Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

333 Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita. Mara nyingi twapata shida, kwani miaka yapita. Tukimwamini Yesu na kumtumikia, tutapata thawabu, kwani miaka yapita.

Pambio:
Yapita, yapita, yapita, yapita, tumikieni Mwokozi, kwani miaka yapita.

 

2. Hatutaogopa kitu, kwani miaka yapita. Bali tutafurahi tu, kwani miaka yapita. Dunia ni shida, mashaka na huzuni. Bali tukaze mwendo, kwani miaka yapita.

 

3. Rafiki wanatuacha, kwani miaka yapita. Na safari itaisha, kwani miaka yapita. Tupande mbegu njema, rohoni mwa wenzetu, wengine waokoke, kwani miaka yapita.

 

MUBIKWA Onesimo, 1963

No comments yet.

Leave a Comment