100
1. Lo! Bendera inatwekwa, yatutangulia! Tusione hofu, wenzi, twende kwa kushinda!
Pambio:
Bwana Yesu atakuja, tuilinde ngome! Kwa uwezo wake Yesu tutashinda yote.
2.Ibilisi azunguka, akitutafuta; anataka tuanguke, tufe, tupotee.
3. Vita kubwa, vita kali inaendelea, tuwe watu wa ‘hodari! Twende, tutashinda!
4. Basi, kwa bendera yake tunashikamana. Atutie nguvu yake hata kuja kwake!