1. Uzima ninao moyoni daima, uzima ni Yesu Mwokozi, aliyeingia rohoni hakika, akanitilia ‘hodari.
Pambio:
Nashiba rohoni kwa raha ya Mungu, na moto wa mbingu ulimo. Napata kukaa nuruni kabisa, na nuru ni Yesu Mwokozi.
2. Baraka zilizo katika wokovu nilizozipata kwa bure, nilipoungama makosa na dhambi kwa Yesu Mwokozi wa wote.
3. Mwokozi aliniondoa porini, natunzwa shambani mwa Mungu. Na sasa kwa mvua na jua la mbingu ninamzalia matunda.
4. Naona maisha ni yenye maana: Ni ku’tumikia Mwokozi. Kuishi ni Kristo na kufa faida kwa kila mkristo wa kweli.
Video ya sauti