170 NIKIONA shida huku katika safari

170

1. Nikiona shida huku katika safari, Yesu aninong’oneza neno la faraja. Ananipa raha tele na furaha ya ajabu. Ninaandamana naye sasa na milele.

 

2. Tena njia ikienda juu ya milima, ninakaribia mbingu, nuru inaang’aa. Na katika nuru hii ninaona kwa uwazi nchi ya ahadi yake na urithi wangu.

 

3. Kwa imani ninaimba, hata hatarini, njia ‘kiwa ndefu huku, nitavumilia. Nyota za ahadi zake zinang’aa kwa usiku, zinaniongoza vema hata huko juu.

 

4. Kama Musa aliona nchi ya ahadi, kadhalika natazama nchi yangu juu; ninaisalimu sasa hwa uheri na imani. Natamani kufikako, kwa urithi wangu.

 

5. Vya hatari vikifika kati’ njia tena, Yesu yu pamoja nami, anichunga vema. Ninaendelea mbele, na mbinguni nifikapo nyimbo nzuri nitaimba na wakristo wote.

Werner Skibsted, Paul Ongman, 1930




173 MAISHA katika dunia

173

1. Maisha katika dunia ni kama kupanda na ‘vuna: Apandaye katika mwili atavuna uharibifu; tukitumikia Mwokozi tutapata thawabu mbinguni; yafaa kuishi na kufa katika maneno ya Mungu.

 

2. Kwa neema kubwa kabisa tumekubaliwa na Mungu, kwa neema kubwa zaidi twapata kumtumikia. Kuishi kwa ‘jili ya Yesu kati’ yote ya dunia hii na kuitangaza injili ni faida kwetu kabisa.

 

3. Wakristo wata’poingia mbinguni kusifu Mwokozi, na mimi nataka kufika kuimba pamoja na wao. Tutamshukuru Mwokozi aliyetununua kwa damu; waliohudumu kwa pendo watamhimidi milele!

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=clHjbEJYgQM?feature=oembed&w=500&h=281]




190 KISIMA cha lehi kingali

190

1. Kisima cha Lehi kingali kwa kila aliye na kiu. Kinatoa maji mazima yaliyo ya kuburudisha.

Pambio:
Kisima chema cha maji safi hakikauki hata milele. Ni heri yangu, napumzika, na roho yangu inatulia.

 

2.Ulie na kiu rohoni, ukinyong’onyea njiani, tazama kisima jangwani kilicho na afya, uzima!

 

3. Mtungi ukiwa mtupu, ukipungukiwa imani, ufike kisima cha maji yabubujikayo daima!

 

4.Na penye kisima cha lehi upange na kupumzika! Uketi kivulini mwake, na moyo utaburudishwa!

Ida Björkman M et T




191 YAPIGWA hodi kwangu

191

1. Yapigwa hodi kwangu, mgeni a’fika, akiniomba: “Nifungulie! Umande umeshuka kichwani usiku, na nywele zangu zimelowa maji”.

 

2. A! Huyu si mgeni, ni Yesu Mwokozi, sauti yake nzuri na’jua. Ninamfungulia, naona ni Yesu; na siku hiyo sitaisahau.

 

3. Anong’oneza sasa rohoni: “U wangu”, karibu naye ninatulia. Ananitia nguvu, baraka ya mbingu; daima nitakaa kwake Yesu.

 

4. Ni kweli, mimi ni wa Mwokozi milele, amenitaja: “Ndugu, mpenzi”. Ananikarimia hazina za mbingu, ninaingoja siku ya arusi.

Fr. Schibboleth. arr L.P




239 NENO mbaya lisitoke kamwe kwa ulimi wako

239

1. Neno baya lisitoke kamwe kwa ulimi wako! Pendo likuchunge pote, hata na maneno yako!

Pambio:
Amri ya Yesu ni “Mpendane”! Kama watoto wema tumtii! Amri ya Yesu ni “Mpendane”! Kama watoto tumtii!

