138 SASA tayari kwetu siku yakuokoka

1. Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka, Yesu alitimiza yote msalabani. Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao, wapate kustarehe, wapone nafsi zao.

Pambio:
Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.

2. Wewe kwa damu yako ulikomboa sisi, na jua la neema linatuangazia. Tumefahamu sasa pendo la Mungu wetu. Damu imetuunga kati’ agano jipya.

3. Njoo upesi nawe uliyesitasita! Mungu atakujaza neema yake kubwa, raha rohoni mwako inayokutuliza, matumaini, nguvu, pendo lililo bora.

H. Schlager, 1925
Speak to my soul, Lord Jesus, R.S. 567




143 HERI alisi

1. Heri halisi, Yesu ni wangu! Yeye mchunga, mimi ni wake. Heri yakini, yote ni heri, roho na moyo zimeokoka.

Pambio:
Yesu ni wimbo na raha yangu, nitamsifu hata milele! Na nitamwona huko mbinguni. Yesu ni wangu na mimi wake.

 

2.Nilijitoa kwa Bwana Yesu, na nilipewa wokovu wake. Huko mbinguni kuna furaha juu ya mtu aliyetubu.

 

3. Sasa naweza kusifu Yesu, na roho yangu inafurahi. Mimi si kitu mbele ya Mungu, bali ni heri. Namshukuru!

 

4.Nimebatizwa katika Roho, shangwe ya mbingu imo rohoni. Moto moyoni, pia kinywani, nashuhudia pendo la Mungu.

 

Fanny J. Crosby – Van Alstyne, 1873
Blessed assurance, R.S. 417

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=GwjZWPdhS_U?feature=oembed&w=500&h=281]




145 MUNGU wangu mkuu

1. Mungu wangu mkuu, wanijaza mwenyewe, na uzima u katika wewe. Nina raha moyoni na amani halisi, ninaishi katika upendo.

 

2. Sasa ninakusifu wewe, Yesu Mwokozi, unakaa rohoni daima. Kila ‘nachohitaji wanijaza kwa pendo. Wewe yote, na mimi si kitu.

 

3. Jina lako ni pendo, kulijua hakika kunafanya safari nyepesi. Mimi mtu dhaifu, ila kwako ni nguvu; niongoze katika safari!

 

4. Mbele ya uso wako giza yote yatoka; nuru inaangaza moyoni. Yamepita ya kale, sasa yote ni mapya. Ni maisha ya heri ajabu!

 

Joseph Gulseth, 1901




148 NGUVU ile ilishuka juu’ya wanafunzi

1. Nguvu ile ilishuka ju’ ya wanafunzi wote mjini mwa Yerusalem’ siku ya Pentekoste, lo! Nguvu hiyo ya Mwokozi ni sawa leo; shukuru Mungu!

:/: Karama, karama, karama yake Mungu ni sawa hata leo, ni sawa hata leo!:/:

 

2.Yesu aliwapa ahadi: «Mtapokea nguvu». Na Roho akashuka na wakamsifu Mungu. Walio wenye udhaifu, wakahubiri kwa uthabiti.

 

3. Roho yule aingiapo anatutia nguvu, tupate kwa imani ku’ kushinda yule mwovu. Kwa moyo wenye moto safi tuite watu kwa Mkombozi!

 

4.Uingie sasa rohoni, uwashe moto wako, tupate kusimama kwa usafi siku zote! Ufike sasa kama mbele wakati huo wa Pentecoste!

Leila Morris, 1862-1929
The power that fell at Pentecost, R.H. 219




158 HERI mtu anayeamini Mungu baba

 158

1. Heri mtu anayeamini Mungu Baba na Yesu Mwokozi! Heri mtu aifuataye njia nzuri ‘endayo mbinguni!

Pambio:
Usifiwe, Yesu Kristo! U Mwokozi mzuri kabisa! Usifiwe, Yesu Kristo! Bwana, nitakuona mbinguni.

