79 MAISHA mafupi yahuku dunia

79

1. Maisha ya mtu [mafupi] ya hapa dunia yanaifanana safari chomboni. Twapita bahari katika hatari, lakini Mwokozi anatuongoza.

Pambio:
Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.

 

2. Twapita katika baridi na pepo, maneno ya Mungu ni nuri gizani. Hatari na hofu na chombo kibaya hatuta’kumbuka karibu na Yesu.

 

3.Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu, tunakaribia bandari upesi. Na humo hakuna dhoruba na pepo; safari tutaimaliza salama.

 

4. Tutakapofika bandari ya mbingu tutamshukuru Mwokozi mkuu. Hatutaziona hatari na hofu karibu na Yesu mwenyewe mbinguni.




140 UKICHUKULIWA na mashaka yako

1. Ukichukuliwa na mashaka yako na kuona hufu kwamba utakwama, uhesabu mibaraka yake Mungu, na utashangaa kwa rehema yake.

Pambio:
Uhesabu mibaraka yote Mungu aliyoyakubariki! Ukumbuke mambo yote pia, na utashangaa kwa rehema yake!

 

2. Na ukiudhiwa na huzuni nyingi, ukiona msalaba ni mzito, uhesabu mibaraka kuchwa pia, na kwa moyo wote utasifu Mungu.

 

3. Wengi watamani mali ya dunia; utajiri wako ni Mwenyezi Mungu. Uhesabu mibaraka na kumbuka: Mali haiwezi kufungua mbingu.

 

4. Na katika mambo yote huku chini ukumbuke pendo kubwa la Mwokozi! Na ujumlishe mibaraka yote, tena mwisho atakuchukua kwake!

Johnson Oatman Jr
When upon life’s billows, R.S. 5


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=1VWWUGwVSTU?feature=oembed&w=500&h=281]

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=-zQDFxB8ZU0?feature=oembed&w=500&h=281]



173 MAISHA katika dunia

173

1. Maisha katika dunia ni kama kupanda na ‘vuna: Apandaye katika mwili atavuna uharibifu; tukitumikia Mwokozi tutapata thawabu mbinguni; yafaa kuishi na kufa katika maneno ya Mungu.

 

2. Kwa neema kubwa kabisa tumekubaliwa na Mungu, kwa neema kubwa zaidi twapata kumtumikia. Kuishi kwa ‘jili ya Yesu kati’ yote ya dunia hii na kuitangaza injili ni faida kwetu kabisa.

 

3. Wakristo wata’poingia mbinguni kusifu Mwokozi, na mimi nataka kufika kuimba pamoja na wao. Tutamshukuru Mwokozi aliyetununua kwa damu; waliohudumu kwa pendo watamhimidi milele!

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=clHjbEJYgQM?feature=oembed&w=500&h=281]




186 FANYIA Mungu kazi

186

1. Fanyia Mungu kazi, mbio usiku waja! Mtumikie Mungu siku zako zote! Anza mapema sana, dumu mchana kutwa! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

2. Fanyia Mungu kazi kama kungali jua, usipoteze bure siku zako huku! Uyatimize yote bila kukosa neno! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

3. Fanyia Mungu kazi, saa yapita mbio! Fanya bidii sana kuokoa ndugu! Mtumikie Mungu kwa nguvu yako yote! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

T. Annie L. Coghill, 1854 M. Lowell Mason, 1864
Work for the night is coming, R.S. 429

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Hc9BgKGWv8o?feature=oembed&w=500&h=281]




238 NIFANANISHWE nawe mwokozi

238

1. Nifananishwe nawe Mwokozi, ni haja yangu iliyo kuu. Ninakuomba, na kwa machozi, nikufuate, Bwana wa juu!

Pambio:
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye upendo, safi halisi! Unitakase, unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!

 

2. Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye rehema, pendo ajabu! Niwapeleke kwa Mkombozi walioshindwa na majaribu!

 

3. Nifananishwe nawe Bwanangu, Mtakatifu, mwenye saburi! Niwe mnyofu kazini mwangu, mtu thabiti bila jeuri!

 

4. Nifananishwe nawe Mwokozi! Nimiminie pendo moyoni! Nibadilishe, e’ Mkombozi, niwe tayari kwenda mbinguni!

Thomas O. Chisholm, 1866-1960
O , to be like thee, blessed Redeemer, R.H. 412




276. MATENDO ya Mungu yapita fahamu

276

1.  Matendo ya Mungu yapita ‘fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.

 

2.Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?

 

3. E’ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama mbinguni!

 

4.Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ‘takwisha, milele nitashangilia.

 

5. Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye neema katika shauri na tendo.

 

6.Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao mbinguni.

 

Emil Gustavsson, 1886

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Livecgf5aQA?feature=oembed&w=500&h=281]




291. MIMI mwenye hatiya nilikombolewa

 291

1. Mimi mwenye hatia nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa. Dhambi zangu na zako alizichukua, kwa damu aliniokoa.

Pambio:
Dhambi zimetundikwa msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.

 

2. Yesu mwenye upole na mwenye upendo ananitakasa rohoni. Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, alikufa msalabani.

 

3.Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, kwa kuwa alinifilia. Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda, daima nakushangilia.

Carrie E. Breck, 1855-1934
There was One who was willing to die in my stead, R.S. 737

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=qXvsR4Oo6io?feature=oembed&w=500&h=281]