1. Mwokozi ameutimiza wokovu kwa neem kubwa,
Na juu ya mwamba wa Neno la Mungu Najenga imani.
Refrain:
Aliniokoa kabisa! Kwa damu alinisafisha.
Ninamshukuru Mwokozi kwa sababu Alinikomboa hakika !
2. Mzigo wa dhambi aliuondoa kwa neema kubwa.
Naona Furaha rohoni kabisa, Amani ya Mungu.
3. Naweza kukaa mweupe rohoni kwa neema kubwa;
Na roho ya Mungu ananiongoza Njiani daima.
4. Karibu na Yesu nalindwa salama Kwa neema kubwa.
Ahadi za Mungu zanipa Furaha iliyo kamili.
Leave a Reply