 

2. Kwa furaha tunakusanyika kusikia maneno ya Mungu, na mbinguni karibu ya Yesu tutamshangilia daima.

 

3. Kuamini pasipo kuona inafaa katika safari. Siku moja atatuchukua, tutakaa milele mbinguni.

 

Tune: In the sweet by and by, R.H. 777

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=dZGuBPUDjkI?feature=oembed&w=500&h=281]

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=H6NBmX6ONrI?feature=oembed&w=500&h=281]




171 MWENYEZI Mungu ngome kuu

 171

1. Mwenyezi Mungu ngome kuu, silaha ya imara! Katika shida na huzuni twategemea yeye. Mwovu akitukaribia kututia woga, akijithibitisha kwa hila na jeuri, tusimwogope yeye!

 

2. Kwa nguvu yetu tu dhaifu, na tungeshindwa hima, ila Mwenyezi yupo nasi, twaambatana naye. Ukitaka jina lake, ndilo Yesu Kristo; aliye mshindaji na mwenye mamlaka, Mfalme wa milele.

 

3.Na dunia yote ikijaa majeshi ya giza, tuliye naye Mungu wetu, hatutaona hofu. Mwovu amehukumiwa, hana nguvu tena ya kutuangamiza maungo wala robo; ashindwa na Mwenyezi.

 

4. Maneno yake Mungu wetu, tushikamane nayo! Hatushindii vya dunia, vya juu twatafuta. Tu hodari siku zote, hata hatarini; uzima twauweka kutii Mungu wetu: Ufalme una yeye.

M. Luther, 1528
A mighty fortress is our Gud, R.H. 431




208 PIGA makengele ya furaha leo kwa sababu mutu ametubu

208

1. Piga makengele ya furaha leo kwa sababu mtu ametubu! Mwana mpotevu amerudi sasa, baba amemsamehe yote.

 

2.Nyimbo za furaha ya mbinguni, Nyimbo za furaha ya wakristo! Tuna’sifu Mungu kwa sababu sasa mtu huyu amwamini Yesu.

 

3. Piga makengele, ni furaha nyingi; mkosaji amefunguliwa! Yesu alivunja minyororo yake, alimpa roho ya kimwana.

 

4. Piga makengele! Hiyo ni habari yakupasha mbali na karibu. Mtu amepata kuwa mtu mpya, dhambi zake zimeondolewa!

W.O. Crushing




215 MWENYEZI Mungu anafanya ishara kubwa Duniani

215

1. Mwenyezi Mungu anafanya ishara kubwa duniani, anaondoa minyororo inayofunga watu huku. Avunja nyavu za shetani, na wakosaji waokoka.

 

2. Maneno yake yana nguvu kushinda yote ya zamani. Na watu wanapiga mbio kuomba ne’ma ya Mwokozi. Wakiyapata masamaha, waimba wote: “Sifu Mungu!”

 

3. Tazama, ndugu wengi sana wanafuata Yesu leo; katika kila nchi sasa maelfu wanapenda Mungu. Wengine wanavutwa naye Mwenyezi Mungu, Baba yetu.

 

4.Inua macho, mvunaji, mavuno yanaiva sana! Uende kutafuta watu, uwapeleke kwake Yesu! E’ ndugu wote, amkeni, ‘kawaokowe wenye dhambi!

 

5. Wengine wanapoingia ufalme wako, Yesu Kristo, nisibakie huku chini, neema hiyo nakuomba! Nakaa mikononi mwako, unifikishe huko kwako!

 

6.Najua siku ni karibu Mwokozi atakaporudi, awachukue watu wake mpaka nchi ya amani. E’ siku ya uheri bora, nakutamani. Uje mbio.

Nils Frykman, 1877




246 HESHIMA na sifa zina Baba mbinguni

246

1. Heshima na sifa zina Baba mbinguni, aliyetupenda zamani na sasa!

Pambio
Haleluya, usifiwe! Haleluya, amina. Haleluya, usifiwa! Haleluya, amina.

