1. E’ mlinzi, twauliza: Yesu atakuja lini? Asubuhi ya sayuni ni karibu? Tuambie! Msafiri, yainue macho yako, angalia! Asubuhi ni karibu, usimame, usimame!
2. Siku heri ya sabato ya milele ni karibu, na dalili yake Yesu hapo itaonekana. Na rohoni tunaona nchi nzuri ya ahadi. Asubuhi ni karibu, na ahadi zatimia.
3. Katika Yerusalemu, mji mpya wa mbinguni, Yesu atatumiliki kwa upendo na amani. Baragumu italia, nasi tutaisikia. Yesu ni karibu sana kutukaribisha kwake.
1. Baragumu litalia sana, watu wote watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika. :/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:
2. Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua. :/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:
3. Najua Mchunga wangu mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa. :/:Nani Mchunga mwema? Yesu, mweza yote. :/:
4. Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja. :/: Nani atahukumu? Yesu, mweza yote. :/:
5. Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi. :/: Nani ni mzabibu? Yesu, mweza yote. :/:
7. Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli. :/: Nani mwenye upendo? Yesu, mweza yote. :/:
8. Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu. :/: Tumshukuru nani? Yesu mweza yote. :/: