320 Mungu aliacha sisi watu wake walimaji kwa dunia

1. Mungu aliacha sisi watu wake walimaji kwa dunia, aliweka mbegu kwa mikono yetu tuzipande katika watu.

Pambio:
Kazi yetu yote itapimwa, mwenye shamba ni Yesu Kristo. Tusishinde huko na mikono bure katika mavuno ya Mungu.

 

2. Hata roho za watu ni ngumu sana usingoje kupanda; tutavuna mavuno kwa furaha tena tutumikie Yesu daima.

 

3. Siku za ujira zinakaribia. Tutapata hukumu, wenye kazi njema watapata sifa; haya itashika wavivu.

Missionnary, 1958




321 Mwokozi mzuri ni Yesu Kristo, ninamshukuru sana

1. Mwokozi mzuri ni Yesu Kristo, ninamshukuru sana. Alinitafuta kwa njia mbaya, ni mali ya Yesu Mwana.

Pambio:
Kwa damu nafunguliwa, kwa damu nafunguliwa. Alitoa yote kwa mimi na wote, kwa damu nafunguliwa.

 

2. Alibeba dhambi msalabani, alitukomboa sote. Barua za deni na mashitaki, alizipasua zote.

 

3. Ni heri kujua makimbilio, wakati wamajaribu. Nashinda kwa nguvu ya damu yake, asanti Mtakatifu.

 

4. Aliteswa sana kwa Getsemane, uchungu aliunywesha. Lakini kwa mwisho msalabani, alisema imekwisha.

Missionnary




322 Nashika njia ya kwenda mbingu

1. Nashika njia ya kwenda mbingu, mimi msafiri duniani, naishi kwa taabu na mateso mengi. Bali nakaza mwendo nifike mbingu.

 

2. Ijapo shida zanizunguuka, mimi msafiri njia, nashika njia nifike mbingu; nitarithi pamoja na Yesu, nitarithi pamoja na Yesu. :/:

 

3. Wenzangu wote wananigombeza na marafiki wananicheka. Nasumbuliwa hata na wanangu, natazama Yesu rafiki Mwema.

 

4. Ninachofanya maishani mwangu, nimpendeze Mungu aliye Mwema. Nijapoteswa, ninatumaini kuingia mbingu, ni nchi ya raha.

 

MUSAFIRI Chidunga Chigangu, 1993

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=t-eACujIe7U?feature=oembed&w=500&h=281]




329 Ewe Mwana wa Mungu, niokoe nami

1. Ewe Mwana wa Mungu, niokoe nami, nikutumikie na niende Sayuni. (2x)

Pambio:
:/: Sifa zina wewe, Sifa zina wewe, Sifa zina wewe, Milele na milele.:/:

 

2. Mavuno ni mengi, watenda kazi ‘chache. Ita wengi Bwana, waingie kazini. (2x)

 

3. Tuombe kwa bidii Bwana wa mavuno, atume watumishi kati shamba lake. (2x)

 

4. Bwana Yesu yu aja, na ujira wake, kulipa watumishi kama kazi zao. (2x)

WATONGOKA Mulonge Erasto, 1964

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=IZbVs56tJFo?feature=oembed&w=500&h=281]




330 Yesu alipoenda alituachia kazi

1. Yesu alipoenda alituachia kazi, na sasa tuifanye, kwani wakati wapita.

Pambio:
Uyainue macho, uyainue macho! Uyainue macho, uyatazame mavuno!

 

2. Usisimame bure, taifa wapotea usiku, wakabili, hakuna atendaye.

 

3. Aliyekwisha ‘lima, atazamapo nyuma hafai utumishi na ufalme wa Mungu.

 

4.Utapokea nini, ‘subuhi ya milele, watakapopata taji watumishi wa’minifu?

WATONGOKA Mulonge Erasto, 1969

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=QUH_Nh9-yaE?feature=oembed&w=500&h=375]




331 Anayeshuhudia kwamba tutafika

1. Anayeshuhudia kwamba tutafika mbingu ni Roho wake Mungu, anayeweka tumaini la kufika mbingu ni Roho wake Mungu. :/: Tumwombe, tumtafute, Ni wetu Yesu alisema :/:

 

2. Roho yule anafanya njia kati vita kali, kuwaendea ndugu, apungungapo mara tunaanza kuogopa na kujihurumia.

 

3.Upendo wako, ndugu uanzapo, kupunguka, ujuwe Roho yule amekwisha kukuacha, pengine mwili wako unaanza kukusonga, tunaye msaidizi.

 

4. Tunakuomba, Bwana Yesu, umtume kwetu, msaidizi huyo wa maisha yetu huku. Tunaingia sasa kati vita duniani, wandugu tumuombe Mungu.

MUBIKWA Onesimo, 1964




332 Sawa na wapitaji wa dunia

1. Sawa na wapitaji wa dunia. Tunapita huzuni na shida. Siku moja tutaongozwa naye, hata huko mbinguni kwa Baba.

Pambio:
Sawa nyota za mbingu tutang’aa, kwa Yesu Mwokozi mbinguni. Tuishike safari kwa nguvu, na kusifu Mwokozi kwa nyimbo.

 

2. Hatushinde katika dunia, kwa kupewa dhahabu na fedha, ila tunatazama shabaha, ni mjini mbinguni kwa Baba.

 

3. Tukikaa nyumbani wala hema. Tangu utoto hata mauti. Tuna ahadi, kuongozwa naye, kwamba tutafikishwa kwa Baba.

MUBIKWA Onesimo, 1963




333 Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita

1. Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita. Mara nyingi twapata shida, kwani miaka yapita. Tukimwamini Yesu na kumtumikia, tutapata thawabu, kwani miaka yapita.

Pambio:
Yapita, yapita, yapita, yapita, tumikieni Mwokozi, kwani miaka yapita.

 

2. Hatutaogopa kitu, kwani miaka yapita. Bali tutafurahi tu, kwani miaka yapita. Dunia ni shida, mashaka na huzuni. Bali tukaze mwendo, kwani miaka yapita.

 

3. Rafiki wanatuacha, kwani miaka yapita. Na safari itaisha, kwani miaka yapita. Tupande mbegu njema, rohoni mwa wenzetu, wengine waokoke, kwani miaka yapita.

 

MUBIKWA Onesimo, 1963




334 Majira yatuonyesha kwamba

1. Majira yatuonyesha kwamba Yesu yu karibu, ahadi sasa zatimia; tujitayarishe mioyoni.

Pambio:
:/: Tujiandae sasa, na tujiweka tayari. :/:

 

2.Dunia yameremeta na kuvuta macho ya wengi, hayo yote yaonyesha kweli, ni ishara za mwisho.

 

3. Tukeshe kati maombi, tutaumaliza mwendo. Yesu ndiye nuru kushinda, tumtegemee yeye.

 

WATONGOKA Mulonge Erasto, 1968




335 Nitafanya nini mimi, siwezi kitu?

1. :/: Nitafanya nini mimi, siwezi kitu?:/: Siwezi kujiokoa, siwezi kujisafisha, siwezi kujigeuza, siwezi kujirefusha, siwezi kujifupisha, na sitajisaidia. Naomba kwake Yesu, anitengeze (sic).

 

2. :/: Nitafanya nini mimi, sijui mtu?: /: Sijui mawazo yake, sifahamu nguvu zake, sijui upendo wake, sijui imani yake, sijui uzuri wake, wala udhaifu wake. Nitaomba kwake Yesu, mwenye hekima, anifahamishe mtu aliyeumba.

 

3. :/: Nitafanya nini na huu mwili wangu? :/: Nasikia, sifahamu, natazama na sioni, naitika na sifanyi, ninatumwa na siendi, na mwili una matata, wachokoza roho yangu. Nitaomba Roho msaidizi wetu. Nitapewa nguvu kwa jina lake Yesu.

 

4. :/: Nitafanya nini mimi niseme vema?:/: Sijui kusema sawa, maneno yaniponyoka, nayo yanachanganyika, mabaya hata mazuri, yote yatoka pamoja, siwezi kuyarudisha. Ninaomba kwake Mungu anisamehe. Nikaseme kila lugha mpya vizuri.

 

5. :/: Roha inapenda kutumikia Yesu? :/: Ni mwili unakataa, unanizuia sana, badala ya kuhubiri, naenda kwa shamba langu, au kwa byashara yangu. Ninapotaka kuomba uvivu unanijaa, kama nataka kuimba watu huja na maneno. Mungu utanisamehe hayo makosa, yananifikia lakini siyapendi.

 

TAMBI Eae Enok Munaongo, 1977




1 E’YESU mshindaji wa Golgotha

1. E’ Yesus, Mshindaji wa Golgotha, twakusifu!
Bendera ya mapenzi ni Alama ya Kushinda.
Ulichukua dhambi zetu juu ya msalaba wako.
Twakuhimidi, Bwana na Mfalme! Haleluya!

 

2. Twashinda na zaidi ya Kushinda Kati’ yote Kwa
damu yako, Yesu, na Watuinua moyo .
Katika vita na ‘jaribu Twaipeleka kwa Furaha
Bendera yako nzuri ya Kushinda kati’ vita.

 

3. Mbinguni Mkombozi ni Mkuu mwenye sifa.
Aliondoa dhambi kwa Kutufilia wote.
Mwana-Kondoo wake Mungu, Umestahili
kupokea Uweza, utukufu na Heshima.
Heleluya!


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Yt2dnFzeXI8?feature=oembed&w=500&h=281]




6 TWA’SIFU Mungu kwa ajili ya damu takatifu

 1. Twa’sifu Mungu kwa ajili ya damu takatifu,
Inayotosha kuonda makosa yetu yote.
 

2.Wakristo wanakusanyika karibu ya kisima,
hawapunguki kitu kanwe, wakaa kwa Mwokozi.
 

3. Tuimbe duniani pote juu ya pendo kubwa, 
kwa kuwa tumefunguliwa kisima cha Golgotha !
 

4. Kisima hicho : Yesu kristo : na maji  damu yake.
Wasumbuka Wastarehe, Waburudishwe hapa!
 

5. Na wanye dhambi wanaitwa kwa wingi wa rehema,
Na wakosaji na maskini wasaidiwa sana.
 

6. Tumeipata tunu kubwa, Neema kwa neema.
Apokeaye fungu lake, Ni mtu wa uheri.
 

7. Heleluya! Tuna’himidi Mwenyezi na Mwanawe
Na Roho takatifu pia. Haleluya! Amina.

 




81 ALIPOKUFA Yesu ju’ ya musalaba

81

1. Alipokufa Yesu ju’ ya msalaba wake akaishinda dhambi na uwezo wa shetani. Aliniweka huru, niwe mbali na hatia; na tena atanichukua kwake.

Pambio:
Mbinguni niendako haitakuwa dhambi, ni nchi nzuri ya salama mno. Na Bwana, Mungu wetu, atatuangazia; tukusanyane sisi sote humo!

 

2.Ninafuata njia ya Mwokozi wangu sasa, aniongoza vema, anafuta kila chozi. Ananilinda katika hatari za njiani, karibu naye vita yatulia.

 

3. Mbinguni nchi yangu, na bendera ni upendo, na Roho arabuni ya urithi wangu huko; na neno lake ni chakula changu safarini; neema inanipeleka kwake.

Carl Widmark, 1912




108 MWANA-KONDOO’ wa Mungu




119 TUIMBIE msalaba wa Mwokozi

119

1. Tuimbie msalaba wa Mwokozi, damu yake inatusafisha sana! Tunaweza kuwa huru, kwani Yesu alikufa ili ku’ondoa dhambi.

Pambio:
Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!

 

2. Twafurahi kwa neema yake kubwa, alikuja ili tuwe na uzima. Kama njia ni nyembamba duniani, Yesu atatupa nguvu na ‘hodari.

 

3. Tuuimbe moto ule ‘takatifu uli’tupwa na Mwokozi duniani! Tuvipige vita vilivyo vizuri, nasi tutapewa taji ya uzima!




124 NAONA pendo kubwa mno

124

1. Naona pendo kubwa mno, latoka kwa Mwokozi wangu, ni tele kama maji mengi yatembeayo baharini. Lanitolea tumaini yakwamba nitatiwa nguvu; na niwe mhodari tena kwa pendo kubwa la Mwokozi!

Pambio:
Haleluya! Ni pendo kubwa linalotoka moyo wako! E’ Mungu wangu nakuomba: Nijaze pendo lako tele!

 

2. Na pendo hilo kubwa mno huyaondoa majivuno, na kunifunza haki kweli, uongo wote niuvue! Hunituliza moyo wangu, huruma nayo hunitia. Na sote tuwe na umoja katika pendo la Mwokozi.

 

3. Nijazwe pendo hilo kubwa, linibidishe siku zote! Rononi niwe na juhudi nitumikie Bwana Yesu! …

Hazina yako ‘nipeleke kwa watu waliopotea, wafahamishwe pendo kubwa ulilo nalo, Mungu wangu!

A. Playle, 1899




125 HALELUYA! nafurahi

125

1. Haleluya! Nafurahi, ninaimba kila siku sifa zake Mungu wangu, aliyeniweka huru. Haleluya! Bwana Yesu aliniokoa kweli! Haleluya! Mimi wake, yeye ni Mwokozi wangu!

 

2. Heri! Nilieokoka kwa neema yake kubwa ninataka kumsifu Mungu na wokovu wake. Wakinung’unika wote, sitawafuata wao; nitasifu Mungu wangu siku zote na milele.

 

3. Kama ndege waimbavyo asubuhi bustanini, Na sauti ya mawingu ivumavyo baharini, hivyo nitamshukuru Bwana wangu kwa furaha. Roho yangu itaimba: Haleluya! Sifu Mungu!

 

4. Haleluya! Furahini mbele yake Mungu wetu! Na watakatifu wote, mwimbieni jina lake! Malaika wote pia, ……msifuni Bwana Mungu! Mbingu zote zitajibu: Haleluya, Haleluya!

Einar Karlsson, 1917




126 E’MTAKATIFU Mungu wamajeshi

126

1. E’ Mtakatifu, Mungu wa majeshi, leo asubuhi tunaimba mbele yako! E’ Mtakatifu, Mungu wa rehema, Bwana Mwenyezi, tunakuabudu!

 

2. E’ Mtakatifu, huko ju’ mbinguni, lo! Wazee huzitupa taji mbele zako. Jeshi la mbinguni wanakusujudu uliye hai sasa na milele.

 

3. E’ Mtakatifu! Mtu mwenye dhambi hataweza kuuona utukufu wako. Wewe tu ni mwema, tunakuheshimu, E’ mwenye nguvu, pendo na uwezo.

 

4. E’ Mtakatifu, jina lako kubwa lisifiwe hapa chini, juu ya po pote! Mungu wa neema, nguvu na uwezo, mwenye baraka, tunakushukuru!

 

Dr. J.B. Dykes
Holy, holy, holy, R.S. 25




129 NINATAKA kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote

1. Ninataka kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote. Twende sote sasa tumsifu Yeye, na pendo kubwa la Mwokozi! Haleluya! Yu Mfalme ‘kuu!

Pambio:
Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!

 

2.Na baraka yake anaimimina, kama mvua inyeshavyo juu yangu. Nastarehe mikononi mwake Yesu, rehema yake inatosha.

 

3. Siku moja nitamwona Yesu Kristo kati’ nchi nzuri sana ya furaha, macho yangu yatamtazama yeye, kuona sura ya Mfalme.

Albert Simpson Rietz




130 NINATAKA kumsifu Yesu

130

1. Ninataka kumsifu Yesu, Bwana wangu mwema. Aliteswa hata kufa, ili niwe huru kweli.

Pambio:
Mwimbieni Bwana Yesu kwa upendo wake ‘kubwa! Alilipa deni langu, nimewekwa huru kweli.

 

2. Ninataka ‘shuhudia pendo kubwa la Mwokozi, jinsi alivyoniponya nilipopotea mbali.

 

3. Ninasifu Mwokozi kwa uwezo wake bora; naye anitia nguvu nimshinde yule mwovu.

 

4. Ninataka kumwimbia Yesu Kristo, Bwana wangu. Aliniokoa kweli, niwe heri siku zote.

Philip P. Bliss, 1838-1876




133 UFURAHI moyo wangu

1. Ufurahi, moyo wangu, heri nyingi umepata!
:/: Sikitiko limekwisha, Yesu ni wangu nami wake. :/:

 

2. Ameponya roho yangu, yeye ni mponyaji mwema;
:/: Na kwa Roho ‘takatifu anabatiza watu wake. :/:

 

3.Jina langu ni mbinguni, Yesu ameliandika.
:/: Mimi mali ya Mwokozi hata milele na milele.:/:

 

4.Na moyoni mwangu sasa ninaimba: Mungu, Baba!
:/:Ni furaha kubwa sana, nina rafiki kila saa. :/:

 

5.Nimeondolewa dhambi, nisitende ovu tena!
:/: Kwani Yesu aokoa kila wakati na dakita. :/:

 

6.Nyimbo za kusifu Mungu zinajaa mbingu zote.
:/: Moyo wangu unajibu: Amina. Mungu asifiwe» :/:

Emil Gustavsson, 1887




134 WETU wa Mungu

1. Watu wa Mungu, mshangilieni kabisa, na mwimbieni Mfalme wa mbingu na nchi! Mungu yu nasi kwa pendo kubwa, kamili ili tupate wokovu.

 

2. Ona ajabu! Mwokozi aliyejidhili! Pendo kamili na neema nyingi ya Mungu: Alizaliwa, akawa mwana Adamu, atukomboe na dhambi!

 

3. Sisi wakristo tumwimbie tena pamoja Yesu Mwokozi aliye dhabihu ya kweli! Na atukuzwe hapa na huko mbinguni, kwani alitufilia!

 

4. Yesu Mfalme, kwa pendo uliniokoa, nikufuate, nikutumikie daima! Huko mbinguni nitakusifu milele katika watakatifu.

G. Tersteegen, 1735




135 SIFU Bwana

1. Tuinue moyo tukisifu Yeye, aliyehukua (sic) dhambi zetu! Yesu, Mkombozi, asifiwe, aliyetufia sisi!

Pambio:
Yesu! Tumwabudu Yeye! Yesu! Sifu jina lake! Tuimbe kwa furaha duniani pote! Tumsifu, tumwabudu Yesu!

2. Malaika wote, msifuni Yesu! Nasi tushukuru Mkombozi! Watu wote wasikie sasa kwamba Mungu ni upendo!

3. Tushukuru Bwana Yesu, sisi sote, tukumbuke pendo lake kuu! Lisifiwe jina lake jema siku zote na milele!

Avis M. Gurgesson




136 TUINUE moyo tukisifu Yeye

1.Tuinue moyo tukisifu Yeye, aliyehukua (sic) dhambi zetu! Yesu, Mkombozi, asifiwe, aliyetufia sisi!

Pambio:
Yesu! Tumwabudu Yeye! Yesu! Sifu jina lake! Tuimbe kwa furaha duniani pote! Tumsifu, tumwabudu Yesu!

2.Malaika wote, msifuni Yesu! Nasi tushukuru Mkombozi! Watu wote wasikie sasa kwamba Mungu ni upendo!

3.Tushukuru Bwana Yesu, sisi sote, tukumbuke pendo lake kuu! Lisifiwe jina lake jema siku zote na milele!

Avis M. Gurgesson




137 NAFURAHI kwa sababu kati’ damu ya Yesu moyo umetakaswa

1.Nafurahi kwa sababu kati’ damu ya Yesu moyo umetakaswa, nimepata amani.

Pambio:
Haleluya! Haleluya! Mkombozi asifiwe! Haleluya! Haleluya! Haleluya! Amina!

2.Sina nguvu, ni dhaifu bila Yesu Mwokozi, ila kwa nguvu zake nasimama imara.

3.Moyo wangu, ufurahi, mimi mtu wa Yesu! Nampenda daima na kumtumikia.

4.Pendo kubwa la Mwokozi lanijaza rohoni. Nina raha kamili, moyo unastarehe.

5.Sifu Mungu, Baba yetu, Yesu Kristo Mwokozi, Roho Mtakatifu! Haleluya, Amina!