 

2. Heshima na sifa zina Yesu Mwokozi, alitufilia kwa’jili ya dhambi!

 

3. Heshima na sifa zina Roho wa kweli, anashuhudia Mwokozi na damu!

W.P. Mackay, 1863




247 NAPENDA sana kumushukuru Mwokozi

247

1. Napenda sana kumshukuru Mwokozi wangu kwa nia huru; kwa wimbo wangu nashuhudia upedo wake na damu pia.

 

2. Nikishukuru mateso yake msalabani na kufa kwake, nataka katika wimbo wangu kumtolea shukrani yangu.

 

3. Naimba sasa, nina faraja, katika Yesu nina faraja. Ni mambo tunayofunuliwa, kwa wenye dhambi yamefichwa.

 

4. Kwa neno lake ananiambia kwamba ananihurumia, na ukombozi ninao sasa kwa damu iliyonitakasa.

 

5. Na msione ajabu sana ya kuwa namshukuru Bwana! Ninamwimbia kidogo sasa, ‘taendelea mbinguni hasa.

 

6. Anipa vyote kwa pendo lake, urithi wangu wachungwa kwake hata wakati wakuhamia mbinguni, na nitashangilia.

Anders Nilsoon




249 ZAMANI mjini mwa Yerusalemu

249

1. Zamani mjini mwa Yerusalemu waisrael’ waliabudu. Wakristo wa sasa wanakusanyika kuomba, kusifu Mwokozi.

Pambio:
Msifuni, msifuni Mungu wetu, kwani ametutendea mema! Tutamsifu tu aliyetoka ju’, shangilieni Mwokozi mwema!

 

2. Mwokozi yu nasi, ame’fumbulia uweza wa kutuokoa. Na yu mwaminifu, atusikiliza, apenda kutupa baraka.

 

3. Twaomba baraka na mvua ya mbingu kuithibitisha Injili! Wagonjwa wapone, vipofu waone, Tupate ‘batizo wa Roho!




252 NINAKUSHUKURU Mungu kwa fadhili

252

1. Ninakushukuru Mungu kwa fadhili zako zote, kwa furaha na uchungu, kwa neema njia yote! Kwa kipupwe na masika, kwa wakati wa machozi. Na kwa raha kadhalika na’shukuru Mkombozi!

 

2. Ninakushukuru Bwana kwa kunifunua siri, kwa kusikiliza sana, ombi na kulifikiri! Na kwa msaada wako, kwa wakati wa jaribu. Kwa agano la Mwanako nashukuru! U karibu.

 

3. Nashukuru wewe pia kwa uzuri wa mbinguni, nuru ulioitia, na kwa jambo la huzuni! Kwa jaribu na kwa giza na kwa siri ya imani, tena kwa kunijaliza ninakuwa na shukrani!

 

4. Kwa waridi za njiani na miiba yao pia, kwa mahali pa amani uliopotuandalia, kwa agano la upendo, kwa kutupa tumaini, kwa kifiko cha mwenendo: Nashukuru! U amini!

Augut Storm, 1891

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=4Z8qtBi6IDY?feature=oembed&w=500&h=281]

 




267. BABA nakuomba leo na mapema

267

1. Baba, nakuomba leo na mapema: Niongoze pote kwa mapito meme!

Pambio:
Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

2. Nistahimilipo kazi za mchana, unitie nguvu, nakuomba, Bwana!

 

3. Hata jua kuchwa liagapo njia, Baba, nakuomba: Unilinde pia!

 

4. Maadui wengi watuwindawinda, kwa maisha yetu Mungu ni mlinda.

 

5. Katika utoto na ujana tena, ne uzee pia: omba, kesha, shinda!

A. Cummings




278. NINAINUA macho yangu ka Mungu

278

1. Ninainua macho yangu kwa Mungu aketiye juu, aliye msaada wangu, njiani pangu nuru kuu. Aliyefanya yote, maombi huyasikia. Katika njia zangu zote atanilinda pote pia.