 

2. Pendo ni la mbingu, safi, urafiki ‘takatifu. Tusiyaharibu tena kwa maneno yetu ‘gumu!

 

3. Neno moja la hasira au tendo la uovu, kwa upesi linavunja fungu la upendo safi.

T. Truvé




241 SITASHAWISHIWA tena na dunia huku

 241

1. Sitashawishiwa tena na dunia huku, mema yote ni kwa Yesu, nampenda yeye. Katika safari yangu, Bwana Yesu wimbo wangu. Mbali, kwetu, kila saa namsifu Yesu.

 

2. Mimi mtu heri sana, nampenda Yesu. Vyote nimempa yeye, namtumikia. Tumaini langu kuu nimeweka huko juu. Mbali, kwetu, kila saa namtumikia.

 

3. Njia yote kwenda mbingu nifuate Yesu! Nifanane naye Bwana, niwe nuru huku! Namkiri Yesu pote na katika hali zote! Mbali, kwetu, kila saa nifanane naye!

James Rowe/ Paul Ongman




242 MAISHA yangu yote nimali ya Mwokozi

242

1. Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Maungo, roho na akili, yeye ameyabadili. Siku zangu zote ni mali ya Mwokozi.

Pambio
Wakati wangu wote ni mali ya Mwokozi. Machoni pake ni amani, natumika kwa shukrani. Namsifu Yesu, amenihurumia!

 

2. Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Naomba niwe mpendevu, nitafute wapotevu! Aliwanunua kwa damu takatifu.

 

3. Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Unijalie kati’ mwendo kuongoza kwa upendo wana wapotevu, wapate kuokoka.

 

4. Maisha yangu yote ni mali ya Mwokozi. Nakaa miguuni pake, siku moja huko kwake inapita elfu pengine bila Yesu!

W.C. Martin




243 UKICHOKA kwa safari ngumu

243

1. Ukichoka kwa safari ngumu, sema na Yesu, sema na Yesu! Waogopa kwamba hutadumu, sema na Yesu daima!

Pambio
Sema na Yesu, sema na Yesu, yeye rafiki amini! Akupenda kwa upendo bora. Sema na Yesu kwa yakini!

 

2.Ukilia chozi ya majuto, sema na Yesu, sema na Yesu! Ukiteswa ju’ ya dhambi nzito, sema na Yesu daima!

 

3.Je, wahofu jua likifichwa? Sema na Yesu, sema na Yesu! Kwa taabu ukihuzunishwa, sema na Yesu daima!

 

4.Ukisumbukia kufa kwako, sema na Yesu, sema na Yesu! Ukiteswa kwa maisha yako, sema na Yesu daima! E.S.

Lorenz
Tell it to Jesus, R.S. 592 




262. KITAMBO bado – vita itaisha

262

1. Kitambo bado-vita itaisha, kitambo, na dhoruba zitapoa. Na tena nitalaza kichwa changu mbavuni mwake anayenipenda.
:/: Nitaziona raha na amani, mbinguni hazitakuwapo dhambi. :/:

 

2. Kitambo bado- roho yaumizwa, kitambo katika usiku huku. Machozi nina’toka mara nyingi sababu sijaona bado Yesu.
:/: Lakini asubuhi ya milele huko mbinguni sitalia tena. :/:

 

3. Kitambo bado ya kuchoka huku, kitambo, tena nitaona Yesu. Na huru mbali na hatari zote nitastarehe mikononi mwake.
:/: Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli. :/:

 

4. Mateso yangu hayadhuru tena, nitasahau yote kwa Yesu. Nikisumbuka mda duniani, mbinguni sitaona shida, kufa.
:/: Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote. :/:




263. ENYI kundi lake Mungu

263

1. Enyi kundi lake Mungu, muda haba mhimili! Kati’ nchi ya milele mtaona raha tele.
:/: Muda haba, muda haba, tena vita itakwisha. :/:

 

2.Usilogwe na dunia, usiache Mungu wako! Katika mabaya, mema ufuate Bwana Yesu.
:/: Siku zote, siku zote! Hivyo utashinda vyote. :/:

 

3.Ukichoka safarini, ukiona njia ndefu na hatari za jangwani, Mungu akuburudisha.
:/: Raha huko, raha huko yatuliza msafiri. :/:

 

4. Kwa imani tunaona nchi yetu ya ahadi. Ni habari nzuri sana: Majaribu yatakoma.
:/: Mbio sana, mbio sana huko ju’ tutaonana. :/:

 

5. Tukiitwa na mauti kwa furaha tutahama. Tulivyovitumaini, ng’ambo huko tutaona.
:/: Heri tele, heri tele: ‘ona raha ya milele! :/:




265. TU wasafiri

265

1. Tu wasafiri, twakaribia nchi ya mbingu kwa Mungu baba. Tusiogope bonde la kufa, Yesu atuongoza kwake!

Pambio:
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote mbinguni!

