1. IKIWA wananiuliza msingi wa uzima je? twahitaji kuongeza kwa kazi yake Yesu? Kwa uhodari nitajibu: msingi wangu ni wa nguvu, ni damu yake Yesu Kristo inatosha sana.
2 UMWAMBA wa zamani sana, Daima utadumu. Na hata siku nita’kufa, nitautegemeya. Nitakapoondoka huku, nitaimbia majeraha na damu ya mwokozi wangu, Funguo la mbingu.
1. Haifai kuyasumbukia mambo yatakayokuwa kesho. Baba yangu anajua yote, ni vizuri nikumbuke hivyo. Yeye mwenye moyo wa upendo ananipa yafaayo kweli, kama sikitiko au shangwe, na amani yake kila siku.
2. Siku zote yu karibu nami, na neema anapima sawa. Achukuwa masumbuko yote, yeye aitwaye Mungu Baba. Kunitunza hivyo kila siku, mambo hayo ame’tadariki. Kama siku, kadhalika nguvu! Ni ahadi niliyoipewa.
3. Mungu, unisaidie tena ‘kaa kimya kwako siku zote! Niamini sana neno lalo, ‘sipoteze bure nguvu yako! Nakatika mambo yote huku nipokee kwa mikono yako nguvu na neema yakutosha, hata nitakapofika kwako!
1. Pendo la mungu ni kubwa, pasha habari hiyo! pendo la Mungu ni kubwa, mwanzo wa nyimbo zote. malaika waliimba wachunga wakasikia. tunafurahi kujua pendo la mungu ni kubwa.
refrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
2. Pendo la mungu ni kubwa kwako uliye mbali. pendo la Mungu ni kubwa, anakuhurumia. ukiendee kisima kinachotoka golgotha, utaupata uzima katika pendo la mungu.
Refrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la mungu ni kubwa!
3. Pendo la mungu ni kubwa, latufikisha mbingu, pendo la Mungu ni kubwa, tutafurahi sana! huko hakuna jaribu wala ugonjwa na kufa. tumeokoka sababu pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
4. Pendo la mungu ni kubwa, pasha habari hiyo! pendo la Mungu ni kubwa, mwanzo wa nyimbo zote. malaika waliimba wachunga wakasikia. tunafurahi kujua pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
5. Pendo la mungu ni kubwa kwako uliye mbali. pendo la Mungu ni kubwa, anakuhurumia. ukiendee kisima kinachotoka golgotha, utaupata uzima katika pendo la mungu.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
6. Pendo la mungu ni kubwa, latufikisha mbingu, pendo la mungu ni kubwa, tutafurahi sana! huko hakuna jaribu wala ugonjwa na kufa. tumeokoka sababu pendo la mungu ni kubwa.
Pefrain: Pendo kuu, pendo kuu, pendo kuu pendo la Mungu ni kubwa!
1. Mimi mkristo nita’vyokuwa katika yote mpaka kufa. Mimi mkristo, ‘navyoshuhudu, dunia yote ikinicheka. Mimi mkristo kwa moyo wote sababu ninampenda Kristo, aliyekufa kwa ‘jili yangu. Anastahili kupendwa nami.
2. Mimi mkristo, neema kubwa! Niliokoka kutoka dhambi. Mimi mkristo, hata ikiwa katika shida na mapigano. Mimi mkristo, na ni askari, nafanya vita kushinda dhambi. Akida wangu ni Bwana Yesu, pamoja naye ‘tashinda yote.
3. Mimi mkristo, na ni mgeni, nimeifunga safari yangu; na sitamani yaliyo huku, ninatafuta yaliyo juu. Mimi mkristo na nchi yangu ni huku juu katika mbingu, hamna njaa na shida humo. Wakristo wote washiba mno
4. Mimi mkristo! Ni neno zuri la kufariji moyoni mwangu linanitwaa ju’ ya huzuni, nipumzike kwa Mungu wangu; Mkristo katika kila hali, na nikiitwa na kufa tena, kwa raha kubwa nitakubali kuchukuliwa mbinguni juu.
1. Israeli wake Mungu, kimya sana, wa’zunguka Yeriko kwa imani. Malaika wake aliwaongoza, na waliendelea kwa kushinda.
Pambio: Twende kwa kushinda, twende kwa kushinda! Kwa damu yake Yesu, twende kwa kushinda! Tegemea Mungu, anatuongoza, na kwa imani, twende kwa kushinda!
2. Na Daudi, mchungaji, alikwenda mbele yake Goliathi bila woga; kwa imani alitupa jiwe lake, kwa jina lake Mungu akashinda.
3. Danieli aliomba kila siku, hakuhofu pango la simba kamwe; katika imani aliomba Mungu, akaokoka katika hatari.
4. Hata safarini huku kwenda mbingu nikipita katika jangwa kavu, na kupatwa na ‘jaribu mbalimbali, najua kwa imani nitashinda.
5. Na imani inashinda hali zote, inaruka juu ya mambo yote. Niliye dhaifu sitahofu kamwe, kwa kuwa Mungu ananiokoa.
1. Askari wa imani sisi, kwa shangwe tunaendelea, hata vita ‘kiwa kali tuna nguvu na ‘hodari. Tuna upanga wa imani, ni neno lake Mungu wetu; na kwa jina lake Yesu tunashangilia sasa.
Pambio: Mbio tutaacha huku, vita ikiisha. Tutaingiamo mbingu ku starehe humo. Wao washindao huku, watapewa taji kwa mkono wa Mwokozi, anayewapenda.
2. Tuvae kila mtu sasa silaha zote zake Mungu. Na mishale ya shetani ‘tazimika mbele yetu. Tukimtii Bwana Yesu, twaendelea kwa ‘hodari, na kwa nguvu za ahadi tutakuwa washindaji.
3.Na ukipungukiwa nguvu, katika vita ukishindwa, Yesu atakutilia nguvu mpya ya kushinda. Kwa nyimbo za kushangilia, utahimili shida zote, na kupata kuokoa wenye dhambi na makosa.