio.

Leila Morris, 1862-1929
Theu who know the Saviour, R. H. 441




157 HAIDURU kwangu uku chini

157

1. Haidhuru kwangu huku chini utajiri au umaskini, ila Bwana Yesu awe nami; ninatunzwa naye siku zote.

 

2. Haidhuru kama ninakuta shida nyingi katika safari, ila Mchungaji wangu mwema anilide na kuniongoza.

 

3. Haidhuru kama tunakaa katika baridi au hari, kwa sababu ukombozi wetu unakaribia. Haleluya!

 

4. Haidhuru kama sitapata utukufu na heshima huku; nikifanywa kama takataka, yanipasa kupendeza Bwana!

 

5. Haidhuru kama njia yangu inanichokesha mara nyingi, basi, nisigombane na ndugu, na pamoja tutashangilia!

 

6.Haidhuru kama tukiona sisi si wakubwa huku chini. Tuwe watumishi wake wema, na tutaingia kwake Bwana!

 

7.Haidhuru kama twasafiri katika dhoruba ya bahari, kwani Yesu ni nahodha wetu, atatufikisha bandarini.

Jonas Andersson




158 HERI mtu anayeamini Mungu baba

 158

1. Heri mtu anayeamini Mungu Baba na Yesu Mwokozi! Heri mtu aifuataye njia nzuri ‘endayo mbinguni!

Pambio:
Usifiwe, Yesu Kristo! U Mwokozi mzuri kabisa! Usifiwe, Yesu Kristo! Bwana, nitakuona mbinguni.

 

2. Kwa furaha tunakusanyika kusikia maneno ya Mungu, na mbinguni karibu ya Yesu tutamshangilia daima.

 

3. Kuamini pasipo kuona inafaa katika safari. Siku moja atatuchukua, tutakaa milele mbinguni.

 

Tune: In the sweet by and by, R.H. 777




159 NASIKIA Bwana Yesu aniita ku’fuata

159

1. Nasikia Bwana Yesu aniita ku’fuata. Aliponitangulia nifuate yeye njia yote!

Pambio:
Nifuate nyayo zake, nifuate nyayo zake, nifuate nyayo zake, nifuate yeye njia yote!

 

2. Nifuate njia yote, na kwa maji nibatizwe, na kujazwa Roho wake! Nifuate Yesu njia yote!

 

3. Nifuate, nihubiri nelo lake la uzima kati’watu wa dunia! Nifuate Yesu njia yote!

 

4. Nifuate Bwana Yesu katika mateso, kufa, na nifufuliwe naye! Nifuate Yesu njia yote!

 

5. Atanipa ne’ma yake kwa kudumu hata mwisho, hata nitakapomwona Bwana Yesu huko ju’ mbinguni.

E.W. Blandley
I can hear my Saviour calling, R.S. 297




160 AHADI zote za Mungu wetu zanasimama hata milele

160

1. Ahadi zote za Mungu wetu zinasimama hata milele. Milima yote ikianguka, ahadi hazipunguki.

Pambio:
Ahadi zake zinasimama, hazipinduki hata milele. Ikiwa nyota zingezimika, ahadi zake zinadumu.

 

2. Ahadi zake zinasimama katika shida, katika giza. Na nikichoka kwa vita kali, ahadi hazipunguki.

 

3. Ahadi zake zinasimama katika homa, katika kufa. Nafarijiwa na Baba yangu, ahadi hazipunguki.

 

4. Ahadi zake zinasimama; nitaamshwa katika kufa. Kwa Baba nitapokea taji; ahadi hazipunguki.

Johan Holmstrand, 1924




161 UMESHIRIKIANA naye Yesu? kama tawi ndani yake mzabibu?

161

1. Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Una raha iliyo timilifu, umejazwa Roho yake ‘takatifu?

Pambio:
Umeshirikiana naye Yesu kama tawi ndani yake mzabibu? Kuna raha na starehe katika kuomba Mungu; akutia nguvu ya kushinda yote.

 

2.Umepata imani ishindayo katika mashaka, shida huku chini? Umepata neema ya kudumu inayokulinda katika hatari?

 

3. Kwake Yesu mahali pa amani, huko ndiko pa kuburudika sana; atujaza mioyo utulivu, tunakaa na raha na starehe. 

 

4. Twafurahi kwa wema wake wote, twamsifu kwa ulinzi wake pia. Hata tukiudhiwa huku chini, atatufikisha kwake huko juu.

F.M. Lehman




162 Bwana Yesu

 162

1. Bwana Yesu, uwe nami, bila wewe nina hofu, unikaribie sana, uwe kiongozi wangu!

Pambio:
Sitaona hofu tena, Yesu Kristo yu karibu. Ninataka kufuata njia yako siko zote.

 

2. Bwana Yesu, uwe nami, kwani mimi ni dhaifu; na unifariji moyo kila siku ya huzuni!

 

3. Bwana Yesu, uwe nami siku zote safarini, zikiwako shida huku au raha na amani!

 

4. Bwana Yesu, uwe nami! Nahitaji nuru yako hata nitafika mbingu, kao letu la milele!

Fanny Crosby, 1884




163 AHADI zote za Mungu zinasimama kweli

163

1. Ahadi zote za Mungu zinasimama kweli, na zilitiwa muhuri kwa damu yake Yesu.

Pambio:
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ‘aminiye ‘taona: Ahadi zinadumu.

 

2. Fanya kama Ibrahimu: Uangalie juu! Nyota ukizihesabu, imani itaota.

 

3. Katika giza njiani tutaamini tu. Muda kitambo, na tena jua litaangaa.

 

4. Watu wakitusumbua, tutaamini tu. Yesu atusaidia majaribuni pote

 

5. Rafiki wakituacha, tutaamini tu. Yesu, rafiki mkubwa, atabaki daima.

 

6. Katika mambo yo yote tutaamini tu. Tutaviona mbinguni tulivyoviamini.

Lewi Pethrus, 1913