181 TUTAZAME kule mbele

181

1. Tutazame kule mbele, asubuhi inakuja! Tuamini Mungu wetu, atafanya kazi yake, kufukuza mashetani, kumiliki nchi yote. Tutashinda tukiomba, Mungu anatusikia.

 

2. Tarumbeta linalia, tuamke wote sasa! Mungu wetu anataka sisi sote tutakaswe! Kila mtu awe safi katika kanisa lake! Uliache nung’uniko, utapata nguvu yake!

 

3. Imba ninyi, watu wake, Bwana yu pamoja nasi! Tutashinda majaribu kwa uwezo wake Yesu. Twende tumhudumie kwa kumpa mali yake; hata roho na akili zimtumikie Bwana!

 

4. Watu wengi hawajui njia yakufika mbingu, wanakuwa wamefungwa kwa mikono ya shetani. Twende tukawatafute, tuwavute kwa Mwokozi, na kuomba na kukesha hata kuja kwake Yesu!




193 NINENO zuri la ‘aminiwa

193

1. Ni neno zuri la ‘aminiwa, listahililo kukubaliwa, ya kwamba Yesu alitujia awaokoe wenye makosa.

 

2. Wa kwanza mimi wa wenye dhambi, lakini ninafurahi sasa sababu Yesu, Mwokozi wangu, aliniosha kwa damu yake.

 

3. Mwokozi wetu yu nasi hapa, atenda kazi kwa nia yake; awasha moto rohoni mwetu, uwezo gani utampinga?

 

4. Viziwi wanasikia sasa, viwete wanatembea sawa, wenye ukoma watakasika, Injili yake yahubiriwa.

 

5. E’ Bwana Yesu, tupulizie, tujaze Roho Mtakatifu! Uwaamshe waliokufa katika dhambi, uwaangaze!

 

6. Fungua mbingu unyeshe mvua panapo kiu na jangwa tupu! Uligeuze, likachanue na kufurahi kwa shangwe kuu!

 

7. Na mataifa wakusujudu mahali pako patakatifu! Amina. Wako ni utukufu na sifa zote! Haleluya!

Joel Blomkvist, 1876




237 MWOKOZI wangu ni mwamba bora

237

1. Mwokozi wangu ni mwamba bora, ahadi kama milima; zaniletea amani tele, na mibaraka daima. Katika mwamba ni raha kuu, baraka tele kutoka juu. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

2. Makimbilio ni mwamba huo katika teso lo lote; Nisikimbie adui ‘kuu, nishinde katika vyote! Dunia yote ikitingika, ahadi zake hazipunguki. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

3. Nakaa mbali ya udhalimu, hatia, dhambi, hukumu. Na kwa imani nikisimama, adui atakimbia. Nayo mawazo ya giza tupu hayatapata nafasi huko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

 

4. Nafurahia baraka zote za ulimwengu wa roho. Karama hizo nalizipewa katika kufa kwa Yesu. Hakuna woga na shaka huko, hayatakuwa manung’uniko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

Otto Witt




245 MIKWAJU itiapo giza na kivuli

245

1. Mikwaju itiapo giza na kivuli katika nchi ya Bersheba ya zamani, alitembea Ibrahimu asubuhi, na maumivu na huzuni ni rohoni, kwa kuwa aliitwa na Mwenyezi Mungu kutii amri yake bila nung’uniko. Na hapo akaomboleza: “E’ Bwanangu, wataka nitakutolea mwana wangu?”

 

2. Sauti ya Bwanake aliifaamu: “Mtwae sasa mwana wako wa pekee, ukamtoe mwana juu ya madh’bahu; kafara ya thamani ukanitolee!” Na moyo wake ukamtulia sana, akitukuza Mungu akitumaini yakuwa yeye atamfufua mwana; alimjuwa yeye aliye mwamini.

 

3. Akaamka Ibrahimu alfajiri, akatandika punda, akatwaa kuni. Pamoja na mwanawe tena ‘kasafiri, na roho yake ikalia kwa huzuni. Mwanawe Isak’ aliyemfurahia: kipeo cha furaha ya uzee wake, matumaini yake yote ya dunia, kafara atakayotoa kwa Bwanake.

 

4. Katika njia ya mlima wa Moriya mtoto akamsaili baba yake: “Tazama moto uko, kuni ziko pia, kondoo mume kwa kafara yuko wapi?” Na Ibrahimu akajibu kwa imani isiyoona shaka wala kudhania: ” Kondoo mume kwa kafara ya shukrani, ninasadiki Mungu atajipatia.”

 

5.Je awezaje Ibrahimu kusahau wakati huo wa uchungu na huzuni, na jinsi akajenga huko madhabahu, na tena akamweka mwana ju’ ya kuni? Akakitwaa kisu amchinje mwana, halafu aliposikia neno tamu:”Usifanyie neno sasa kwa kijana, najua wanipenda sana Ibrahimu!”

 

6. Akainua macho yake kwa haraka, tazama dume la kondoo, nyuma yake, aliyenaswa pembe zake kwa kichaka! Akamtoa akomboe mwana wake. Na malaika akamwita akasema:”Umenitii nami nitakubariki. Na kwa uzao wako mataifa tena wa’barikiwa kwani umenisadiki”.