 

2. Bwanangu asiache tena mguu wangu usogezwe, kwa kuwa ni mlinzi mwema, naye hatasinzia kamwe. Alinda roho yangu nisije nikapotea. Hitaji za maisha yangu baraka yake ya’enea.

 

3. Aniokoa na uovu, na roho yangu imepona. Kwa yeye nguvu na wokovu, nilizionja naku’ona. Ananilinda pote: kutoka na kuingia; anijaliza mema yote hata nakutumainia.

J. Arrhenius, 1694




292. KATIKA damu takatifu

292

1. Katika damu takatifu ya Mwokozi wangu nimesafishwa. Na nguvu ya Mwokozi wangu tu yaweza kunilinda safi.

Pambio:
Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya wokovu na nguvu ya kushinda! Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya wokovu wote!

 

2. Kwa wingi wa neema yake tu nimeokoka, nimeokoka. Wokovu ni kwa ‘jili yako na kwa kila ‘aminiye kweli.

 

3. Kwa nguvu zangu sitashinda na siwezi neno, siwezi neno. Ila Yesu anayenifahamu atanisaidia pote.

 

4. Babangu mwema ananipenda na ananilinda, ananilinda. Sitaogopa giza huku kwa maana yu pamoja nami.

Otto Witt/ C.H. Morris




295. E’FURAHENI watu wake Mungu

295

1. E’, furahini watu wake Mungu! Mwokozi wetu alituokoa. Neema kubwa, pendo la ajabu! Tusifu Mungu sana siku zote!

Pambio:
E’ Mungu ana mamlaka yote, ni ngao na makimbilio yangu; Ni Baba yangu, na anasikia maombi yangu. Asifiwe!

 

2. E’, furahini watu wake Mungu! Tuimbe nyimbo za furaha nyingi! Tusiogope ila tumwamini na twende mbele kwa uweza wake!

 

3. E’, furahini watu wake Mungu! Tukimahangilia (sic) Mungu wetu, jirani zetu wasioamini watatamani kumjua Yesu.

 

4. E’, furahini watu wake Mungu! Mfalme wetu yu pamoja nasi. Kitambo bado- na tutahamia mbinguni kwake Mkombozi wetu.




298. NINAO wimbo wakunifurahiya

298

1. Ninao wimbo wakunifurahisha wa Mwokozi, wa Mwokozi. Namshukuru kwa roho yote pia, Mwokozi mzuri ninaye!

Pambio:
Mwokozi – wimbo wangu, Mwokozi, Mwokozi! Mahali pote na siku zote nitamsifu Yesu kati’ yote. Mwokozi ni wimbo wangu wa huku na Mbinguni.

 

2. Na jina moja ni lenye pendo tele: Yesu, Yesu, ndilo jina! Anipa yote niliyokosa mbele, Mwokozi mzuri ninaye.




300. MUNGU abariki nyote

300

1. Mungu awabarikie nyote na awe pamoja nanyi! Awalinde kwa amani! Mungu n’awe nanyi siku zote!

Pambio:
Mungu n’awe nanyi daima hata mwisho wenu wa safari! Mungu n’awe nanyi daima hata tuonane huko juu!

 

2. Mungu wetu awalinde pote na kuwahifadhi vema kwa mikono ya rehema! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

3. Mungu awaangazie nuru, na awashibishe sana kwa fadhili zake Bwana! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

4. Mungu awainulie uso! Na wakati wa kuhama mpelekwe kwa salama! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

5. Mungu awabarikie nyote, awalinde m-we huru, awaangazie nuru! Awainulie uso wake!

J.E. Rankin / Daniel Hallberg
God be with you till we meet again, R.S. 942; R.H. 722