1. Naiamini damu yako yesu na msalaba wako Yesu.
Mwokozi wangu wa pekee napata yote, Napata yote kwako.
Refrain :
Uliyoyahidi Na’pata kwa imani.
Huwezi kuniacha mimi, Napata yote kwako.
2. Kwa damu nimetasika, Namto wa uzima wako
waniletea nguvu tele, napate yote kwako. [br]
3. Nafungwa kwa upendo wako, Njiani unaniongoza,
Na katika hatari zote napat nguvu kwako. [br]
4. Ninakupenda, Bwana Yesu, Wanisikia niombapo,
Wanipa jibu la mombi Napata yote kwako.