113
1. Msalabani Mwokozi wangu alijitoa kuniokoa, na damu yake ilimwagika kwa’jili yangu, kunikomboa.
Pambio:
E’ Golgotha, e’ Golgotha, alipoteswa Bwana Yesu! E’ Golgotha, e’ Golgotha, nilipopata raha kweli!
2. Na nchi ile ilitetema, mbinguni jua likafunikwa wakati Yesu alipokufa, akichukua hatia yangu.
3. Likapasuka pazia lote, kwa hiyo neno limetimizwa. Naona njia ya mbingu wazi: Nikutakaswa kwa damu yake.
4. Mwokozi wangu, upendo gani: Uliutoa uzima wako! Kunikomboa ulisikia mateso yote ya msalaba.
William Darwood, 1886
On Calvary’s brow, R.S. 153