10 DAMU yako yenye baraka inayotuosha makosa

1. Damu yako yenye baraka Inayotuosha makosa.  

Ilitoka musalabani, Bwana YESU, alipokufa alipokufa.  

Nastahili pata hukumu, Na siwezi mimi kujiosha.  

Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa!

Refrain:
Safi, Safi kweli, Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa!

 

2. YESU ulivikwa miiba, kuangikwa juu ya mti.  

Ulivumilia mateso, Maumivu na majeraha.  

Ninataka kijito hicho N’ende na nikasafishwe sana!  

Unioshe katika damu, Nipate kuwa safi kabisa.

 

3. BABA kweli nina makosa, moyo wangu wa udhaifu;

mimi mwenye dhambi rohoni nitaona wapi mwokozi?

yesu kwako msalabani naja ninakuamini sasa.

unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa.

 

4. BWANA, nimefika karibu, unilinde kwako,

mille! ufungue kila kikamba, unijaze moyo mwenyewe!

na karibu ya msalaba nitakaa hata kufa kwangu.

unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa.


 

Comments

4 responses to “10 DAMU yako yenye baraka inayotuosha makosa”

  1. muhongya.kiro Avatar

    thanks a lot for the work
    be blessed

    1. Nyimbo Za Wokovu Avatar

      To God we give glory,
      Be blessed too dear Kiro

  2. Mlasi Avatar
    Mlasi

    Asante sana kwa nyimbo hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

HTML Snippets Powered By : XYZScripts.com