 

7. Machozi yamekuwa mengi tangu hapo; wakristo wamekamilika kwa jaribu. Na mlimani mwa Moriya wazikapo matumaini yao, pendo na nasibu. Lakini juu ya mlima wa kafara Mwenyezi Mungu abariki watu wake. Awajulisha nguvu zake na ishara, awajaliza Roho ya ahadi yake.

Otto Witt 




248 YESU akiniongoza sitaanguka

248

1. Yesu akiniongoza sitaanguka, sitaanguka. Ni Mfalme mtukufu, Mwokozi wangu, Mwokozi wangu.

Pambio
Wakati huu, hata milele apita vyote vya dunia. Yesu amenichagua, Mwokozi wangu, Mwokozi wangu.

 

2. Yesu amenipa raha, ni kiongozi, ni kiongozi. Anaka’ moyoni mwangu, Yesu Mwokozi, Yesu Mwokozi.

 

3. Nilikuwa kama chungu kilichovunjwa, kilichovujwa. Sasa nimeokolewa na Bwana Yesu, na Bwana Yesu.

 

 4. Nitakapofika mbingu nitamsifu, nitamsifu Yesu kwa upendo wake, Mwokozi wangu, Mwokozi wangu.




271 UWATAFUTE wenzako wapoteao mbali

271

1. Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Yesu mwenyewe apenda kuwaokoa wote.

Pambio
Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Pasha habari ya Yesu na ya wokovu wake!

 

2.Uwatafute wenzako kwa neno la upendo! Mungu atalibariki na kulithibitisha.

 

3.Uwatafute wenzako kwa’jili ya Mwokozi! Aliwakomboa wote, ni mali yake kweli.

 

4.Uwatafute wenzako kabla ajapo Yesu! Wasipotee kabisa, uwaokoe mbio!

Fred P. Morris




273. NI uheri kumwamini Mungu

273

1. Ni uheri kumwamini Mungu kama Ibrahimu wa zamani. Hakutiwa shaka kwa uchungu, ila alitii kwa imani. Ni uheri kuendea sawa katika mapito ya sheria. Ukijaribiwa na kukawa, mwisho Mungu atakujalia.

 

2. Mashujaa wote wa Biblia hawakufurahia anasa. Wakafunzwa kutumainia Mungu na uweza wake hasa. Tena wakaenda kwa imani ya kutetemesha ulimwengu, wakashinda giza na shetani. Sifa na heshima zina Mungu!

 

3. Yesu atakaye kuzwa naye kwanza adhiliwe kuwa vumbi; Mwana wake mwema na ambaye baba humpenda, humrudi. Hivyo Mungu awakamilisha watu wake kwa mateso huku, na zaidi kuwafahamisha kulijua pendo lake kuu.

 

4.Na ikiwa raha ya dunia yatoweka katika jaribu, mwaminifu atafurahia Mungu wake, kwani yu karibu. Na mavuno ya taabu yake yakichomwa na kuharibika, atategemea Bwana wake na kwa hiyo hata nung’unika.

 

5.Jipe moyo, enyi kundi dogo, na msiogope hatarini! Shika neno la Mwenyezi Mungu, litawaongoza safarini! Haleluya, kwani majaribu yahimiza msafiri mwendo, hata ataona kwa karibu mji wa amani na upendo!

Emil Gustavsson, 1889




276. MATENDO ya Mungu yapita fahamu

276

1.  Matendo ya Mungu yapita ‘fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.

 

2.Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?

 

3. E’ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama mbinguni!

 

4.Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ‘takwisha, milele nitashangilia.

 

5. Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye neema katika shauri na tendo.

 

6.Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao mbinguni.

 

Emil Gustavsson, 1886

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Livecgf5aQA?feature=oembed&w=500&h=281]




277. NITAOGOPA nini gizani duniani

277

1. Nitaogopa nini gizani duniani? Sikuachiwa peke’ mbali ya tumaini! Mwokozi yu karibu, asiyebadilika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Pambio:
Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.

 

2. “E’ usifadhaike moyoni mwako, mwana”, anong’oneza Yesu, “Nitegemee sana!” Na hapo woga wangu waruka kwa hakika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

 

3.Na nikijaribiwa na jua lifichwapo, hata sioni raha, wala faraja hapo, nakimbilia Yesu, na yote yapinduka.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Mrs. C.D. Martin




282 UKIONA kiu sana ujalivu

 282

1. Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi, roho yake safi pia, liamini neno la babako na atakujazi, nawe utashangilia.

Pambio:
Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: “Njoo bila ‘sitasita!” Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

 

2. Vichukue vyombo vyako, uvioshe safi sana kisimani pa Golgotha! Afadhali kujitoa lote kwa Mungu Bwana, na imani itaota.

 

3.Na mafuta ya neema hayakomi. Asifiwe! Tunakuwa na shukrani! Anataka kumimina Roho ya ahadi yake. Mpokee kwa imani!

Leila Morris, 1922
Are you looking for the fulness, R.H. 214