 

2. Wengi katika wapendwa wetu wamevuka mto wa kufa. Walifuata mwito wa Mungu. Wakahamia nchi nzuri.

 

3. Katika mwendo wa duniani walitazama Mwokozi wao, na waliacha mambo ya huku, walipendeza Bwana Yesu.

 

4. Ndugu wapendwa, tuendelee, hata ikiwa shida njiani! Yesu ni njia, kweli, uzima; tumfuate siku zote! Paul Ongman




266. AYALA naye anayo shauku

 266

1. Ayala naye anayo shauku ya maji ya kisima; na vivyo hivyo ninaona kiu kwa Mungu wa uzima.

Pambio:
Kama ayala aonavyo shauku mito ya maji safi, na vivyo hivyo rohoni mwangu naona kiu kwa Mungu wangu.

 

2. E’ Mungu wangu, Mungu wa fadhili, nakutafuta wewe! Je, nikuone lini kwa ‘kamili, niburudishwe nawe!

 

3. Nazifikiri siku za zamani niliposhangilia. Nijaze tena raha na amani, nakutumainia!

 

4. Na usifadhaike moyo wangu, amini Mungu wako! Fadhili zake hata huko mbingu zatosha sana kwako!

H.E. Lute




274. NINAFURAHIYA kisima daima

274

1. Ninafurahia kisima daima, kisima cha damu ya Yesu. Katika upendo nalindwa salama, nasifu Mwokozi mpendwa.

Pambio
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.

 

2. Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi kwa maji ya ‘hai. Yananilietea kupita kipimo uzima na shangwe rohoni.

 

3. Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi katika uheri. Ufike upesi ulie na kiu, kisima kinabubujika!

 

4. Nakaa karibu ya kisima hiki, naona furaha na raha. Nakando ya maji nafasi kwa wote, waweza kupona kabisa.

Emil Gustavsson, 1892




275 E’MUNGU mwenye haki

275

1. E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku katika mambo yote yanayokupendeza! Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka yananitia tetemeko mpaka kufa.

 

2. Ni heri siku zote kutegemea Yesu na kuenenda sawa katika nyayo zake, kwa kuwa yeye ni Mchunga anayeniongoza vema, nipate kuingia katika raha yake.

 

3. Safari yangu sasa yaelekea mbingu, Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha kuona yeye aliyeninunua kwake.

 

4. Ulimwenguni humu, matata na kuchoka. Nikihitaji kitu nafadhahika bure, lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi, natumaini sitakosa dhawabu yangu!

 

5. Mbinguni sitaona adui zangu tena. Hayatakuwa mambo yakupokonya pale. Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya! Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu!


Video imeimbiwa na METHUSELA Bushambale na DAVID IMANI

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=IyxLpC7tyaw?feature=oembed&w=500&h=281]

THAMBI




289. NINATAMANI kwenda mbingu

289

1. Ninatamani kwenda mbingu nchi yangu niliyopewa na Mungu kwa imani. Ni shangwe bora kuona mji ule; kwa kwenda kule sitaogopa kitu.

Pambio:
E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ‘takatifu!

 

2. E’ Mungu, tumepata Mwana Yesu Kristo, kipawa kweli kinachoshinda yote. Anahubiri amani kwao wote walio huku karibu, nao mbali.

 

3. Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si wapitaji na tena si wageni, tunatumika kwa roho ya upendo.

 

4. Amani kwetu na matumaini tele, salamu toka kwa Mungu wa milele ni posho ya watumishi wa upendo; tunaurithi uzima wa milele.

THAMBI Aae