1. IKIWA wananiuliza msingi wa uzima je?
twahitaji kuongeza kwa kazi yake Yesu?
Kwa uhodari nitajibu: msingi wangu ni wa nguvu,
ni damu yake Yesu Kristo inatosha sana.
2 UMWAMBA wa zamani sana, Daima utadumu.
Na hata siku nita’kufa, nitautegemeya.
Nitakapoondoka huku, nitaimbia majeraha
na damu ya mwokozi wangu, Funguo la mbingu.