4 USIKU kabla yakuteswa

1. Kabla ya kuteswa, Yesu Alikusanya wanafunzi wake; Alifahamu kwamba saa yake ya kutolewa ilikaribia.

 

2. Kwa roho aliona gethesemane, Meteso yake na huzuni nyingi;  Zaidi alihofu saa ile, ata’poachwa hata naye Mungu.

 

3. Alitamani saa ya pasaka pamoja na wapendwa wake huku. Katika pendo lake kubwa sana Aliyashinda majaribu yote.

 

4. Akautwa’ mkate, aka’mega, Twaeni, mle, hu’ ni mwili wangu!  Na akawapa wanafunzi wake. Wa heri kila mtu aminiye.

 

5. Ba’daye akawapa na kikombe, Na akasema: Nyweni nyote hiki! Ni damu yangu inayomwagika kwa ondoleo la makosa yote.


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=xaJOREk2_oY?feature=oembed&w=500&h=281]




54 USIOGOPE mateso yako

54

1. Usiogope mateso yako, Mungu anakulinda, bali tazama mapenzi yake,

Pambio:
Mungu anakulinda Mungu anakulinda siku kwa siku njiani mwake. Anakulinda salama. Mungu anakulinda.

 

2.Ukichukuwa mizigo ‘zito, Mungu anakulinda, kati’ hatari za njia yako Mungu anakulinda.

 

3. Anakumbuka hitaji zako, Mungu anakulinda. Utashiriki ujazi wake, Mungu anakulinda.

 

4. Katika njia ya migogoro, Mungu anakulinda. Mfunulie fadhaa zako, Mungu anakulinda.

Cevilla D. Martin, 1904
Be not dismayed, R.H. 458

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Dl89FTY2gaU?feature=oembed&w=500&h=281]




75 NILIE msafiri

75

1.Niliye msafiri, mgeni duniani; sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni. Ninatamani nami kukaa siku zote pamoja naye Baba katika utukufu.

Pambio:
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri wa binguni wapita yote huku.

 

2. Mwokozi yuko huko, rafiki yangu mwema, aliyenikomboa na ku’chukua dhambi. Na hata nikiona furaha siku zote ningali natamani makao ya mbinguni.

 

3.Na nikipewa huku vipawa vya thamani, na wakiimba nyimbo za kunifurahisha, rafiki wangu wote wakipendeza mimi, ningali natamani makao ya mbinguni.

 

4.Upesi nitaona kifiko cha mbinguni, Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha; Na huko nitaona nilivyotumaini, kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.

Lina Sandell-Berg, 1868
Home, home, sweet home


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=RMNKXUgJql4?feature=oembed&w=500&h=281]




275 E’MUNGU mwenye haki

275

1. E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku katika mambo yote yanayokupendeza! Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka yananitia tetemeko mpaka kufa.

 

2. Ni heri siku zote kutegemea Yesu na kuenenda sawa katika nyayo zake, kwa kuwa yeye ni Mchunga anayeniongoza vema, nipate kuingia katika raha yake.

 

3. Safari yangu sasa yaelekea mbingu, Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko na siku nitakapofika ‘tashangilia kwa furaha kuona yeye aliyeninunua kwake.

 

4. Ulimwenguni humu, matata na kuchoka. Nikihitaji kitu nafadhahika bure, lakini siku ile kuu nita’pomwona Mwokozi, natumaini sitakosa dhawabu yangu!

 

5. Mbinguni sitaona adui zangu tena. Hayatakuwa mambo yakupokonya pale. Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya! Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu!


Video imeimbiwa na METHUSELA Bushambale na DAVID IMANI

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=IyxLpC7tyaw?feature=oembed&w=500&h=281]

THAMBI




291. MIMI mwenye hatiya nilikombolewa

 291

1. Mimi mwenye hatia nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa. Dhambi zangu na zako alizichukua, kwa damu aliniokoa.

Pambio:
Dhambi zimetundikwa msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.

 

2. Yesu mwenye upole na mwenye upendo ananitakasa rohoni. Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, alikufa msalabani.

 

3.Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, kwa kuwa alinifilia. Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda, daima nakushangilia.

Carrie E. Breck, 1855-1934
There was One who was willing to die in my stead, R.S. 737

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=qXvsR4Oo6io?feature=oembed&w=500&h=281]