1. Sawa na wapitaji wa dunia. Tunapita huzuni na shida. Siku moja tutaongozwa naye, hata huko mbinguni kwa Baba.
Pambio:
Sawa nyota za mbingu tutang’aa, kwa Yesu Mwokozi mbinguni. Tuishike safari kwa nguvu, na kusifu Mwokozi kwa nyimbo.
2. Hatushinde katika dunia, kwa kupewa dhahabu na fedha, ila tunatazama shabaha, ni mjini mbinguni kwa Baba.
3. Tukikaa nyumbani wala hema. Tangu utoto hata mauti. Tuna ahadi, kuongozwa naye, kwamba tutafikishwa kwa Baba.
MUBIKWA Onesimo, 1963