1. Yesu Kristo asifiwe! Alizichukua dhambi,
Ne’ma inatoka kwake kati’ damu.
Umeosha moyo wako, umekuwa safi,
huru umeondolewa dhambi kati’ damu?
Refrain:
:|: Kati’ damu :|: Umeosha moyo wako, umekuwa safi, huru?
:|: kati’ damu :|: Umcondolewa dhambi kati’ damu?
2. Ukilia, ukijuta dhambi hazitoki kamwe;
Haki kweli uta’pata kati’ damu.
Mambo yakusumbuayo Yesu a’ondoa mara,
Unapata ukombozi kati’ damu.
3. Yesu atatuchukua arusini mwake huko.
Umevikwa nguo safi kati’ damu?
Je, wajenga ju’ ya mwamba, moyo wako u mzima,
unashinda kila saa kati’ damu?
4. Bwana Yesu asifiwe! Aliloa damu yake,
na kwa damu ya thamani tutashinda.
Asubuhi kubwa ile vita itakapokwisha,
tutaimba kwa Furaha ju’ ya damu.